Pinda sasa ageukia mavazi awataka Watanzania kuachana na suti

Hata miye nakubaliana naye kwa kiasi fulani, ila mfano mzuri aanze yeye!
 
Maneno mengi vitendo sifuri...hivi pinda amesoma kweli??? unauliza wananchi maswali wakti wewe ndio unatakiwa ufanye kazi ..shame on you!
 
Sasa kama Pinda naye anasema tu Je sisi tufanye nini??
 
nadiriki kusema huyu pinda akapimwe akili..hatuwezi tukawa na pm anaropoka ropoka tu mambo yasiyo na mantiki,yaani yeye kipimo cha matumizi ya pesa na anasa ni kuvaa suti??hivi huyu ana nini?mi ananitia mapka kichefuchefu jamani

tumeaandika na kusema mara nyingi. Huyu ni pm dhaifu kabisa tanzania kuwa naye. Sasa akibanwa tu. Atalia na kutafuta visingizio chungunzima. Aha! Wakati mwingine tunawaza hivi hawa wazee wakienda asia wanapewa nini? Mwingine alikwenda thailand akarejea na mvua ya mabomu. Kabla hajamkufuru mungu akaondolewa. Huyu naye kaja na kukomesha vazi la suti. Tunakwenda wapi?
 
Breaking news
tafadhali wana jf wa morogoro tupeni habari zilizojiri siku mbili hizi. Kuna taarifa kuwa moto umechoma bweni la shule na kuteketeza wanafunzi watatu. Inaelezwa kuwa ni shule ya walemavu. Miezi miwili haijapita tangu tukio la idodi.
 

Unategemea nini kutoka kwa mtu aloteuliwa MSANII na yeye si ataendeleza hilo hilo tu. Kuchekeshs na kusema asilolitekeleza . Ni mchezo wa kuigiza hauna ukweli wowote.
 
Breaking news
tafadhali wana jf wa morogoro tupeni habari zilizojiri siku mbili hizi. Kuna taarifa kuwa moto umechoma bweni la shule na kuteketeza wanafunzi watatu. Inaelezwa kuwa ni shule ya walemavu. Miezi miwili haijapita tangu tukio la idodi.

Mazee hii ina warrant thread yake tofauti, vipi kuichomeka hapa?
 
mkuu pinda hiki ni kigugumizi cha akili, aache nidhamu ya uoga mimi nadhani ana wazo zuri na anatamani baadhi ya mambo yakifahari yafutwe kwa vigogo lakini anaogopa. sema mzee mkubwa wakikufukuza ni sawa utakuwa umetunza heshima yako kuliko kukaa na kitu moyoni na kuanza kuteleza kujikwa ulimi unadhalilika. kama huwezi kusema lifute rohoni ili uzungumze yanayo eleweka ina sikitisha sana ukimuona mtu mzima ana adhirika kwa kuropoka. tunajuwa mkuu pinda ana uchungu na nchi lakini yuko katikati ya mafisi wenye uchu watamtafuna
 

Unaonekana kuelekea ktk kupata ufumbuzi mkuu. Following your argument it appears so simple here to draw the conclusion: WAACHE KWENDA ASIA.!
 

Nadhani hapa kila mtu kaja na translation yake kuhusu alichokizungumza PM. Kwa kusema suti ni gharama kubwa mimi nakubaliana nalo kimsingi suti moja inagharimu sio chini ya Tshs 200,000/= sasa kwa maana hiyohiyo kuna viongozi wengi na maafisa wengi waandamizi ambao wanapata allowances kwa ajili ya mavazi na kwa mavazi huwa wanamaanisha suti hizi hela ndio zinaonekana ni gharama kubwa sana na hivyo basi PM anajaribu kuhimiza au kuzuia matumizi makubwa kama haya kwa ajili ya mavazi ambayo hayaleti maendeleo yoyote kwa watanzania.

Mkuu kama ni suti kila mtu ajinunulie kwa kipato chake lakini sio hela za wananchi zitumike kuwapa suti hawa viongozi. Nadhani umefika wakati kila mtu na hasa great thinkers kuwa na uwezo angalau wa kujaribu kutafakari kabla ya kuanza kubonyeza buttons za keyboard. PM mimi nakuunga mkono 100% lakini pia nakuhimza uwaonyeshe Watz mfano na tuone kama hao walio chini yako hawatafuata.... Kudos Pinda!
 
Kwanza nafikiria kuwa itakuwa busara sana kama akianza yeye mwenyewe kuvaa nguo za asili za Tanzania
 
Kwanza aanze yeye kuvaa nguo kila wakati wa mkutano au mwaliko wowote ule
 
Mbona wao ndio wa kwanza kuagiza suti toka ulaya na America??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…