Mwezi uliopita nilikua sijui kuendesha pikipiki, ila leo napita highway kwa tahadhari, cha kwanza nilimkodi boda boda nikampa elfu 10 tukaenda uwanjani akaanza kunipa initial training ambayo kikubwa ni balance, control, kujua,brakes clutch na throttle zinakuwa controlled vipi, baada ya hapo nikanunua pikipiki akawa anakuja jamaa yangu tunfanya practise kwenye eneo la wazi kwa muda wa masaa mawili kila siku kwa siku sita, baada ya hapo, nilianza kutoka lami siku ya saba, na kila siku jioni nilikua naangalia motorcycle riding tips, kama una bundle la kubania zipitie WikiHow maana hizo ni za maandishi na picha haziconsume MB Nyingi, otherwise angalia youtube kuna mamilioni ya Video yanakusubiri!! ila ningekushauri uanze kujifunza na mtu anaejua kwenye eneo lililowazi hasa viwanja.