Pikipiki zinazouzwa Dar es Salaam ni za magendo au halali?

Pikipiki zinazouzwa Dar es Salaam ni za magendo au halali?

Captain mopao

Senior Member
Joined
Feb 25, 2021
Posts
133
Reaction score
384
Habari zenu ndugu wananchi,

Leo naomba kuwauliza swali wakaz wa Dar mliopo humu JF

Nimejiunga na ma group kadhaa yanaouza vitu used kutoka mikoa mbali mbali

Kuna jambo moja linanipa utata, pikipiki nyingi zinazowekwa mtandaoni kwa ajili ya biashara ni moya na bei yake ni ya chini sana

Nyingi ni Boxer ambazo mpya dukani ni miliom mbili km na nusu hivi. Ila zinazouzwa mtandaoni ni kuanzia milioni moja mpka laki tano na pia zipo katika condition nzuri kbsaaaa nyingine ni km imetmbea kilometer 100 tu na nyingi naona location ni Kbamba, Dar es Salaam.

Nimenikuta nashawishika kuja Dar kununua, lakini swali langu si sa magendo kweli au Dar bei ya pikipiki ipo chini tofauti na Dodoma?

Wadau mda mchache baada ya kiandika ujumbe huu zimeripotiwa taarifa kwenye gazeti la mwananchi na jf.., imeripotiwa watu 161 wamekamatwa dar kwa wizi wa pikipiki 🙉🙉
 
Back
Top Bottom