Pigana na umasikini

prosper cliff

JF-Expert Member
Joined
Jan 19, 2017
Posts
661
Reaction score
695
PIGANA NA UMASKINA NA NJAA KWA KUTUMIA SUPER GRO:
ANGALIZO:
Super gro hutumika sambamba na mbolea pamoja na dawa ya kuua wadudu.
Super gro ni bidhaa maarufu sasa duniani na hasa nchi za Afrika mashariki, ni kwa namna ambavyo imeweza kumsaidia mkulima kuongeza mazao na kupunguza gharama za kilimo hasa madawa na mbolea.

Ni bidhaa bora kutoka kampuni ya kimataifa inyoitwa GNLD (Golden Neo Life Diamite International kutoka Marekani. Imesajiliwa inafanya biashara Tanzania kama kampuni yoyote ya kibiashara tangu April 1999’

UFUATAO NI MWONGOZO WA NAMNA YA KUTUMIA SUPER GRO:
Mwongozo huu umeandaliwa ili utumiwe na wakulima na sio msingi wa majadiliano ya kisayansi, taarifa za kisayansi zimeshatolewa na bodi ya wanasayansi washauri wa GNLD ambao ndio nguzo ya GNLD katika utafiti, utengenezaji na uendeshaji, uimamizi na uboreshaji wa bidhaa zote za GNLD, Super gro imesajiliwa na mkemia mkuu wa serikali.

Taarifa hii imetolewa kama mwongozo rahisi shambani. Mwongozo huu umeandaliwa kutokana na uzoefu uliopatikana kwa wakulima wenyewe baada ya matumizi ya muda mrefu kutoka sehemu mbalimbali za Uganda, Kenya, Iringa Dodoma hasa Kilosa, Mbeya, Kilimanjaro .
MAHINDI

Loweka mahindi kwenye mchanganyiko wa cc moja ya Super Gro na maji lita moja, kwa saa sita. Panda kati ya futi (lula) moja na nusu na futi mbili kila upande mbegu. Weka mbegu mbili kila shimo. Puliza mchanganyiko wa Super Gro na maji (CC 1 KWA LITA 1 MAJI) baada ya mahindi kuota yakiwa na majani wawili hadi manne au urefu wa nusu futi.

Utaendelea kupuliza mara moja kila baada ya wiki mbili kama ni wakati wa mvua na mara moja kwa wiki kama kuna ukame. Puliza kwenye majani na ardhi kuzunguka shina. Inashauriwa kuchanganya na dawa za kuua wadudu kama kuna mdudu, endelea kupuliza mpaka mahindi yatakapotoa Super Gro mahindi yana uwezo wa kutoa hindi baada ya wiki 6 na yatakuwa tayari kuvunwa yakiwa mabich baada ya miezi 3.

Uzoefu wa wakulima.
Matokeo ya kutumia Super Gro Uganda.
ENEO
MASAKA
MITYANA

MAHINDI YALIYOPANDWA
KILO 50
KILO 1,000

MAHINDI YALIYOVUNWA
KILO 6,000
KILO 13000

MTAMA (MILLET)
Loweka usiku kucha panda kama yalivyo mahindi
KARANGA (GROUND NUTS)

Loweka kwa saa 6 tu, panda katika mstari kati ya nusu futi ( nusu lula) kila upande na mbegu moja kila shimo. Puliza mchanganyiko wa Super Gro na maji (cc 1 kwa lita 1 ya maji) baada ya kuota mara 1 kila baada ya wiki moja wakati wa ukame na mara 1 baada ya wiki 2 wakati wa mvua. Acha kupuliza mara zinapoacha kutoa maua.

VIAZI VITAMU (SWEET POTATO)
Loweka(mche) sehemu ambayo utaizika ardhini ndio iingie kwenye mchanganyiko wa Super Gro (cc 1 kwa lita 1 ya maji) kwa saa 12, siku tatu baada ya kupanda puliza mchanganyiko kama mwanzo, juu ya tuta la viazi endelea kupulizia mara 1 kila wiki wakati wa ukame na mara 1 baada ya wiki mbili wakati wa mvua.

