Kwa marehemu mzee Ondolo, alikuwa kiongozi wa Vijana Jazz enzi hizoPanaitwa uwanja wa sanaa mkuu au dagaa dagaa, wanachoma mdudu pale ni balaa.
Kwa watu wa Dar, kuna lile eneo kubwa opposite na San Cirro, ambapo kuna groceries nyingi na parking za magari.
Pale ndani kuna kina kiti-moto matata sana, lkn kinachonivutia mimi ni ile pilipili tamu ya aina yake ambayo binafsi sijapata kuionja mahala popote mikoa yote niliyozunguka.
Kwa huku Arusha hata hawana idea ya ninachoongelea, maana hakuna kitu ya aina ile.
Hakika sijui ile makitu spicy namna ile huwa inatengenezwaje!!
Naomba ajuaye anijuze ili Mama Naniliu aiandae siku moja!
Tumecheza sana cha ndimu pale enzi hizo pakimilikiwa na mzee chacha ondolo.Panaitwa uwanja wa sanaa mkuu au dagaa dagaa, wanachoma mdudu pale ni balaa.
kweli pale chachandu si mchezo.Pakajimmy ukionjeshwa na za kiunoni c utahamia kabisa
Nauliza tu dadaKing'asti , hii chachandu inakaa siku ngapi bila kuharibika? halafu pilipili mbuzi mbivu au mbichi na ka sipendi limau naweza weka ndimu? Wabeja sana!Badala ya kumuelekeza mapishi ya pilipili mnaanza chit chat!
Haya mahitaji babaake:
ambia mama yeyoo, achukue pilipili mbuzi nzima nzima (sipendi kuzikatakata ili kila mtu ajitie wazimu mwenyewe), weka sufuriani pamoja na mafuta ya kupikia mengi kiasi. Kitunguu kilichokatwa in cubes, carrots, nyanya na vitunguu swaumu na tangawizi. Kamulia limao ama weka vinegar. Weka jikoni kwa muda wa kama dakika 20, then punguza moto. Ukiona viungo vinajitenga na mafuta ngoma mdundo.
Chachandu nyingine unasaga kwenye blende nyanya, pilipili mbuzi, kitunguu, saumu, karoti na maganda ya matango. Then chemsha na mafuta. Usisahau vinegar ama malimao.
Kwa watu wa Dar, kuna lile eneo kubwa opposite na San Cirro, ambapo kuna groceries nyingi na parking za magari.
Pale ndani kuna kina kiti-moto matata sana, lkn kinachonivutia mimi ni ile pilipili tamu ya aina yake ambayo binafsi sijapata kuionja mahala popote mikoa yote niliyozunguka.
Kwa huku Arusha hata hawana idea ya ninachoongelea, maana hakuna kitu ya aina ile.
Hakika sijui ile makitu spicy namna ile huwa inatengenezwaje!!
Naomba ajuaye anijuze ili Mama Naniliu aiandae siku moja!
Nimesema watu wa Arusha nyie mnajua Mbuzi wa Kwa Mromboo tu.
Nauliza tu dadaKing'asti , hii chachandu inakaa siku ngapi bila kuharibika? halafu pilipili mbuzi mbivu au mbichi na ka sipendi limau naweza weka ndimu? Wabeja sana!
ukiikaanga sana na mafuta mengi na kuhakikisha hakuna maji hata chembe yanabaki, inaweza kukaa sana. ila ukimaliza kutumia ukaiweka kwenye friji itakuwa mwake zaidi.
pilipili zozote tu zinafaa japo za kijani zitanukia zaidi.