Pika Samaki wa mchuzi kwa dizaini hii

Pika Samaki wa mchuzi kwa dizaini hii

Jospina

JF-Expert Member
Joined
Apr 19, 2013
Posts
2,421
Reaction score
1,395
Mahitaji:

  • Samaki 2 (Tunatumia samaki wabichi)
  • Vitunguu maji
  • Vitunguu saumu
  • Nyanya
  • Mafuta
  • Ndimu
  • Chumvi
  • Carrots
  • Tangawizi
  • Pilipili hoho

Maelekezo:


  • Andaa vitunguu saumu, tangawizi na ndimu. Tenga kitunguu saumu kwenye sehemu mbili.
  • Osha na kisha mchukue samaki wako – weka tangawizi, vitunguu saumu, ndimu na chumvi.
  • Acha samaki akae kiasi – ikiwezekana kwenye jokofu – ili viungo viingie vizuri.
  • Menya vitunguu, nyanya, pilipili hoho na karoti na kisha kata vipande vidogo.
  • Weka mafuta kwenye kikaangio kilicho jikoni. Subiria yapate moto vizuri.
  • Weka samaki na ukaange hadi aive vizuri. Ukimaliza weka samaki pembeni.
  • Bandika sufuria, weka mafuta uliyokaangia samaki. Subiria yapate moto vizuri kisha weka vitunguu na uvikaange mpaka viwe vya kahawia.
  • Weka pilipili hoho na koroga mchanganyiko.
  • Weka vitunguu saumu huku ukiendelea kukoroga kuzuia visigande kwenye sufuria.
  • Weka karoti na endela kukoroga
  • Weka nyanya kisha funika kwa muda wa dakika 5. Hakikisha kuwa moto si mkali sana, bali uwe wa wastani.
  • Kamulia ndimu kwenye mchanganyiko na weka chumvi kisha koroga kiasi.
  • Weka samaki na ongeza maji kiasi (usifanye hapo kwa mama ntilie mchuzi maji tu, hapo nyumbani jaribu kuandaa mchuzi mzito)
  • Acha mboga ichemeke. Maji yakikaukia mchuzi wako utakua tayari na unaweza kula na chakula chochote ila mimi napendelea kula na ubwabwa
 

Attachments

  • SAMAKI MCHUZI.jpg
    SAMAKI MCHUZI.jpg
    28.2 KB · Views: 862
Hua napika sana mchuzi wa aina hii.Ila zaidi unapendeza ukitia nazi halafu ule kwa wali.
Ila kama ukipika kama hapa ulivyotoa maelezo unafaa zaidi kwa ugali.

sawasawa!
 
naam, haswahaswa samaki mwenyewe awe changu napendelea sana huu mchuzi kwa ugali.
 
Back
Top Bottom