Baada ya kilio cha muda mrefu cha madai ya Katiba, hatimae hii leo serikali ya Tanzania imekiri kuwa ipo haja ya kuifanyia mabadiliko Katiba ya sasa ili iweze kukidhi mahitaji na mabadiliko ya sasa.
Akiongea na wahariri wa vyombo vya habari leo Jijini Dar es Salaam, Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda amesema serikali itaunda jopo la wataalam kupitia mapendekezo ya awali na ya sasa yaliyotolewa kuhusiana na mabadiliko ya Katiba.
Hata hivyo Mh. Pinda amesema serikali bado haina jibu iwapo yafanyike mabadiliko makubwa ama mabadiliko madogo kutokana na mapendekezo yaliyokwishatolewa, au suala hilo lipelekwe bungeni ama lirudishwe kwa wananchi kwa maamuzi.
Source-Mimi