Pinda ambeba Rostam Igunga

Hapo Pinda amenoa. Tamko hili la kuwataka watu wasisikilize yanayosemwa bungeni ni la kulaaniwa na wapenda maendeleo wetu wa nchi yetu. I hope Spika ameshaanza kuangalia vifungu vinasemaje kuhusu mtuy anayekejeli Bunge kama alivyofanya Pinda.
 

Pamoja na mambo mengine hilo dole gumba la Pinda alikuwa anamwambia RA nakujua wewe ni fisadi papa dont F%^$£"&CK me up
 
Naona ipo kazi kubwa kuliko tulivyofikiri kuirudishai hii nchi utawala wa sheria!
Je waraka wa wapiganaji utafanya kazi? Je, ni kweli kuwa hao wapiganaji wapo?
Hapa suluhisho ni kuhakikisha kuwa utawala huu haurejei madarakani! Lakini, ni kwa vipi?


Tunaweza! Ni lazima tutumie nguvu ya umma. Naamini kwamba sasa hivi zaidi ya nusu ya Watanzania wote wameshajua kwamba umaskini wao unatokana na mismanagement ya resources za nchi yao unaofanywa na baadhi ya viongozi tuliowapa dhamana ya kuongoza nchi yetu, wakishirikiana na mafisadi walafi kama akina RA. Tunapaswa kufanya kazi ya kuwaelimisha zaidi wana wa nchi hii ili wawakatae watawala wasiofaa na wasiotetea maslahi yao. Hili linawezekana kabisa! Hebu fuatilia thread ya MKUMBO KITILA kuhusu activism.
 
Hapo Pinda amenoa. Tamko hili la kuwataka watu wasisikilize yanayosemwa bungeni ni la kulaaniwa na wapenda maendeleo wetu wa nchi yetu. I hope Spika ameshaanza kuangalia vifungu vinasemaje kuhusu mtuy anayekejeli Bunge kama alivyofanya Pinda.


Kabla bunge halivunjwa Hamad Rashid au Dr. Slaa atamuuliza atoe maelezo, kwenye kipindi cha maswali ya hapo kwa hapo kwa waziri mkuu. Hapooo...ndio utakapoona mchozi tena...huyu jamaa sio makini kabisa...anajiropokea bila kufikiri madhara ya matamshi hayo kisiasa na kisheria.
 

Natumaini watu wa Igunga wanaweza kuchambua mbivu na mbichi,hicho alichokisema Pinda kuhusu Rostam Aziz ni uvundo unaotoa harufu chafu.Rostam na nduguye Edward Lowasa wameoza na wanatoa harufu ya kifisadi.Hata watumie sabuni gani hawawezi kusafishika.

Ni kwa wajinga wachache wasiopenda kupambanua mambo kama Waziri wetu Mkuu ndio wanaoweza kwenda kuwasafisha watu waliojimwagia maji taka.Hii ni dalili kwamba mafisadi wamekibana chama kuwa ni lazima wasafishwe kwa gharama yoyote ile.

Watanzania wasioweza kupambanua mambo ndio watakao yumbishwa yumbishwa,lakini ukweli unabaki pale pale mafisadi wataendelea kuwa mafisadi hata wakisafishwa na Kikwete mwenyewe wataendelea kuwa mafisadi.

Pinda angalia unakokwenda itakugharimu kurudi tena bungeni kama mwendo wenyewe ni huu,kwa kumsafisha Rostam hapo umejipaka matope mwenyewe.
 
Nooooooo! siamini Pinda hawezi kusema vile, itakuwa "maybe" waandishi wamemnukuu vibaya. Yaani kumbe hata Pinda nae ni wa kichina!! duh Bongo imeoza! Rostam kiboko!!
 
Huyu mzee is more Idiot that I really thought!Kwa hiyo pale bungeni tunachezewa danadana tu!

Sioni ajabu huyu bwana kumsifia Rostam, kama mtakumbuka huyu bwana kabla ya kilio chake bungeni alikwisha kili kuwa hawa mafisadi ni watu hatari sana na wakuogopwa; sasa inaelekea kwa woga wake ndio anaanza kuzumza hovyo na kujipendeka kwa hawa mafisadi.
 
Hicho kidole cha Waziri Mkuu katika picha ni kwa ajili ya wale wote wanaomtetea Rostam Aziz na kundi lake la mafisadi.

Duh, kweli bwana lile dole la tusi kubwa!! tehe tehe litakuwa linaelekezwa kwa mzee wa Speed plus Standard Mheshimiwa6!
 
Siri ya ukombozi tunayo sisi wenyewe.

Kuendelea kulalamika haitatusaidia chochote, kikubwa hapa tuahidi kufuatilia kwa karibu kampeni zijazo ambazo kwa bahati mbaya zimeshaanza isivyo rasmi tena zinafanywa na waheshimiwa wakubwa sana ndani ya dola hili.
Tuhakikishe kwamba tunachagua watu ambao tunaamini watatuvusha.
Wenye busara zao walishasema: SAMAKI MMOJA AKIOZA..........wote kushnei (including MKPP) aka PM.

Kwangu mimi pinda amejidhalilisha, sijui watanzania wengine watamchukuliaje. Wakati utaamua.
 

Noted
 
Hii ni changa moto moto kwetu wananchi nadhani tumeelewa tunaongozwa na viongozi wa aina gani tunayo kazi kubwa mbele yetu.
 
Miaka ya nyuma nilimuona Mh. KMP kama mtu mwenye busara; aliyetulia; mwenye kupima hoja na kauli kabla hajanena. Lakini anazidi kunistaajabisha na kauli zake zinazoashiria tatizo katika kufikiri. Huenda ni mtu asiye na ajenda wala mikakati makini ya kisiasa. Kwanza, alisema mafisadi wanatisha. Kisha akamvisha BWM ucha-Mungu na utakatifu usio wa kawaida alipokuwa akimtetea kuhusu mgodi wa Kiwira. Sasa, hata Rostam? Unamsifuje huyu ambaye hata chama chake kinaumia kichwa jinsi ya kumvisha pazia angalau 2010 ipite salama? Si heri kunyamaza na kupiga blabla nyingine za kiutu uzima bila kuji-compromise?
 
Sometimes huwa simuelewi Pinda.Duu ameniacha hoi.Kama ni hivyo siko tena kwenye boti ya Pinda i thought ni mtu makini kumbe loo,nalikuwa najidanganya.basi bora Lowassa arudi tu ulingoni kama Pinda mwenyewe ndio yuko hivi.
 
mheshiwa mwenye nchi si alisema mambo kupigiana ndogo ndogo hayajaanza ,huyu pinda iweje aanze chokochoko hizi mapema ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…