Pigo Lingine kwa Police wa Bongo: Police Abuse, Torture, Impede HIV Services

Pigo Lingine kwa Police wa Bongo: Police Abuse, Torture, Impede HIV Services

Determinantor

Platinum Member
Joined
Mar 17, 2008
Posts
59,045
Reaction score
94,974
Wadau katika pita pita zangu nilikuatan na hii kitu toka Human Rights Watch, ukiisoma vizuri utakuta kuna video na ipo pia version ya kiswahili, nikaona si vibaya kushirikishana. Kama ilishawekwa hapa jamvini basi kindly ignore. Gonga hio link halafu utajisomea mwenyewe jinsi askari wetu wanavyoendekeza rushwa ya ngono tena bila hata kinga, mezani na uchochoroni.

Tanzania: Police Abuse, Torture, Impede HIV Services | Human Rights Watch
na hiii hapa ni ya kiswahili.
http://www.hrw.org/sites/default/files/reports/tanzania0613kiwebwcover.pdf
 
Muhtasari​
Nimejaribu kuweka kwa kifupi japo nimekopi na kupesti toka kwenye PDF​
*Mnamo Desemba mwaka wa 2011, polisi wa Dar es Salaam walimkamata na kumtesaSuleiman R., ambaye hutumia heroini, katika juhudi za kumlazimisha akiri wizi ambaohakuwa ameutekeleza. Walimpiga kwa vyuma na kuuchoma mkono wake kwa pasi. Polisiwalimzuia Suleiman usiku kucha na kumlazimisha mamake alipe shilingi laki mbili zaTanzania (dola za 125) ili kumwachilia Suleiman siku iliyofuata. Alipoachiliwa, Suleimanaliwaomba polisi wale Fomu Nambari 3 ya Polisi (PF-3), ambayo hospitali za umma huhitajikabla ya kuwatibu waliovamiwa. Polisi walikataa, wakisema, "Ikiwa tutakupa PF-3,utashtaki polisi mahakamani." Suleiman alilazimika kupata matibabu ghali katikahospitali ya kibinafsi.***Saidi W., Mwamini K., na Suleiman R., wana mambo mawili yanayofanana. Kwanza, wotewamo katika kile ambacho wataalamu wa afya ya umma wanaoushughulikia mlipuko waVVU/UKIMWI wanarejelea kama "kundi la watu walio katika hatari kubwa zaidi" au"makundi maalum." Ingawa kiwango cha maambukizo ya virusi vya Ukimwi (VVU)miongoni mwa umma kwa jumla kimepungua Tanzania, data iliyopo inadhihirisha kuwakiwango hicho kimeongezeka miongoni mwa watu katika kundi hili maalum, wakiwemowanaume wanaofanya ngono na wanaume, wafanyakazi wa ngono, na wanaojidunga dawaza kulevya.
Watu hawa watatu pia wana sifa nyingine ya bahati mbaya kuwa sheria za Tanzaniazinawatambua wote kama wahalifu. Hali inayowafanya kwenda mafichoni; hivyo basikuwafanya walengwa wepesi wa ukiukaji wa haki za binadamu na maafisa wanaotekelezasheria; kuhalalisha stigma dhidi yao kutoka kwa wengi; na kuyapa mashirika ya serikalikisingizio cha kutowazingatia au kutowashughulikia vilivyo.
Ripoti hii imetokana na utafiti uliofanywa na shirika la kutetea haki za binadamu la HumanRihts Watch pamoja na shirika la "Wake Up and Step Forward Network" (WASO), ulioko Dares Salaam ambao ni mtandao wa makundi yanayowakilisha wanaume wanaofanyamapenzi na wanaume, kati ya Mei 2012 na Aprili 2013. Ripoti inarekodi ukiukaji wa haki za
kibinadamu unaowahusu wafanyakazi wa ngono; wanaojidunga dawa za kulevya; na
wanawake wanaofanya mapenzi na wanawake (​
women who have sex with women, WSW),wanaume wanaofanya mapenzi na wanaume ( men who have sex with men, MSM),wanaovutiwa kimapenzi na jinsia zote mbili, wanaotamani kubadilisha jinsia zao, na watuwenye jinsia mbili (kiume na kike), ama "LGBTI" (lesbian, gay, bisexual, transgender andintersex). Pia inafichua hali ya kusikitisha ya unyonyaji wa kingono wa watotowanaoshiriki biashara ya ngono. Ripoti vile vile inamulika aina mbili kuu za ukiukaji wahaki za binadamu: ukiukaji unaowahusu maafisa watekelezaji wa sheria kama walaumiwawa kimsingi, na ule wa sekta ya afya.
