Pinda, Muungano, na Hatima ya Zanzibar

WAJUMBE wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar wamewataka wazanzibari kulaani kwa nguvu zote matamshi yaliotolewa jana na Waziri Mkuu Mizengo Peter Pinda ya kutaka kuifuta Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ)na kubakia serikali moja ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Matamshi hayo yametolewa na wajumbe hao wakati wakichangia makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Fedha na Uchumi katika kikao cha baraza la wawakilishi kinachoendelea Maisara Mjini Unguja.
Wawakilishi hao walisema Waziri Mkuu Pinda ni Kiongozi asiyeitakia mema Zanzibar kutokana na kauli zake za mara kwa mara za kuidharau na kuikejeli serikali ya mapinduzi ambapo walisema wanalaani matamshi hayo lakini pia wamewataka wanzanziri wote kulaani vikali matamshi yake aliyoyatoa juzi bungeni.
Mwakilishi wa Jimbo la Tumbatu (CCM) Haji Omar Kheri amemtaka Waziri Mkuu Pinda aanze kujizuia kutoa matamshi yake yanayoiweka Zanzibar katika wakati mgumu na wasiwasi wa utatanishi.
Kheri ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Chama Cha Mapinduzi (CCM) alisema kutokana na Zanzibar kuwa na nia njema na Muungano ilisamehe na kukubali kupoteza hata Utaifa na utambulisho wake kwa kuungana na Tanganyika mwaka 1964, jambo ambalo alisema halionekani kuthamininwa na Watanganyika hivi sasa.
Alisema kama kuna mtu anabeza hoja ya mafuta na gesi asilia kuondolewa katika orodha ya mambo ya Muungano basi huyo ndiye adui anayetaka kuuvunja muungano uliopo kwa miaka 45 na sio wazanzibari amabo wanadai haki zao katika muungano uliopo amabo hautendi haki sawa kwa pande mbili hizo.
Mwakilishi huyo alisema hakuna haja ya wabunge kuwaona wawaklilishi hawana mamlaka ya kujadili mustakabali wa Zanzibar na badala yake kinachotakiwa ni kuheshimiana na kuthanminiana katika pande zote mbili ambazo kila moja ina mamlaka yake na katiba ya kuendesha nchi.
"Uchumi wa Zanzibar haulingani na Tanzania Bara,bajeti ya Zanzibar ni 400 bilioni wakati wenzetu wanagota katika Trilioni 35,mafuta ni kichocheo cha SMZ kujinasua kiuchumi na kukuza maendeleo ya jamii lakini naona hivi sasa kila siku kunazuka jambo jengine" alisema Kheri ambaye pia ni Mnadhimu wa Baraza la wawakilishi kwa upande wa CCM.
Mnadhimu huyo alisema hoja ya mafuta na gesi asilia kubakishwa katika orodha ya mambo ya muungano sio ya Rais wa Zanzibar na Mweyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Aman Karume na Waziri wa Maji Ujenzi Nishati na Ardhi, Mansoor Yussuf Himid bali ni msimamo wa Baraza la Wawakilishi na ndio uamuzi wa wananchi wote wa visiwa vya Unguja na Pemba.
"Suala la mafuta ni gumu na halitekelezeki katika mfumo wa Muungano, litashindikana kama suala la Bandari linavyoleta utata ambalo ni la Muungano, lakini likisimamiwa na kila upande chini ya chombo chake husika yaani PTA na ZPC" Alisema Kheri.
Kwa upande wake Mwakilishi wa Jimbo la Chonga (CUF) Abdallah Juma Abdallah alisema kauli ya Waziri Mkuu Pinda si kauli ya kiungwana na haipaswi kuzungumzwa na mtu mzito kama yeye.
Alisema kauli yake hailengi kuimarisha Muungano bali inalenga kuvunja Muungano na hakutarajia kabisa kama mtu mzima kama yeye anaweza kufikiria kuifuta SMZ wakati huu ambao Muungano umedumu kwa miongo kadhaa.
"Kwa Kweli Mheshimiwa Spika nilikuwa natizama TV na niliposikia kauli ile ya Pinda alipoitoa bado kidogo tu niivunje TV yangu mwenyewe…niliitukana na kukereka jinsi alivyokuwa akitoa matamshi yale,sisi ni watu wazima hakuna sababu ya kutishana kama ni Muungano wa kutishana mimi simo kabisa nasema kwa uhakika kabisa" alisema Mwakilishi huyo.