Acha kupuliza baada ya majani kutambaa na kufikia tuta la pili yake. Kutoka watumiaji wazoefu wa Super Gro wanasema baada ya wiki 2 hadi 3 viazi uweza kutoa viazi vichanga ukubwa wa kidole, ni muhimu kufahamu kuwa Super Gro hulainisha udongo na kuhifadhi maji kwenye matuta ya viazi wakati wa kiangazi na viazi vinaweza kuendelea kuzaa hata mwaka mzima.
KAHAWA (COFFEE)

(Kwa mimea kama miti puliza na mwangilia kuzunguka shina)
Super Gro inaweza kutumika kuanzia kwenye kitalu cha miche mpaka kupandikiza mpaka uhai wote wa mibuni, weka cc 1 ya Super Gro kwenye Lita 1 ya maji kwenye mmea mmoja wakati wa mvua, weka mara mbili kwa mwezi na wakati wa kiangazi usiweke kabisa.

Rudia wakati wa mvua tu. Kiasi na utaratibu kama huu unaweza kutumika kwenye mimea kama mibuni. Unapotumia Super Gro mibuni itaanza kutoa maua mara mbili kwa mwaka, kwa mibuni iliyopukutika majani ukipulizia Super Gro huota majani haraka na kuota maua haraka, baada ya mavuno ukipuliza Super Gro hutoa maua tena, huzuia sisimizi ambao hupanda kwenye mibuni. Wakati wa kahawa inatoa maua puliza Super Gro bila kuweka dawa yoyote ya kuuwa wadudu.

Kwa mibuni mikubwa tumia lita 5 za maji changanya cc 1 Super Gro kwenye mbuni mmoja na unaweza kutumia kwenye majani pia.

MATOKEO: MBUNI MMOJA HUTOA HADI KILO 20 ZA KAHAWA ILIYOKOBOLEWA GRADE 18
NDIZI (BANANA)

Kabla ya kupanda loweka shina la mgomba kwa saa 24 baada ya kupanda weka Super Gro kwa kufuata utaratibu kama uliotumika kwenye kahawa, vilevile unaweza kutumia kwenye dawa ya kuuwa magugu.
VIAZI MVIRINGO – VIAZI VYA CHIPS (IRISH POTATO)

Puliza mbegu usiku kesho yake panda, baada ya kuota pulizia kila baada ya wiki 2 mpaka vitaacha kutoa maua. Shuhuda, mkulima mmoja (Masaka ) alipanda kiroba kimoja akavuna viroba 15, kwa kawaida viroba 5 hutoa viroba 15 lakini baada ya kutumia GNLD Super Gro kiroba kimoja kimetoa viroba 15.

MBOGA ZA MAJANI
Hii inajumuisha (nyanya, nyanya chungu, cabbage, pilipili hoho bilinganya, spinachi mchicha na vitunguu n.k)

NYANYA
MBOGA ZA MAJANI NYINGINE FUATA UTARATIBU KAMA HUO WA NYANYA.
Loweka mbegu kwa siku mbili kabla ya kupanda, unaweza kupanda kwenye vitalu au moja kwa moja kwenye shimo, kwa kuwa mbegu huwa zinashikana ni vizuri kuziachanisha kabla ya kupanda.

Mbegu huota haraka baada ya siku tano tu ukilinganisha na kawaida bila kutumia Super Gro ambapo huota baada ya siku 14. Changanya Super Gro kwenye dawa zote za kupuliza kwenye majani (cc 1 kwa maji lita 1) kama ni bomba la lita 20 weka cc 20 za Super Gro hufanya dawa za kuua wadudu na za ukungu kushika vizuri kenye majani (mfano bluu kopa kwenye nyanya) shuhuda mkulima wa kishuro (Kagera)

Super Gro inapunguza ukungu wa nyanya. Endelea kupulizia Super Gro kila unapopuliza dawa mpaka nyanya zinapoacha kutoa maua.
Pia changanya mchanganyiko kama huo kwenye maji ya kumwagilia itapunguza kupotea kwa maji kama mvuke , na kwa kuwa maji mengi yanazama chini hivyo kupunguza mzunguko wa kumwagilia angalau kila baada ya siku 3. Vilevile huongeza uwezo wa nyanya kufyonza mbolea za chumvichumvi na virutubisho vingine kutoka ardhini.