Dhuluma Kutoka kwa Polisi​
Utafiti huu umerekodi visa kadhaa vya ukiukaji mkubwa wa haki za binadamuunaotekelezwa na polisi, vikiwemo mateso na ubakaji, uvamizi, kuwakamata watukiholela, na kudai hongo, pamoja na kutokubali kupokea malalamishi kutoka kwa walewalioko hatarini ambao vile vile ni waathiriwa wa uhalifu.Katika kisa kimoja cha kutisha sana, polisi walimkamata John Elias, anayetumia heroini,katika msako wa mihadarati katika eneo la Kigamboni kule Dar es Salaam mnamo Februari18, mwaka wa 2010. Katika kituo cha polisi, afisa wa polisi aliyadunga macho yake yotekwa sirinji iliyojaa kiowevu. Elias alipoenda hospitalini wiki moja baadaye, aligunduakuwa kiowevu kile kilikuwa ni asidi. Leo hii, Elias ana mashimo badala ya macho.Makundi yanayodumisha amani ingawa si rasmi sana, hasa Sungu Sungu, piayamelaumiwa kwa kuzua vurugu dhidi ya makundi yaliyo hatarini kwa kutumia nguvu maranyingi. Ukiukaji wao unajumuisha uvamizi wa Mwanahamisi K., karibu na njia ya reli kuleTandika, Dar es Salaam, mnamo Mei mwaka wa 2012, ambapo alikuwa ameenda kuvutaheroini. Aliliambia shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch: "Sita katiyao walinilazimisha kufanya ngono nao…. Hawakutumia kondomu. Ubakaji huo ulichukuasaa moja au mbili. Nilikuwa na mtoto wangu. Mtoto huyo wa kiume alikuwa akilala ardhinikando nilipokuwa nikibakwa... Baada ya kunibaka, waliniambia, ‘Usizurure usiku.'"Kusisitiza zaidi hadhi ya chini ya na kutoheshimiwa kwa kundi hili la wale walio hatarini,polisi hukataa wakati mwingine kukubali malalamiko wakati wafanyakazi wa ngono,​
"T​
UCHUKULIE KAMA WANADAMU" 4
wanaojidunga dawa za kulevya au wana LGBTI ni waathiriwa wa uhalifu, ama kutoka kwavikosi vya usalama vyenyewe au kutoka kwa wananchi wengine. Kama alivyoelezamfanyakazi wa afya ya umma kutoka Mwanza, "Wafanyakazi wa ngono hawana nafasi yakuzungumza dhidi ya ukiukaji wa haki dhidi yao, na polisi wanaweza kuwanyanyasa ikiwawataenda kupiga ripoti. Ikiwa wataenda kwa polisi, polisi basi wanageuka kuwa watejawao kwa usiku huo."Ukiukaji wote huu wa haki za binadamu unaendeleza stigma na kuchangia mazingiraambapo wanaume wanaofanya mapenzi na wanaume, wafanyakazi wa ngono, nawanaojidunga dawa za kulevya, huishia kuzidi kutengwa na kupoteza imani kwa serikali,hivyo kudhoofisha miradi ya afya ya umma inayotegemea ushirikiano na ubia baina yaserikali na watu walio katika hatari ya kuambukizwa virusi vya Ukimwi.Miongoni mwa makundi matatu muhimu katika jamii, utafiti wetu unakisia kuwa walewalio katika hatari kubwa zaidi ya kudhulumiwa na polisi wanatoka katika matabaka yachini ya kijamii na kiuchumi. Katika visa vyote vilivyoangaziwa hapa, maafisa wa serikalina mawakala wao wanahudumu bila hofu ya kuadhibiwa kisheria.​
Ukiukaji Katika Sekta ya Afya​
