Pinda: Maadamu suala la Utekaji linasemwa, liwepo au lisiwepo lazima tuendelee kuwa Wakali hasa upande wa Serikali

Pinda: Maadamu suala la Utekaji linasemwa, liwepo au lisiwepo lazima tuendelee kuwa Wakali hasa upande wa Serikali

Influenza

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2018
Posts
1,509
Reaction score
3,756
Waziri Mkuu mstaafu, Mizengo Pinda ameeleza anavyosikitishwa na matukio ya utekaji watoto na wengine kuuawa katika mazingira ya utatanishi huku miili yao ikikutwa imenyofolewa baadhi ya viungo kwa imani za kishirikina zinazohusishwa na harakati za uchaguzi

Amesema "Wakati naingia Uwaziri Mkuu ndio ilionekana sana imejikita [Utekaji] katika kwa Watu wenye Ualbino, wengine walikuwa wanakatwa viungo na wengine kupoteza maisha na kadhalika. Safari hii ni kama ukurasa mwingine umejitokeza, kuna baadhi wanadai kuwa Wanasiasa nao wameingia kwenye tatizo hilo kwa kujitumaisha kuwa akifanya hivyo ndio anashinda. "

Amesisitiza "Huwezi kutumia kiungo cha binadamu mwezako kwa maana kwamba ndio unatumia kutaka kushinda. Unashinda kutokana na kazi nzuri unaoifahanya na upo kazribu na watu wako waliokutuma kwenda kuwawalikisha, unashinda kama unatumia muda wako wingi kuwatumikia walio kuchagua wawakilishe"

 
Waziri Mkuu umenena.👏👏

Tunapaswa tukemee Kwa nguvu zote, kuhusu utekaji wa raia wasio na hatia

Tunaambiwa kuwa ni watu wasiojulikana wanaojihusisha na utekaji, hivi ikiwa Jeshi la Polisi, wajibu wao namba Moja ni kutulinda sisi raia na Mali zetu, hivi inapotokea wimbi la utekaji wananchi, tafsiri yake tunayopata ni kuwa Jeshi letu la Polisi, limeshindwa wajibu wake namba moja?
 
Back
Top Bottom