Mwakilishi huyo mbali ya kulaani kauli ya Waziri Mkuu alisema matamshi hayo ni kama ni mwendelezo na dhamira ya SMT kutaka kuifuta SMZ katika ramani ya dunia na kuongeza kwamba wazanzibari hawatakuwa tayari kuona kifo cha SMZ kwani hivi sasa inaonekana Tanganyika wameshoshwa na wazanzibari kutokana na kauli zao wanazozitoa ambazo zimekosa uvumilivu.
Mwakilishi wa Jimbo la Chake Chake (CUF), Omar Ali Shehe amewataka wawakilishi na wananchi wote wa Zanzibar kulaani vikali matamshi hayo ambayo yenye kutishia kuifuta Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
Alisema lengo la Tanganyika hivi sasa ni kuifanya zanzibar ni mkoa mmoja wapo wa Tanzania jambo ambalo kabisa halitawezekana kwa kwa kuwa Zanzibar ina mamlaka yake kamili kama ilivyo Tanzania.
Mwakilishi huyo wa Chake Chake alisema kufa kwa SMZ hakutakubaliwa kabisa kwani wazee waliotangulia walipindua kwa kutumia mawe, mashoka na mapanga ambapo wengi wao walipoteza maisha yao hivyo sio rahisi leo hii ielezwe kuwa hakuna serikali ya Zanzibar.
Alisema bila ya kuwepo Serikali ya Mapinduzi Zanzibar hakutakuwa na heshima ya mzanzibari hivyo alimtaka Waziri Mkuu Pinda na wenzake wenye ndoto ya kuizika Zanzibar na kuitoa katika ramani ya dunia wasahau jambo hilo kwani hakuna mzanzibari atakayekubali suala hilo hata siku moja.
"Mheshimiwa Spika tumekerwa sana na kauli ya Pinda na kwa umoja wetu tunasema kwamba tunayalaami matamshi haya ya mtoto wa mkulima (Pinda) na tunamwambia kama ameshindwa kazi aende akachuke jembe na kuendeleza kilimo na sisi tumeshaamua kuwa mafuta hayatakuwa ya Muungano wala hatubadilishi kauli zetu huo ni msimamo wa wazanzibari" . Alisisitiza mwakilishi huyo ambaye ni mdogo kiumri
Shehe alisema kwamba Zanzibar haiwezi kabisa kusaga meno ikiwa nje ya muungano kwani rasilimali zilizoko Zanzibar zinawatosha wazanzibari kwa uchache wao na hivyo hakuna haja ya kutishana na kudhalilishana.
Mwakilishi wa Jimbo la Kiwani (CUF) Hija Hassan Hija alisema kuwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imevumilia sana uonevu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuikandamiza na kuiburuza Zanzibar kwa muda mrefu katika uchumi.
Amesema wakati umefika hivi sasa uonevu huo hautakubalika tena na kuwataka wananchi wasikubali kabisa kuyakubali maneno yanayoendelea kutolewa na viongozi wa seriakli ya jamhuri hasa yale yenye nia ya kuivuruga Zanzibar na kuipoteza katika ramani ya dunia.
Wananchi mbali mbali jana walionekana kujikusanya wakitafakari juu ya kauli ya waziri Mkuu Pinda aliyoitoa bungeni ambapo wengi wao walisema hivi sasa inaonekana watanzania hasa viongozi wamechoshwa na uvumilivu na wanataka Muungano uliopo kati ya Zanzibar na Tanzania Bara uvunjike.
"Hata siku moja maneno ya pinda hayawezi kuchukuliwa kama ni sahihi tanznaia bara ina mikoa mingapi? Ikiwa wanashindwa kuihudumia mikoa yao kuwa watu wanakaa na njaa wataweza kuifanya serikali moja halafu waweze kuihudumia huyu hana…akili zao sio timamu akapimwe kwanza Zanzibar ni nchi huru Pinda hata aende kuzikiri uchi Zanzibar haiwezi kufanywa nchi moja alaaa" alisema kwa hasira mkaazi mmoja wa Said Sudi Mkaazi wa Michenzani.
Juzi Waziri Mkuu Pinda wakati akijibu maswali ya papo kwa hapo Bungeni Mjini Dodoma alisema kwamba kelele kuhusu mafuta na gesi asilia zitakwisha kwa kuwa na nchi moja yenye serikali moja kuliko serikali mbili.
Waziri Mkuu Pinda alisema hayo kufuatia swali aliloulizwa na Mbunge wa Jimbo la Ziwani (CUF) Ali Said Salim kuhusu mambo yasiokuwa ya Muungano yanaongozwa kupitia serikali gani kwa upande wa Tanzaania Bara wakati Zanzibar imesimamiwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