Ukiukaji wa haki za binadamu katika sekta ya afya unajumuisha kunyimwa huduma,kudhulumiwa kwa maneno na kutusiwa pamoja na kukiuka faragha zao. Visa kama hivyovinajumuisha tukio la mwaka wa 2011 katika hospitali ya Temeke jijini Dar es Salaamambapo mhudumu alikataa kutumia anestezia alipokuwa akimshona mtumiaji wa dawa zakulevya baada ya kuvamiwa na kundi la watu, na kisa cha Machi, mwaka wa 2012 ambapodaktari katika hospitali ya Mnazi Mmoja huko Unguja alidinda kumtibu mwanamumeanayefanya ngono wa wanaume kisonono akidai, "Tayari umefirwa na wanaume, sasaunakuja hapa kutuletea shida. Ondoka."Ripoti hiyo pia ina rekodi za mahitaji magumu kuyatimiza katika sekta ya afya ambayo,ingawa hayajakusudiwa kubagua, huweka vikwazo fulani kwa upatikanaji wa huduma zaafya kwa wanaume wanaofanya ngono na wanaume, wafanyakazi wa ngono, nawanaojidunga dawa za kulevya. Kwa mfano, Jamila H., mfanyikazi wa ngono, alibakwa nagenge mnamo Februari mwaka wa 2012 na akaenda katika hospitali ya umma, lakini​
5 H​
UMAN RIGHTS WATCH | JUNI 2013
aliambiwa kuwa alihitajika kujaziwa fomu ya uvamizi na polisi kabla ya kupewa matibabu."Walisema kuwa ilinibidi kwenda kwa polisi, lakini singeweza kwa sababu nilikuwamfanyakazi wa ngono," alisema. Wawili kati ya waliombaka hawakutumia kondomu, lakinibila huduma za hospitali, hakupimwa virusi vya Ukimwi. Halima Y., pia mfanyakazi wangono, alisema kuwa wafanyakazi wa afya katika hospitali ya Mwananyamala jijini Dar esSalaam walikataa kumtibu ugonjwa wa zinaa kwa sababu hangeweza kuandamana namwenziwe wa ngono hadi hospitalini ili kupimwa na kutibiwa.Matibabu yanayotolewa kwa njia ya ubaguzi, yakijumuishwa na ukosefu wa maagizodhahiri kutoka serikalini kuwa hakuna yeyote atakayekamatwa au kuteswa kwa kutafutahuduma, inasababisha watu kususia huduma za afya. Polisi au makundi yale yakudumisha usalama wakiwadhulumu au kuwakamata kiholela wanachama wa kundi lolotelililotengwa, au wahudumu wa sekta ya afya wakiwawanyima huduma, matendo yaoyanakiuka kanuni dhahiri za kimataifa kuhusu haki za binadamu, na pia hukiuka sheria zaTanzania.​
Makundi Yaliyoko Katika Hatari Zaidi/ Makundi Maalum​
Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ya Tanzania, kama wizara nyingi za afya kote duniani,imetambua kuwa wanaume wanaofanya ngono na wanaume wengine, wafanyakazi wangono, na wanaojidunga dawa za kulevya ni washirika muhimu katika vita dhidi ya Ukimwi.Mkakati wa Pili wa Taifa Kudhibiti Ukimwi, 2008-2012 (National Multi-sectoral StrategicFramework II on HIV and AIDS, 2008-2012), ulitambua kuwa stigma huzuia utafutaji wahuduma. (Mkakati wa sasa kwa kipindi cha mwaka wa 2013 hadi 2017 ulikuwaukitayarishwa ripoti hii ilipokuwa ikiandikwa). Mkakati huu ulibainisha mikakati kadhaainayolenga kupunguza maambukizo baina ya makundi yaliyo katika hatari kubwa zaidi,wakiwemo wanawake wanaofanya mapenzi na wanawake, wanaume wanaofanya mapenzina wanaume, wafanyakazi wa ngono, na wanaojidunga dawa za kulevya. Mkakati huuunajumuisha mikakati mitatu muhimu. Kwa kunukua mkakati ule:​
•​
Kuhimiza upatikanaji rahisi wa taarifa za kinga na huduma za VVU (vipeperushi,upatikanaji wa kondomu, elimu rika, upimaji rafiki, ushauri rafiki na huduma zamaradhi ya ngono) kwa walio katika hatari ya kuambukizwa zaidi.)
"T​
UCHUKULIE KAMA WANADAMU" 6
•​
Kujenga ubia kati ya serikali na asasi za kijamii pamoja na taasisi nyinginezinazofanya kazi na jamii zilizo katika hatari zaidi ili kushawishi kujengewa uwezona kupatiwa ulinzi, vilevile kuwezesha uwekaji wa kumbukumbu na ubadilishanajiwa taarifa.)
