Piga chini mahusiano yanayokutesa na usonge mbele

Piga chini mahusiano yanayokutesa na usonge mbele

Equation x

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2017
Posts
33,679
Reaction score
49,841
Mapenzi yanatakiwa yakupe furaha ya kimwili, akili na kiuchumi.

Sasa utakuta mtu ameingia kwenye mahusiano, ghafla uchumi unayumba; fedha hazipatikani tena, madeni yamekuwa mengi, kila kona ukipita unadaiwa.

Mara kurukwa na akili na kujikuta unaongea mwenyewe mwenyewe barabarani, ukiwa kwenye kikao unashinda kuongea pointi kutokana na changamoto ya magonjwa ya akili.

wakati mwingine unavaa mavazi yaliyochakaa, mkanda umepauka, viatu vimepauka, soli ya kiatu inaenda upande; mipango ya kimaendeleo ya kufungua biashara ujenzi n.k yote imekufa.

Na haya yote, unakuta yameanza ukiwa kwenye mahusiano; kabla ya mahusiano hayakuwepo.

Sasa, kwanini ubaki kwenye mahusiano ya namna hiyo, yanayokutesa?

Piga chini na usonge mbele.​
 
Mahusiano yenye upendo, unyenyekevu na utii kamwe hayawezi yaka watesa wapendanao, na badala yake huruma na msamaha vinachukua nafasi kubwa zaidi katika wakati huo...😊
And thi's why I'm always happy....🤗
Changamoto kwa wenzetu, wanasukumwa kuingia kwenye mahusiano kutoka na changamoto za kiuchumi; watakao bahatika kwa uchache kupata mtu sahihi ndio kama ulivyoshuhudia.
 
Back
Top Bottom