Wangeamua tu makao makuu yawepo Shirati, kuna hospitali, kuna ofisi za serikali kama polisi, mahakama, uhamiaji, uvuvi, posta. Mitaa yake imekaa vizuri hasa Obwere hata Kabwana, manake watu miaka hiyo ya nyuma waliondolewa ziwani na sehemu nyingine na kupewa ardhi. Kuna maji ya uhakika na umeme upo. Sema na wajaluo kwa kushikilia koo (ukiwa koo ya ka Maganga, basi koo ya Sote hata ikifiwa hakuna kusikitika). Utegi na Randa hakujaendelea kama Shirati, sasa huko Ingri, kazi ipo katika maamuzi ya kisiasa bila kufuata ukweli.