Hilo moja, lakini la pili ni kwamba je, kiutawala na kisheria ana madaraka ya kumfukuza mtu kazi ki hivyo, au naye aenatafuta umaarufu usio na mpango wowote?
Mi nilisema huyu mtu bogus tangu day one.Hofu yangu ni kwamba asije kuwa mtupu kuliko Sumaye.
Definitely huyu ni mtupu zaidi, tena sana tu!
Halafu wala si vigumu kubaini kwamba ni mweupe...kwikwikwiiiii...
Ila mbona CCM imejaa vilaza namna hii...?
Amefukuzwa wapi:
Mkutanoni? (asiwepo katika hadhara hiyo) au amefukuzwa (futwa kazi?)
Mimi nadhani ni lile la mwanzo.
There is something to route for drastic measures in some instances.
Watanzania wakati mwingine tumeleema mno! Kazi tunafanya si kwa kujituma na wakati mwingine inakuwa kana kwamba tufanye tusifanye hakuna litakalobadilika.
Mimi nasema, it is about time tuwe na discipline ya kufanya kazi bila ya kusubiri kusukumwa; lakini ikibidi tusukumwe, basi tusianze kulialia kuwa tunaonewa.
Pinda ‘amfuta' kazi mtendaji
Angela Semaya, Nkasi
MTENDAJI wa Kata ya Kabwe wilayani hapa, amejikuta katika wakati mgumu baada ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kumsimamisha kazi kwa kushindwa kutekeleza wajibu wake. Waziri Mkuu aliwataka watendaji kutoa taarifa za mapato na matumizi kwa kuzibandika katika sehemu mbalimbali, ikiwamo misikitini, makanisani, pamoja na kuwataka wananchi kugoma kama watendaji hao hawataki kutoa taarifa hizo.
Charles Sichela alijikuta akipoteza kazi baada ya wananchi kumtuhumu kushindwa kutoa taarifa za mapato na matumizi ya michango wa shule za sekondari. Pinda aliamua kumuita Sichela na kumhoji kama tuhuma hizo ni kweli na alikiri kweli hajatoa taarifa ya mapato na matumizi kwa mwaka jana.
Diwani wa kata hiyo, Asante Lubisha (Chadema) alipoulizwa, alisema katika taarifa ya mwaka 2004 inaonyesha zilikuwa Sh milioni 34, lakini tangu mtendaji huyo aingie anashangaa taarifa ya matumizi na mapato kuna Sh milioni tano, hali ambayo inakatisha tamaa.
Waziri Mkuu alisema mtendaji huyo hajui kazi kwani kwa kawaida mtendaji hawezi kukaa mwaka mzima bila kutoa taarifa ya mapato na matumizi kwa wananchi.
"Haya kweli ni ya kujitakia mwenyewe, kuanzia sasa mtendaji huyu amesimamishwa kazi," alisema. Waziri Mkuu alimueleza Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya, Christina Midelo, kufanya kazi ya kuchunguza na hatua zaidi zitachukuliwa na kwamba hata kama mtendaji huyo amekula fedha, atarudisha kila senti. "Ole wake kama amekula, fedha zitarudi kila senti.
"Si haki kama wananchi hawapewi taarifa zozote za michango yao."
Hapa naona kuna confusion.
Lililowazi ni kwamba Mtendaji wa Kata amesimamishwa kazi ili uchunguzi ufanyike na kama akikutwa na makosa then achukuliwe hatua za kinidhamu au sheria ichukue mkondo wake.
Kosa la Mh. Waziri Mkuu ni kutumia Jukwaa kumsimamisha kazi mhusika, si ajabu hata kosa lenyewe halikuwa linahitaji kumsimamisha kazi bali ni kutoa karipio au maelekezo ya namna ya kufanya.
Sijui sheria na taratibu za mahesabu ya serikali za mitaa, sina hakika kama ni sahihi kutangaza report ya mahesabu ya mwaka wa fedha kabla hazijakaguliwa na wakaguzi na kuidhinishwa ama kuthibitishwa kwamba ni sahihi. Suppose ukitoa mahesabu ambayo baadaye wakaguzi wakaja kugundua kwamba hesabu hazikuwa sahihi utarudi vijijini kutoa mahesabu mapya? Nadhani hapo kuna utata na huenda Mtendaji wa Kata ana sababu za msingi. Kosa ni la wakaguzi ambao hawajakagua ama hawajatoa report yao ya ukaguzi.
Kwa mwendo wa kutoa hukumu kwenye majukwaa, inaweza kumpa mtu cheap popularity lakini ikawa ni damage kwa watu wenye uelewa. Mtindo huu haufai, hatuwezi kwenda kwa kutoa hukumu za papo kwa hapo. Hapo sioni kama kuna tofauti na Mob Justice ambapo mtu akizushiwa wizi anachomwa/pigwa on the spot bila hata kujua kama kazushiwa ama kweli ni kibaka au mwizi.
Hata hivyo kuna taratibu za kufuata kabla hujamsimamisha mtumishi kazi, ikiwa ni pamoja na kumpa onyo/karipio na mengineyo. Bado tuna safari ndefu sana!