SOURCE: ZANZIBAR YETU BLOG.
 
Last edited:
Kajipalia makaa chachandu, chuki zake alizorithishwa na Nyerere zidi ya Zanzibar atarudi nazo kwao Subwawanga.
 
Muungano mzuri sana, kwa sababu unawafanya wajiite sisi Wazanzibari! Nje ya Muungano watajiita sisi Wapemba, Waunguja, Watumbatu, nk. Udumu Muungano milele!
 
Huyu Pinda amesema kile ambacho na mimi Mvutakamba naamini kwamba kufuta smz ni jibu na tutaondokana na kelele za kila siku .Nadhani iwe mkoa tu tumalize hili jambo .Kujipalia makaa hapa hakupo nia tabia na mwenendo wa wenzetu kule visiwani unasababisha haya .Pinda kusema vile inaweza ikawa ni mawazo ya Serikali , maana Karume si alijifanya mjanja na hata kwenye sherehe hakuja ?
 
Hivi bajeti ya SMT kumbe ni trilion 35? Jazba mbaya sana!
 
Inferiority complex inawatafuna sana Wazenj. Wako tayari hata kugombana na ZeComedy kwa jambo dogo tena la kuigiza!
 
Kwi kwi kwi, mie sioni tofauti kati ya Zanzibar nzima na mkoa mmoja tena mdogo wa Tanganyika.
Pinda kasema kweli na wengi ukweli hawautaki, ndio umoja na serikali moja, na zanzibar waendelee na serikali ya mitaa (madiwani n.k). Ajabu kweli, mbunge wa watu 3000-5000. Kweli mnainyonya Tanganyika, wabunge zaidi ya 50 badala ya 2 wawili tu stahili kwa pemba na unguja!

Kama hamuutaki muungano si muondoke tu! mnanang'ania nini? kama ni serikali mnayo maneno mengi machafu kwa Pinda aliyewaambia ukweli ya nini?
 
Mi sioni ubaya wa kauli ya pinda hao wazanzibari waache kelele.Bravo Mkuu Pinda
 


Mfalme maneno yako ni sahihi ndiyo maana Pinda alisema wakivunja Mungano wataumia hawa .Hivi wakivunga CCM zanzibar watajiunga na CUF ama wataanzisha chama kuchuana an CUF ?
 
Kajipalia makaa chachandu, chuki zake alizorithishwa na Nyerere zidi ya Zanzibar atarudi nazo kwao Subwawanga.

Pole sana inaonekana unaandika kwa jazba vibaya hadi Sumbawanga imeguka kuwa Subwawanga. Ila ambacho sielewi kama ninyi Wazanzibari mmechoka kwa nini hamsemi basi muungano kwaheri. Semeni tu nyie machogo hatutaki ushirikiano na nyie siyo kila siku kulalamika tu kama watoto. Kwa Kizanaki tunasema "you people need to grow up."
 
