Kwanini huwi muungwana na kukubali Wazanzibari watumie kilicho chao?
Hii kauli ya "Changu changu ... Chao changu " mbona unaigeuza?
Kwani Zanzibar ilishadai kitu gani kutoka bara kuwa ni chao? Kwa sasa bara wana madini, mapori na maziwa makubwa, jee ulisikia zanzibar ikidai ipatiwe mgao? Jee umesikia lini pato a inayoitwa Serikali ya Muungano likakasimiwa na kutiwa kwenye Bajeti ya Zanzibar? Ukisikia asilimia 4.5 ni kwa mapato ya misaada inayokuja kwa jina la Tanzania. Sasa wapi inapply hiyo chenu changu? Umeme zanzibar wanaadhiriwa kila siku kwa kuchelewa kulipa.
Naona hivi Muungwana huwa hanganganii ujinga wa mtu na kwa vile Wazanzibari ni wajinga kwa kungangania mafuta yasiopo basi nyie mlio sio wajinga ni bora mkawachia na ujinga wao na hapo mtakaspothibitisha ujinga wao itakuwa wakati mzuri wa kuwacheka lakini kwea sasa Wazanzibari wanataka chao na ni haki kupewa basi!
Mkuu wangu pengine wewe huelewi bajeti ya serikali mbili zilizoungana inakwenda vipi.. Na hii ndiyo tofauti ya kuelewa kwenu.
Nitajaribu kukufahamusha naposema Changu Changu, Chako Changu wala sii kinyume...nitakubali tu kupata elimu (somo) toka kwako ikiwa kinachofanyika ni kinyume na kuelewa kwangu..
Mkuu kwanza hii ni lugha inayotumiwa kila siku na lazima uifahamu vizuri mtililiko wake laa sivyo utaona maji hayafuati mkondo - maluweluwe!
Serikali ya Zanzibar haiwezi kudai wala kuwa na bajeti inayotegemea bara ktk bunge lake kwa sababu hii ni serikali nzima inayoingia ktk muungano wetu..hili gumu nalo mkuu wangu kuhafamu, labda pitia na utazame site ya bunge lake upate kuelewa kuwa hakuna mwakilishi wa bara hata mmoja.. site hii
Hapa.
Hivyo kile kinachopatikana Zanzibar pato la makusanyo ya kodi zao ndicho kinachounda bajeti ya Zanzibar, wanachagua mawaziri wao na viongozi wao bila kumshirikisha Mbara yeyote wala bara hawakatiwi kitu toka bunge hilo maanake sii mali yao..ndio naposema Changu Changu..Yaani kinachochumwa Zanzibar kinabakia Zanzibar.
Sasa ukija tazama upande wa bara, hawa hawana serikali kama ya Zanzibar ama utaratibu unaofanana na huo wa visiwani.. Seikali yao (Tanganyika) imekwisha kufa siku nyingi pamoja na kwamba nyie mnahofia kifo cha serikali ya Zanzibar au hilo jina la Zanzibar na sijui kutoitwa Zanzibar ni nchi..Tanganyika sii serikali, sii nchi wala hakuna jina Tanganyika ktk ramani wala fikra za watu miaka 45..Na hakuna hata haja ya kumwambia mtu kuwa Tanganyika sio NCHI kwani haipo kweli.
Jambo ambalo linanishinda kuelewa sijawahi kuwasikia Wazanzibar wakilalamika na uonevu huo kwa Tanganyika, na kuuliza kwa nini muungano uliua nchi iitwayo Tanganyika, ikiwa kweli nyie ni Waungwana wenye mapenzi na haki maanake haki haiwezi kusimama tu kwa mahitaji yenu isipokuwa kwa kila atakaye tendewa kinyume cha haki..itokee nchi yoyote, mahala popote duniani nilitegemea kwamba wananchi na viongiozi wa zanzibar wataipinga mfumo unaovunja jina na kupora haki ya watu kuwa na NCHI yao..
Maajabu ya mwafrika imewatokea usoni mwao lakini hawakuona ubaya wowote Tanganyika kupoteza serikali, nchi na jina lake ila itauma tu ikiwa Zanzibar itapoteza vitu hivyo.. (mkuki kwa nguruwe)
Pili, napozungumzia Chako Changu ni kwamba mapato yote ya madini, maziwa maji na kadhalika ni mapato ambayo yanatengeneza Bunge la muungano ambapo pato lake linalotengeneza bajeti haligawiki kwa madini au maziwa ila makusanyo ya kodi zote. Hivyo Barricks wanapolipa kodi huingia ktk mfuko wa Taifa, samaki wa Kanda ya ziwa wanapouzwa Ulaya nchi za EU pato lake (kodi zake) huingia ktk mfuko wa Taifa.. Hivyo kila kitu kilichopatikana toka mfuko wa Taifa kwa jumla ya kodi zote ndio hutengeneza bajeti ya serikali ya Muungano ambayo Zanzibar pia imo na ina wawakilishi wake tofauti na ile ya Zanzibar..
Kumbuka tu ktk pato hilo la mfuko wa Taifa, Zanzibar haikuingiza hata chapa, lakini bajeti ikisomwa huambatanisha matumizi kwa visiwa vya Pemba na Unguja. Ukitaka pia pitia site ya Bunge la muungano utaona wawakilishi kibao na hata bajeti zinazohusu matumizi ya visiwani..site hii
Hapa.
Hivyo visiwa hivi hupata pango lake toka bajeti yao wenyewe na kisha toka bunge la muungano. Bara wanachotegemea ni toka Bunge la Taifa tu ambako kila mkoa na wilaya zake hukatiwa ktk fungu moja na mikoa ya visiwani pamoja na kwamba pato zima limetoka bara..