Ndiyomimi tena
Anhaaaa okay, vizuri umelisema hilo mkuu.Hizi zinachomolewa sana vitu na kuwekwa vibovu
Probably hazita faa, pikipiki nyingi bei rahisi ni aina ya vespa ambazo zimetengenezwa kutumika barabara za lami zisizo na mashimo.Wakuu, sijaidharau, ila nimeshangazwa na bei yake. Nimeona mtandaoni pikipiki zinazouzwa Dar Es Salaam kwa bei ndogo sana. Zipo za kuanzia laki tano mpaka sh 1.8m. Zote ni used.
Sikuwahi kumiliki pikipiki. Lakini nilipoziona leo mtandaoni, kwa jinsi zilivyo bei "chee", nimepata wazo la kuinunua moja niipeleke shambani iwe inatumika kwa safari za "hapa" na "pale" zinazohusiana na shamba.
Shamba lipo mbali na zilipo huduma muhimu za kijamii. Linahudumiwa na "wafanyakazi" watatu. Usafiri wanaotumia kwa sasa huko shambani ni baiskeli.
Je! Hizo pikipiki za bei rahisi zinazouzwa Dar Es Salaam zinaweza zikafaa?
Japo zipo mpaka za laki tano, lakini ninafikiria niwachukulie ya kuanzia laki saba.
Haitapakizwa mizigo mizito, labda vitu vidogo vidogo kama unga kilo ishirini n.k.
Hizo zinazotangazwa mitandaoni zinafaa? Namaanisha hizo za bei rahisi ambapo zingine zinauzwa mpaka shilingi laki tano!
Zinafaa?
Mkuu, 200k?πUhakika Mkuu Chukua Jombo, Halaf Pikipki Inatengenezeka Hata iwe Mbovu Vipi Na Garama Za Matengenezo Nafuu Tofauti Na Gari, Me nina Jombo Langu SANLG Nilinunua 200k Kizima Kilikuwa Injini Tu, Nimeipga Spea Huwez Amini Sasa Hvi Jombo Linapiga Kaz Huko Lichehe Kweny Ufuta.
πππMimi sijui sana kuhusu vyombo vya usafiri, lakini mtoa mada unaweza kuangalia minada ya vyombo vya moto vilivyotelekezwa polisi, huwa inafanyika unaweza pata chombo safi kwa bei ya kutupa, japo zile nzuri nzuri wanakuwaga wameshazichukua waoβ¦. (Sorry kama hizi ni siri zenu)
Kwa kupitia huu uzi wenye taarifa zaidi wanaweza kukupatia.
πππProbably hazita faa, pikipiki nyingi bei rahisi ni aina ya vespa ambazo zimetengenezwa kutumika barabara za lami zisizo na mashimo.
Tafuta model husika fanyia utafiti.
πππPikipiki used kupata ambayo haitaleta usumbufu ni kubahatisha tu, nyingi used kibongo bongo zinakuwa na tatizo mmiliki anaamua kuiuza. Kama ukiwa tayar kununua pikipiki used kuwa tayari kununua injini mpya, matairi mapya, na pia kucheki kama wiring ipo vizuri ili usijutie.
Habari kiongozi, mimi nahitaji pikipiki za laki 5, naweza kuzipataje, msaada wako mkuuPiki Mpya Dukani ni million 2.9 na sasa hivi zimefika usajili Namba E
Kwa uwiano huo wa bei mimi sishangai piki piki Namba B au A kuuzwa laki tano ujue ni nzima mimi piki piki ikiwa inauzwa laki 2 na nusu
Hapo lazima nishtuke hata ikiwa Namba A lazima nijue nanunua mkangafu au nikute piki piki Namba c inauzwa laki tano mh lazima nijue hapo nauziwa Namba na sio piki piki.
Kwa soko la piki piki sasa hivi lilivyo kwa laki 5 unapata piki piki Namba A au B Iliyo nyooka sio MIKANGAFU Ila kama huzijui ni vizuri ukaenda na fundi wako pia.