Habari Ndiyo hiyo.
Mkimeza mkitema shauri yenu.
 
Pinda ameshazoea makelele ya Zenj, ndio maana hana wasiwasi na kile anachokisema! Hongera Pinda kwa ujasiri!
 
Unanipeleka maeneo yasiyonihusu, mimi sina jazba mwenye jazba unamjuwa vizuri, nataka ujuwe tu naumwa na uzanzibari kuliko utanzania wa kupewa, kwangu mm Zanzibar mwanzo halafu ndiyo njaa zangu, nakukaribisha BLW 2010,uwone patakavo waka.
Sumbwawanga au Sumbawanga???!!!
Aaaah! jina la mji wa Pinda lipo Kipindapinda, hata ukilitamka linagandaganda, ukiliandika linazongazonga, kumbe nayeye pia Mizengo. Mikasa mitupu. Tangu lini usalama wa taifa na uwaziri mkuu ww???!!!
Nilimkimbia Eliezer Feleshi alipotaka kunipeleka huko sumbwawanga sijuwi. nilimwambia hoooo bwana mkubwa nakwetu kazi zipo. Kwahala kuna jina la kichawichawi kwanini mwana wa mwenzako mie, haaa!!!
 
Pinda ameshazoea makelele ya Zenj, ndio maana hana wasiwasi na kile anachokisema! Hongera Pinda kwa ujasiri!

Mkuu si unajua tena kuna watu wasipo sikia maneno yaki tamkwa kama wanavyo taka wao basi ugomvi. Kwanza maneno ya Pinda si sheria. Yeye katoa suggestion sasa badala ya watu wajadili hoja kwa hoja wana anza kuingiza emotions.
 
Muungano mzuri sana, kwa sababu unawafanya wajiite sisi Wazanzibari! Nje ya Muungano watajiita sisi Wapemba, Waunguja, Watumbatu, nk. Udumu Muungano milele!
Kwani kabla ya huo muungano ndivyo walivyokua wakijiita ? BRAZA WEWE NAONA KUA UNA UMRI AU UWEZO MDOGO SANA WA KUJADILIANA KWA SUALA LA ZANZIBAR. Kumbuka hizi ni nchi mbili zilizokubalian ( atleast naweza kusema Znz iliingia kwenye makubaliano ya muungano kwa nia nzuri) kuungana na znz ikaweka mashrti yake kua haitapoteze utaifa au serikali yake, hiyo ilikua 45 years ago na ikakubalika pande zote mbili, leo hii anakuja mtu aliopinda akili yake na kujisemea as if yuko mkahawani maneno hata huyo mwendazimu alioko mental hospital in znz angeliyasikia basi nina hakika siku hiyo angelikataa dawa na akasema sasa nimepona hii nafasi ndani ya hii mental hospital bora aletwe pinda na BUCHANA. Mimi kwa mtizamo wangu naona hii ni njama ya kuimaliza znz kwa wivu wa wadanganyika, Lakini znz ina Raisi wa kuchaguliwa kama wana wa CCM wanavyosema, sasa ikiwa amechaguliwa na wazanzibari kweli, basi wacha tumsikie msimamo wake. Na huyo bwana mikasi mwache akae kimya tu angoje muda wake kwisha.
 
dua la kuku linapompata MWEWE!
Kweli kabisa. Na hapa wameonyesha dhahiri lengo lao kuwa hawataki kuungana. Hata hao Nyerere na Karume walikubaliana kuwa huu muundo wa serikali mbili ni wa mpito kuelekea serikali moja
 

Mfalme maneno yako ni sahihi ndiyo maana Pinda alisema wakivunja Mungano wataumia hawa .Hivi wakivunga CCM zanzibar watajiunga na CUF ama wataanzisha chama kuchuana an CUF ?
Jamani shule kweli muhimu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…