Pilau ya kuku na nyanya

Pilau ya kuku na nyanya

farkhina

Platinum Member
Joined
Mar 14, 2012
Posts
14,568
Reaction score
16,917
Mahitaji

Mchele kg 1
Kuku
Mayai 3-4 yaliyochemshwa
Nyanya 3 kubwa
Kitunguu thomu 1teaspoon
Tangawizi 1teaspoon
Chumvi kiasi
Bizari ya pilau 1teaspoon
Mdalasini wa unga 1teaspoon
Pilipili mboga 1 kubwa
Vitunguu maji 2 vikubwa
Pilipili manga 1/2 teaspoon
Ndimu 1
Hiliki 1/2 teaspoon
Mafuta ya kupikia
Kotmiri/giligilani...

Namna ya kutaarisha

1) Roweka mchele weka pembeni
2) Osha kuku weka chumvi,thomu,tangawizi ndimu na pilipili manga weka jikoni hadi iwive ya ikikaribia kukauka kaanga kaanga kwa hayo maji yake...
3) Kaanga vitunguu maji hadi viwe brown alafu weka pilipili mboga na nyanya na kotmiri/giigilani.
4) Weka kuku uliemtaarisha maji kiasi
5) Weka mchele na hakikisha unaoja chumvi ili kama ndogo uongeze..
6) Funika hadi ukauke maji
7) Weka mayai yako juu na uweke kwenye oven hadi ukuke vizuri...

Pilau ya nyanya tayari kwa kuliwa...
 
Attachments

  • 1384934772517.jpg
    1384934772517.jpg
    49.3 KB · Views: 1,132
  • 1384934788564.jpg
    1384934788564.jpg
    39.8 KB · Views: 687
Last edited by a moderator:
Leo umenikumbusha mamaangu bi shosti anapenda kupika pilau ya nyanya...waswahili waita pilau ya kihindi loh na tukiulizwa mbona hii pilau nyekundu ha ha ha
 
Leo umenikumbusha mamaangu bi shosti anapenda kupika pilau ya nyanya...waswahili waita pilau ya kihindi loh na tukiulizwa mbona hii pilau nyekundu ha ha ha

Ahahahahh tamu jeee...ndio umpikie mkwe wangu nae afaidi mapishi ya mama yake....
 
Ahahahahh tamu jeee...ndio umpikie mkwe wangu nae afaidi mapishi ya mama yake....
anapenda vyakula vya nyumbani mpaka ugali mkweo anashusha hana makubwa maskini mwenyewe tena ugali anaula kwa kijiko akishika kwa mkono ana kazi ya kujifuta saa zote loh
 
oh my my! wapenda kuku apo chacha! farkhina ya samaki unapikaje
 
Last edited by a moderator:
oh my my! wapenda kuku apo chacha! farkhina ya samaki unapikaje

Hahahahaha...ya samaki unapika kama pilau ya kawaida tu....ila samaki mkoleze viungo kama thomu,pilipili manga,pilipil ya kuwasha,chumvi,tangawizi na ndimu waache nusu saa wakolee viungo...then kaanga
Pilau ipike peke yake.
 
Last edited by a moderator:
anapenda vyakula vya nyumbani mpaka ugali mkweo anashusha hana makubwa maskini mwenyewe tena ugali anaula kwa kijiko akishika kwa mkono ana kazi ya kujifuta saa zote loh

Hahahahahaha umfundishe na kuusonga pia aje ampikie mwanangu lol..n
 
Hahahahaha...ya samaki unapika kama pilau ya kawaida tu....ila samaki mkoleze viungo kama thomu,pilipili manga,pilipil ya kuwasha,chumvi,tangawizi na ndimu waache nusu saa wakolee viungo...then kaanga
Pilau ipike peke yake.
thanx swirry
 
duh, picha tu mate yananitoka. Japo mi ni mpenzi wa pilau ila Ndo mara ya kwanza nasikia pilau ya aina hiyo.
 
Back
Top Bottom