Pikipiki yageuka fusso

Pikipiki yageuka fusso

Pengo

JF-Expert Member
Joined
Oct 15, 2009
Posts
579
Reaction score
10



Kufuatia wingi wa ajali za pikipiki mjini Morogoro, madereva wa usafiri huo maarufu kama bodaboda wamekumbwa na uhaba wa abiria (wateja) na kuamua kubuni mbinu mpya ya kujipatia pesa ambapo sasa vyombo vyao vya usafiri wamevigeuza kuwa Fusso kwa kuzibebesha lumbesa ya magunia ya mkaa.

Mpiga picha wetu jana aliwakuta waendesha pikipki wawili wakiwa katika msitu wa Dakawa, Sokoine wilaya ya Mvomero wakisafirisha magunia ya mkaa kutoka eneo hilo kwenda mjini Morogoro.

Kwa mujibu wa madereva hao waliofahamika kwa jina moja moja la Ally na Joseph walidai kwamba husafirisha gunia moja la mkaa kwa malipo ya shilingi 5,000 kila moja kutoka eneo hilo mpaka mjini Morogoro.

Madereva hao walisema wingi wa ajali inaweza kuwa sababu ya wao kubadili biashara lakini hata hivyo walidai kwamba wingi wa pikipki ni moja ya sababu ya wao kufanya biashara hiyo ya kusafirisha mkaa.

 

Attachments

Back
Top Bottom