Pilau ya nafaka na nyama ya kusaga

Pilau ya nafaka na nyama ya kusaga

farkhina

Platinum Member
Joined
Mar 14, 2012
Posts
14,568
Reaction score
16,917
VIPIMO

Mchele 3 vikombe

Nyama ya kusaga 1 LB

Mchanganyiko wa Nafaka (upendavyo) 1 kikopo (maharagwe, njegere, mbaazi, na kadhalika)

Vitunguu maji kata vipande vipande 3 vya kiasi

Thomu na Tangawizi 2 vijiko vya supu

Mafuta ½ Kikombe

Mchanganyiko wa bizari (Garam Masala) 2 vijiko vya chai

Vipande vya supu (Maggi cubes) 3

Maji (inategemea mchele)

Chumvi Kiasi

NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA

1) Osha mchele na roweka.

2) Weka mafuta katika sufuria na kaanga vitunguu mpaka viwe brown.

3) Tia Thomu na tangawizi, kaanga kidogo.

4) Weka nyama ya kusaga, chumvi na garam masala, endelea kukaanga mpaka nyama iwive.

5) Mwaga maji yaliomo katika kopo la nafaka na utie nafaka pekee humo.

6) Tia maji na vipande vya sup u (Maggi cubes) huku unavivuruga, koroga kidogo.

7) Tia mchele, koroga kidogo.

8) Funika na pika kwa moto mdogo mpaka karibu na kukauka ukikorogoka kidogo. (kama unavyopika pilau ya kawaida)

9) *Epua uipike katika moto wa oven 350-400 Deg kwa muda wa dakika 15.

*Kama sufuria uliyotumia sio ya kupikia katika oven, mimina katika chombo chochote kinachotumika kwa oven kama bakuli la pyrex au treya za foil.

10) Pakua katika sahani na iko tayari kwa kuliwa
1384529234043.jpg
 
mbona umeshachelewa karamu imeshaliwa!!
Sasa dada gani anambania kaka yake!!!! Hebu fanya mambo umshawishi mrembo watu tuchukue jiko. Si unajua kwetu tunaoa ukoo mzima, kwa hiyo utakuwa unakuja kwangu unakaa, unapikiwa na kula bata mwanzo mwisho 🙂
 
Hiyo ndoa au utumwa?
 
Hujanielewa naona...keshaolewa...
 
Back
Top Bottom