Piga Kura: Mtandao Gani Wa Simu Inaongoza Kwa Wizi

Piga Kura: Mtandao Gani Wa Simu Inaongoza Kwa Wizi

brasy coco

JF-Expert Member
Joined
Apr 25, 2012
Posts
1,489
Reaction score
900
Ndugu;

Watanzania Katika Nchi Kuna Mitandao Tofauti Ya Simu Leo Ni Nafasi Yako Ewe Mtanzania Kupiga Kura Ya Kampuni Gani Inaongoza Kuwaibia Watanzania Tena Walala Hoi Na Wasio Walalahoi.

Mchezo huu Upo Sote Tunajua Hakuna Asiyejua Juu Ya Wizi Wa Hawa Jamaa ZETU ivyo Basi Katika Mitandao Ifuatayo Upi Unaongoza Kwa Wizi??????

#Airtel
#Vodacom
#Tigo
#Zantel
#Sasatel

Kura Yako Itahesabiwa Na Kupelekwa Mamlaka Husika.

Nawasilisha
 
Tigo wanatisha,juzi walinikopesha sh 180/-,jana nimeongeza salio wakakata sh770/.
 
Tigo wanaoongoza
tena umenikumbusha ngoja nikanunue zantel niwatupilie mbali hawa wezi
 
airtel ni kiboko yao. matangazo yao hayaendani kabisa na huduma halisi. kwenye internet ndio kabisa wanaiba. wezi sana.
 
yaani mwana umelonga kabisa yaani airtel na tigo ni wezi kabisa jamani ukikopa kwa tigo niwezeshe kama sh450 unakatwa 750 jamani huu sio wizi mtupu, na airtel katika mtandao wa internet ndo wezi kabisa yaani we acha mwana sijui nasi tuzindue jf mobile phone yetu? @brass coco
 
Vodacom ndo wezi wakuu. Kesho wasiponirudishia 10,000/- au bomba 7 yangu nafungua new thread kuanika uozo wao.
Customer care kwenye namba hii 15366 ni hovyo na wanalijua suala la wizi huu.
 
mimi ni mteja wa muda mrefu wa airtel, lakini kwa sasa wanibore sana, gharama zao za upigaji simu ziko juu sana, hivi kweli ktk ulimwengu wa mkonga bado tunalipia sh.6 kwa dakika kama sio wizi nini sasa, halafu eti wanatangaza senti 10 kwa sekunde eti ni gharama nafuu.

mimi nawaomba wapunguze gharama zao za kupiga simu, kwanini isiwe shilingi 1 kwa dakika
 
Vodacom ndo wezi wakuu. Kesho wasiponirudishia 10,000/- au bomba 7 yangu nafungua new thread kuanika uozo wao.
Customer care kwenye namba hii 15366 ni hovyo na wanalijua suala la wizi huu.

Pole sana mkuu,ulikuwa unanunua kwenda namba nyingine?
 
mimi ni mteja wa muda mrefu wa airtel, lakini kwa sasa wanibore sana, gharama zao za upigaji simu ziko juu sana, hivi kweli ktk ulimwengu wa mkonga bado tunalipia sh.6 kwa dakika kama sio wizi nini sasa, halafu eti wanatangaza senti 10 kwa sekunde eti ni gharama nafuu.

mimi nawaomba wapunguze gharama zao za kupiga simu, kwanini isiwe shilingi 1 kwa dakika

Mkuu,shilingi 1 kwa dakika?
 
Vodacom ndo wezi wakuu. Kesho wasiponirudishia 10,000/- au bomba 7 yangu nafungua new thread kuanika uozo wao.
Customer care kwenye namba hii 15366 ni hovyo na wanalijua suala la wizi huu.
Mkuu, hawa mbwa kwenye ishu ya vifurushi mi wameniliza mara kibao tu
 
aisee TIGO ni wezi aiseeee..kha...ila sijui wameniwekea nini ...nashindwa kuwahama..........
 
Kwanza kabisa nakushukuru wewe mleta thread, lakini pia naomba huu ujumbe ufike huko ulikotuambia kuwa unaupeleka. Ama baada ya hayo napenda kuutaarifu uma kuwa hawa vooodaa hawa, ni wezi wezi hakuna tena hadi wananifanya nitamani ningekuwa hacker/crecker wanikome pu..........mbav zao(samahani lakin). Hebu fikiria, mtu unanunua kifurushi letb say cha mb50 halafu ile unafungua browser hata kabla haijafunguka wanakutumia meseji kuwa salio limekwisha hivyo uongeze salio, hii haki kweli? Nsiseme sana nsije nkajitafutia bani bure mie
 
ukinunua mb50 voda ufingua kubrowse JF kabla haujalogin wanatuma ujumbe bundle yako imeisha ukiwapigia wanakuambia hzo bundle za kwenye sim
 
Voda wezi, lakini ndiyo hivyo wako kama CCM wamekamata akili za wateja wao!.
 
Back
Top Bottom