Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Nyota wa Klabu ya Simba, Joshua Mutale, hatoshiriki kwenye mechi za kufuzu michuano ya AFCON 2025 ambazo Zambia itacheza kwenye tarehe za FIFA, Novemba 15 na 19.
Mutale, aliumia katika mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya KMC na alijumuishwa kwenye kikosi cha Chipolopolo, lakini taarifa zinathibitisha kuwa anarejea Tanzania kwa ajili ya matibabu ya ziada.
Hii ni changamoto nyingine kwa Mutale, ambaye ameanza vibaya katika utumishi wake ndani ya Simba kutokana na majeraha. Mutale atakosa mechi dhidi ya Ivory Coast na Sierra Leone na sasa atapewa uangalizi wa karibu na madaktari wa Simba SC.