Pikipiki imegonga gari yangu, ila nimeambiwa kila mtu atengeneze chombo chake kwa hela yake

Ngwega

JF-Expert Member
Joined
Aug 6, 2019
Posts
589
Reaction score
632
Nilipata ajali boda boda kagonga gari langu kwa nyuma na kusababisha uharibifu mkubwa tu. Sasa nashanga naambiwa eti kila mtu atengeneze chombo chake hii wanasheria humu ndani imekaaje? Msaada tafadhali
 
Kwanza pole sana mdau, ila kwa namna maelezo yako yalivyo ni kama yameacha gap ya namna mtu anaweza kukusaidia. Mfn, hujasema hata ni chombo (authority) gani ama ni nani aliyekuambia kua ukatengeneze gari lako mwenyewe. Wala hujaeleza hata hatua ulizozichukua baada ya ajali kutokea (i.e kwenda polisi, mahakamani n.k) ili mtu ajue anakushauri kwa angle gani.​

Nadhani ukitoa maelezo hayoπŸ‘† itakua raisi kusaidiwa.
 
Asante ndugu,,Hatua niliyochukua baada ya kutokea ajali nilipiga polisi wakaja eneo la tukio na kupima ajali kisha kwenda kituoni na kuchukua maelezo na kuandaa file kisha kupeleka mahakamani.Sasa jambo la kushangaza naambiwa kuwa hii kesi ni ya jamuhuri kwahiyo wewe gari yako utalipwa na bima,au kutengeneze kwa gharama zako mwenyewe,mimi hii imekaaje na sijui nifanyeje ili niweze kupata haki yangu
 
Kachukue pesa yako bima utengeneze gari.
Ndo kazi ya bima hio
 
Of course iyo case niya Jamhuri ivyo kama una taka ulipwe fatiria iyo case ikiisha kama kakutwa na hatia , omba copy ya iyo hukumu uka fungue case ya madai .iyo hukumu utumie kama moja ya evidence uko uendako
 
Nashukuru kiongozi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…