MATUNDA

MITI YA MBAO
SUPER GRO KATIKA ULIMAJI WA MITI.
Super gro inatumika hata kwa miti ya kuzalisha mbao.
Kama miti ni mifupi hupuliziwa hadi kwenye majani,kama miti imeshakuwa mirefu hupulizwaa kwenye shina tu.

VIPIMO NA UTUMIAJI
Vipimo havitofautiani na vipimo vingine vya miti.mfano;miembe ,minazi,miparachichi,mipera n.k.

Changanya 20cc za super gro kwenye lita 20 za maji,halafu pulizia kama unavyopulizia kwenye mazao mengine.
Ni vizuri kama itapulizwa angalau mara tatu kwa mwaka.

FAIDA YA SUPER GRO KWENYE MITI
Inasaidia miti kukua haraka na kwa viwango kinacholingana.
Inasaidia kutunza unyevu katika udongo hata waakati mvua ni chache.
Husaidia miti kupanuka,hivyo kuongeza uzalishaji wa miti.
Husaidia miti isishambuliwea na wadudu hivyo hutengeneza mbao ambazo hazina makovu.
Miti mingine ni kama minazi,miembe,miparachichi nk

UFUGAJI WA SAMAKI
-Weka maji kwenye bwawa,
_Ukiweza kuyapima ni sawa au ukijua bwawa lako lina lita ngapi pia ni vizuri,
_Weka 1cc ya Super gro kwa kila lita 10 za vizuri,
_Acha maji kwa siku 7-10 kurutubisha bwawa,
_Ondoa maji yako yite alafu weka maji masafi yasiyokuwa na super gro,
Acha maji hayo kwa siku 5-7 ,
_Weka samaki ndani,

FAIDA YA SUPER GRO KWASAMAKI.
*Huongeza ukubwa wa samaki.
*Samaki hukua kwa ukubwa sawa.
*Super gro husaidia ukuaji wa (plankton) ndani ya bwawa, na hii huzuia vifo vya samaki pia huondoa tabia ya samaki kula samaki wengine.
*Husaidia kufanya maji yawe safi na usibadilishe mara kwa mara, kwani huongeza kiasi cha oxygen ndani ya maji.
*Inaweza kutumika kwenye bwaw la plastic, matope, au sakafu.
*Super gro husaidiamaji katika bwawa yasitoe harufu.
*Gharama yake ni nafuu kwani unahitaji 1cc kwa kila lita 10 za maji.
Hupunguza gharama za utunzaji wa miti ,kwani miti huvunwa kwa haraka.

Super Gro ikichanganywa na maji huwezesha maji kupenya hadi tabaka la tatu ambapo huwa kuna madini na virutubisho vingi.; Vilainisho vya maji huongeza na kuboresha utendaji kazi wa madawa na mbolea za kilimo na hutumika kama:
Kuyeyusha hali ya mafutamafuta hasa kwenye majani ya mimea
Kulainisha maji na kuondoa mzio (surface tension)
Kutawanyisha maji kwa urahisi.

Ni kama gundi kuwezesha madawa ya kilimo aina zote kushika vizuri zaidi kwenye majani na hivyo madawa huweza kuua wadudu badala ya wadudu kuruka pembeni kama hutatumia Super Gro na hivyo kupunguza kurudiarudia kupuliza dawa, kutumia dawa kidogo kwa msimu, muda kidogo pesa kidogo na kuongeza mavuno.

Kuondoa nguvu ya kushikana kwa dawa na kuifanya ichanganyikane na maji vizuri itawanyike vizuri kwenye maji. Majani na ikae kwenye maji kwa muda mrefu bila kujitenga.

Kuwezesha maji kupenya mpaka tabaka la tatu la udongo na kuwa kuwa tabaka la tatu huwa gumu mizizi hushindwa kufyonza virutubisho na kuishi juu, Super Gro hulainisha tabaka la tatu na kufanya mimea kufikia sehemu yenye virutubisho vingi na kukua vizuri.
Kuongeza uwezo wa udongo kutunza unyevu.

FAIDA ZAIDI
Haina sumu yoyote ni salama kwa binadamu na wala haiathiri mazingira.
Haibadili wala kuharibu udongo.
Kupunguza matumizi makubwa ya mbolea na madawa.

