Pinda awashangaa wanaochakachua asali

Pinda awashangaa wanaochakachua asali

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363
MizengoPinda(6).jpg

Waziri Mkuu,Mizengo Pinda


Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, amesema mojawapo ya changamoto inayoikabili biashara ya asali nchini ni uchakachuaji wa asali hiyo kwa kuchanganywa na vitu vinginevyo vikiwamo maji,Sukari gulu pamoja na kupikwa kitendo kinachoharibu ubora wa soko la asali ndani na nje ya nchi.

Pinda aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam kwenye Maonesho ya 37 ya Biashara ya Kimataifa yanayofanyika viwanja vya Mwalimu JK Nyerere, jijini Dar es Salaam.

Alifafanua kuwa mbali na changamoto hiyo uzalishaji huo unakumbwa na changamoto nyingine ya ubovu wa miundombinu kwenye maeneo ya uzalishaji na viwanda vichache vya kuongezea thamani ya mazao ya nyuki.

Alisema changamoto nyingine ni upungugu wa wataalam wa ugani na vitendea kazi, mfumo usioridhisha wa soko la asali nchini kuanzia vijijini hadi ngazi ya taifa.

Aliongeza kuwa Tanzania inakadiriwa kuwa na makundi ya nyuki milioni 9.2 yenye uwezo wa kuzalisha tani 138,000 za asali na tani 9,200 za nta kwa mwaka.

Alisema kiasi cha asilimia 4.5 ya asali ndicho kinauzwa nchi za nje na kiasi
kilichobaki kinatumika hapa nchini, pia asilimia 66 ya nta inauzwa soko la nje.

Aidha, Pinda alisema ufugaji mifugo usiozingatia mazingira endelevu na kukata miti na kuchoma moto ovyo nyika katika mbuga ambazo nyuki wanafugwa na mabadiliko ya tabia nchi yamesababisha ukame na uharibifu wa mazingira jambo ambalo linatakiwa kufanyiwa haraka marekebisho.

Alisema katika kubaliana na changamoto hizo, serikali imechukua hatua mbalimbali zikiwamo kila halmashauri kuanzisha kitengo maalum cha nyuki ili kusogeza huduma za ugani kwa wafugaji nyuki.




CHANZO: NIPASHE

 
Teh teh teh!Ina maana hajui usanii wabongo?
 
Polisi wawapige wachakachuaji....maana tumechoka sasa!
 
Tamaa ya pesa ni mabya sana!! mpaka chakula kinachakachuliwa? hawa TBS wako wapi mpaka asali hiyo iingie madukani???:disapointed:
 
Back
Top Bottom