Pikipiki aina gani yafaa kwa kazi ya boda boda?

Manselly

JF-Expert Member
Joined
Dec 17, 2010
Posts
456
Reaction score
130
jamani kichwa cha habari chajieleza. Nipeni ushauri juu ya aina gani nzuri kwa mazingira yetu haya hasa kati ya sanlg na boxer
 
BOXER ndo inafaa ila wakati unanunua ujiwekee akiba ya miguu bandia kama si hela ya sanda & jeneza, maana chochote chaweza kutokea
 
umetisha mkuu
Mkuu si unajua mchina ndio hana gharama tena kwa biashara ya bodaboda huhitaji pikipiki ya gharama maana watakuharibia tu baada ya muda mfupi...kiboko yao mchina hata ukinunua leo kesho ikala mzinga hasara sio kiiiiiiiivoo
 
BOXER ndo inafaa ila wakati unanunua ujiwekee akiba ya miguu bandia kama si hela ya sanda & jeneza, maana chochote chaweza kutokea

kila mtu ni maiti mtarajiwa na kabla hujafa hujaumbika.....yashike maneno Haya iko siku utayakumbuka
 
SAN LG mpango mzima,boxer haifai kwa mizigo mizito labda kwa abiria tu na isiwe mshikaki.Kiufupi katika piki piki za kichina na kihindi SAN LG ipo kikazi zaidi na BOXER haiwezi kupiga show za kibabe.
 
Mchina mchina tu hata umpambe vipi.
Kwanza Abiria wenyewe wakifika wanaangalia aina ya Pikipiki.SANLG na mchina wengine zinatabia ya Vibrations,yaani full mitetemoko abiria wengi wanazipotezea.Na ndio maana ukifika kituoni unaona abiria anachagua na akipanda mtetemo harudi tena.
Boxer ndio dhamana,kimya ipo safi,hataka spare zake ni ghali ila zinadum sana tofauti na mchina,na hata ukisema uuze unauza bei nzuri kuliko SANLG hata laki laki tisa mtu hakupi.
Boxer ndio habari ya mjini,hata Benz spare zake ni ghali lakini inadum kwa muda mrefu,Uimara wa Boxer ni Zaidi ya miaka miwli hadi mitatu kwa mtunzaji ikiwa katika hali ya ubora wake,lakini mchina muda mfupi tu Engine inaanza kelele na kunguruma kama Pungo.
Boxer ukiipatia Services zake basi kesi kishwa.Na ndio kipenzi cha kina Dada kama Vitz,we mdada yuke kwenye Hedhi unamtetemeshea ------ kwa Pikipiki ya Mchina kwanini.Ndio maana wanapenda Boxers hawataki kero.
 
Kwa uzoefu wangu kama utampa dereva aendeshe wewe umetulia nyumbani na mama nunua FEKON. kama utaendesha mwenyewe nunua boxer. Madereva wa boda boda hakuna mwenye nafuu wote ni wa.she.nzi tu. usiku wanawapa night worker pikipiki yaani hawana maana.
 
Hapa kuna k2 kinachanganya ukiwa mbeya songea wanasifia snlg ukiwa arusha manyara wanasifia toyo..hapo ndyo nashndwa
 
boxer ndo mpango mzinga hakuna mtetemo wala nini unafika hom ukiwa fresh na unaunga kusimamia shoo kwa mama watoto bila longo longo.
 
biashara bwana, nzuri na mbaya bila vigezo vya kiuchumi ni majunguuuuu tu
 
Yaani skyMARK ni nzuri sana haina mpinzani kwa sasa.
 
Last edited by a moderator:
Boxer kutoka India, mimi ninazo zinapiga mzigo. Bei ni kubwa, vipuri ni aghali, zina operational cost kubwa lakini zina maisha marefu.
 
Haya other new Offer
Naomba kutaarifu kwamba ile ya Mwanzo niliopost imeishauzwa(Red Color)

Hii nyingine ipo sokoni kwa sasa(Black)

Pikipiki Boxer BM 150 Full Bima kwa mwaka mzima.

Kama kawaida Wakuu nauza moja ya Pikipiki zingu ya Boxer,kwa utaratibu wangu wa kufanya kazi kwa miezi sita kishakuiuza na kununua mpya na kumpa tena Driver.

Imenunuliwa mwaka huu Mwishoni mwa mwezi wa Pili.
Inafanyakazi na kila kitu kipo in good order pamoja na helmets.

Number:CTX
Bei 1.8M,net
Hapo utakuwa ume save muda na pia kiasi cha kama laki tano kununua mpya which is a huge Gape kwa life ya Boxer ambayo ni miaka miwili na nusu hadi mitatu kama ni mtunzaji na wakati huo chombo kinakuwa katika hali ya ubora wake ule ule.
Call or sms kwenda 0772 990971


 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…