NAMNA YA KUTUMIA
CC Moja ya Super Gro changanya na lita Moja ya maji.
Au CC Tano za Super Gro changanya na lita Tano za maji.
Au CC Mia za Super Gro changanya na lita Mia za maji.

MAHARAGWE NA SOYA
Loweka mbegu kwa saa 4 kabla ya kupanda kwenye mchanganyiko wa Super Gro na maji, rejea maelezo hapo juu, tafadhali loweka kiasi ambacho utatumia na kumaliza. Acha nafasi ya sentimita 30 au lula moja kila upande kati ya mbegu na mbegu.

Baada ya kuota puliza tu wakati maharage yana majani mawili au matatu kila baada ya wiki mbili wakati wa mvua na mara moja kwa wiki wakati wa ukame.
Kuzuia wadudu waharibifu changanya duducyper (Cc 15 Super Gro) kwenye Super Gro cc 15 na maji lita 15) Puliza kila baada ya wiki mbili mpaka maua yatakapokomaa na kudondoka yenyewe, baadhi ya sehemu huko Uganda wameweza kuvuna chini ya miezi miwili baada ya kupanda, jedwali lifuatalo linaonyesha matokeo baada ya kutumia Super Gro katika wilaya ya Masaka na Mityana

MASAKA
MITYANA

KIASI CHA MAHARAGE YALIYOPANDWA
KILO 6
KILO 7

KIASI CHA MAHARAGE YALIYOVUNWA
KILO 250
KILO 250

Morogoro, Mtwara, Kagera (Nyamilamba, kanyinya kanywangonge na kishuro)
Ili kumrahisishia mkulima matumizi onyesha jinsi inavyofanyakazi kwa kwenda shambani. Toa maelezo kwa ukamilifu na sahihi na faida zake.

Ikumbukwe kwamba matokeo yaliyotolewa kwenye majedwali msingi wake ni wakulima wenyewe baada ya matumizi ya Super Gro, yanaweza kutofautiana kutoka sehemu moja na nyingine kwa sababu ya hali ya hewa na mazingira ya eneo Fulani kwa ujumla.

Wakulima wanashauriwa kutoa ushirikiano hasa matokeo baada ya matumizi ili ushauri mzuri uweze kutolewa na itawezesha maelezo zaidi kuandikwa na kusambazwa kwa wengine. Kutokana na GNLD Super Gro nyuso za wakulima wengi zinaonyesha furaha na matumaini makubwa ya maisha mazuri.

SUPER GRO INAPATIKANA KATIKA UJAZO WA CC 250 NA LITA (5) TANO
Lita tano (5) za Super Gro zinaweza kutumika kwenye eneo la ekari 15
KAZI ZA SUPER GRO

GNLD Super Gro hufanya kazi ya kulainisha maji na kuondoa mzio wa maji. Kawaida maji hutiririka juu ya udongo na majani ya mimea bila kupenya ardhini au kiasi kidogo hupenya na kuishia tabaka la juu la udongo jua likiwaka maji hayo hupotea ka mvuke hewani.

ANGALIZO
Kwa mazao yote yafuatayo ambayo hujichavua yenyewe unaweza kuchanganya Super Gro na madawa yote ya mimea na kupulizia maua yake. Mazao hayo ni mpunga, mahindi, ngano, soya, mazao yote ya jamii ya ngano, dengu, njegere, maharage, jamii yote ya pilipili , nyanya, ufuta, bilinganya n.k

Kwa mazao yote ambayo huchavuliwa na wadudu ni vizuri kufahamu kwamba inapendekezwa usitumie madawa ya kuua wadudu wakati mazao hayo yakitoa maua kwani dawa hizo zinaweza kuuwa wadudu wanaochazisha mimea hiyo lakini Super Gro inaweza kutumika kwa kuwa haiui wadudu. Mazao hayo ni kama : Kahawa, Cocoa, apples, zabibu, alizeti, tikiti maji, maboga, matango n.k
 
Na kama mnaitaka Mali mtaipata shambani
 
Mawasiliano:0766371956
WhatsApp: 0744065796
Eneo:Mwanza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…