•​
Kukubali kuwa wafanyabiashara wa ngono na wanaume wanaofanya ngono nawanaume wenzao wako katika hatari zaidi hivyo kuhimiza wapatiwe taarifa za VVUna huduma na pia kutokudharau shughuli zao.Kwa sababu ambazo hazijulikana kwa Human Rights Watch na WASO, mkakati huu wa tatuni tofauti katika toleo la Kiingereza ya Mkakati wa Pili wa Taifa Kudhibiti Ukimwi.Unasomwa katika Kiingereza: "Kukubali kuwa wafanyabiashara wa ngono na wanaumewanaofanya ngono na wanaume wenzao wako katika hatari zaidi na kutetea haki zao yakupata taarifa na huduma kuhusu kinga dhidi ya Ukimwi, na kutetea kuondoauharamishaji wa shughuli zao." Hatua muhimu ya uharamishaji wa shughuli wa makundimaalum inakosa katika toleo la Kiswahili.Huko Unguja – jimbo linalodumisha muungano wa kisiasa na Tanzania, lakini lina bungelake na Rais wake – Mkakati wa Pili wa Taifa wa Ukimwi Zanzibar (2011-2016) haubainishiuhalalishaji wa biashara ya ngono au ngono ya hiari baina ya wanaume, lakiniunapendekeza kampeni ya kitaifa ya kuhamasisha kuwepo kwa stahamala kwa makundimaalum. Pia inahimiza kuwepo kwa hatua nyinginezo endelevu, zikiwemo ubadilishanajiwa sirinji kwa wanaojidunga dawa za kulevya, na kutolewa kwa kondomu na vilainisho vyamajimaji kwa wanaume wanaofanya mapenzi na wanaume.Kwa bahati mbaya, sheria iliyopo, ikijumuishwa na nyendo za kudhulumu za maafisawanaotekeleza sheria na wale wa afya, hukwaza mikakati yote hii, katika Tanzania bara napia Unguja.
Wahalifu katika Muktadha wa Sheria​
Sheria za Tanzania huharamisha tendo la ngono ya hiari baina ya wanaume na adhabu yakifungo cha kati ya miaka thelathini hadi maisha gerezeni, mojawapo ya zile adhabu kalizaidi ulimwenguni kwa kosa la mapenzi ya jinsia moja. Unguja ina sheria tofauti kidogolakini imeharamisha mapenzi ya jinsia moja kati ya wanaume na kati ya wanawake. Katika​
7 H​
UMAN RIGHTS WATCH | JUNI 2013
maeneo yote mawili, hakujatokea mashtaka yanayolenga tendo la mapenzi ya jinsia mojakatika miaka ya hivi karibuni, lakini sheria hii – na jinsi inavyotekelezwa vibaya --inawabagua wanawake wanaofanya mapenzi na wanawake, wanaume wanaofanyamapenzi na wanaume, wanaovutiwa kimapenzi na jinsia zote mbili, wanaotamanikubadilisha jinsia zao, na watu wenye jinsia mbili (kiume na kike). Hii pia huwatia katikahatari zaidi ya kukumbana na unafiki na kudaiwa hongo na polisi wanapoazimiakudumisha hadhi yao ya kisiri.Sheria ya Tanzania pia huharamisha biashara ya ngono: adhabu ya kurandaranda kwalengo la kutekeleza ukahaba ni kifungo cha miezi mitatu gerezani katika Tanzania bara, nakufanya ngono kwa lengo la kujipa pesa ni ya miaka mitatu gerezani huko Unguja.Matumizi ya kibinafsi ya aina yoyote ya dawa za kulevya au dawa zozote za kusisimua akilihuadhibiwa kwa kifungo cha miaka kumi gerezani katika Tanzania bara, faini ya shilingimilioni moja za Tanzania, au zote mbili. Huko Unguja, kosa hili huadhibiwa kwa kifungo​
cha hadi miaka saba gerezani.
 
ahsante kwa kushare nasi japo sijamaliza kusoma vyote :glasses-nerdy:
 
Hata polsi nao ni wangonjwa na pia hushiriki mapenzi ya jinsia moja. but kuna ukweri kwa yaliyosemwa
 
hao ndio Polisi wetu na hayo ndio mambo yao......wanagonga nanihii hadi kwenye meza juu, sipati picha kavua gwanda kamlaza mtu juu ya meza as if anamu-operate.
 
Back
Top Bottom