Pinda: Serikali kuunda jopo kuchunguza madai ya katiba mpya

Thanks Pinda, umewapatia kweli, ngoja sasa uone watavyoigeuza hiyo.
 
Safi sana, cha msingi wamekubali kwanza kuna haja ya kuangalia mapungufu yaliyopo.
 
Ukweli wenyewe bila kusema hivyo hawana mgao kutoka kwa wahisani ,wameambiwa ili kuwe na uwezekano wa wao kuwapaia mshiko lazima washughulike manug,uniko ya wananchi vyama vya upinzani ,hamna kitu hapo tukomae tuu kudai katiba kwa namna tunayoona wananchi inafaa lakini serikali ya CCM haitafanya kitu chohote.
 

Sasa nadhani kelele humu JF zitaisha, na karata hii wakiicheza vizuri 2015 watarudi madarakani kiulainiiiiiii
 

You are right pal!

Hiyo inaitwa kipoza joto, dana dana na buy time, huenda joto la katiba likapungua na wakaendelea kupeta. We have seen this movie before!

Man, these CCM people have been scrupulous not to commit to katiba Mpya, they are just brilliant in meandering discourse.
 
Wakuu, mnafikiri ni busara kwa CCM ku-lead hii process ya mabadiliko ya katiba?
Mnafikiri tupo tayari kwa sasa? mnafikiri wananchi wanajua katiba ina matatizo gani?
CCM ipo very strategic, mnafikiri itajitengenezea kaburi lake yenyewe?

Nipo skeptic kidogo on this one. Sorry.
 
Hivi huyu mama kombani yuko katika serikali ya nchi gani na kateuliwa na nani?
Inakuwaje leo pm aseme kuna haja ya katiba alafu kombani anasema hakuna haja ya katiba.
Hawa mawaziri wengine wanatolewa wapi? Haya ndo matatizo ya mfumo huu haki sawa kwa wote unaleta mawaziri wengine kichwani hakuna kitu.

Pindi yuko makini hakurupuki.safi
 
suala la katiba ni la wananchi serikali ni chombo ya kusimamia mchakato unaohusu katiba, suala la mabadiliko kuwa ni MADOGO au MAKUBWA sio la serikali wananchi ndio tutaamua.
 

Kibangusilo Pinda!!! Hivi hizo ripoti walipoletewa hawakuzipitia......................?? Sasa wanataka kuunda jopo la wataalamu kupitia ripoti.....Mimi nilifikiri tume inapoundwa huwa inakuja na findings pamoja na suggestions?? Sasa kwa nini tena tutafute wataalamu wengine kuzipitia?? Au ndio sasa wanazitoa kwenye makabati zikiwa na vumbi tele???

Hivi kweli amekumbuka kuwambia wananchi hizo pesa za jopo la wataalamu zitatoka wapi?? Maana waziri wake alishasema hawana pesa!!!
 
Wanatafuta kupachika OIC na kadhi kama Kenya. Sitaki katiba mpya kwa sababu hiyo tu
unajua taifa linapoangalia mustakabali wake kwa ujumla halafu mtu anakuja na kaseksheni kamoja anakoamua kukashabikia na kuharibu maana nzima ya katiba na nchi zima inakera sana

wewe badala ya kufikiria nafasi na wajibu wako kwenye kusaidia nchi kuondoka kwenye undundu tulio nao leo, unakuja na madudu kama haya

watu kama nyinyi ndio mnamfanya JK aonekane genious na wengine wote mbayuwayu
 

Mkuu,

Naomba nitofautiane na wewe kwa kauli hii,”Serikali yanywea katiba mpya”. Wanachojaribu ni kuwapoza wadanganyika kuwa this time wamesikia vilio, mayowe ya katiba mpya , lakini kunywea, hapana!

Pia umeona Wana CCM wengi wanajitokeza katika mchezo huu wa maigizo,wanasema ,yah, tupate katiba mpya, tuifanyie marekebisho. Wanajaribu kuuteka nyara mjadala wa katiba na wameanza kufanikiwa,.title yako inaashiria hivyo.

Ukweli CCM na serikali itarudi katika drawing board yao na kupanga mkakati kabambe wa how they can screw better wadai katiba mpya . Maybe we underestimate CCM.
 
Niliandika hapa kwamba moto kuhusu katiba mpya uliowashwa na CHADEMA hakuna wa kuuzima. Sasa ni kuendelea kuishinikiza Serikali kwamba hatutaki kuongeza viraka kwenye katiba mpya ambavyo vinavyoulizana mwenzangu umekuja lini, bali tunataka katiba mpya ambayo itaendana na hali halisi ya siasa za vyama vingi nchini na pia kuhakikisha katiba hiyo inapatikana kabla ya uchaguzi ujao 2015. Hongera sana CHADEMA juhudi zenu taratibu zinazaa matunda.
 
Kwanini Kombani asijuuzuru uwaziri!!
ukiondoa lile gari na ofisi kwani anajua hata kama yeye ni waziri?? yeye anachojua katumwa na kikwete kufanya kazi... kazi ipi... hilo swali gumu
 
pinda ni makin
Alisema hataki magari ya kifahari bado yanendelea kununuliwa, akasema hawezi kuwakamata mafisadi kwa sabau wananguvu wana weza kutetemesha nchi, niambie umakini wake uko wapi au anapoanza kulia kulia bungeni......mimi nilikuwa na mwania sana ila kadiri siku zinavyoenda na mwana nayeye siyo...
 
Kukubaliana na hoja ni hatua moja kubwa ingawa utekelezaji na namna itakavyotekelezwa ni suala lingine. CCM naamini wanaipedna nchi hii kama raia wengine wote. Hawawezi wakafanya kosa la kuichezea katiba ambayo kama itatokea madaraka akayapata mwendawazimu basi atawachapa wote hata hao watunga katiba.
Katiba lazima iwe kweli ni katiba isiyo na longo longo.
 
Kwanini Kombani asijuuzuru uwaziri!!

kwa sababu hata yeye tamko lake la awali lilikuwa ni la kutumwa tu

wa kulaumiwa ni serikali nzima kwa ku flip flop
 
Serikali hivi sasa (ukimsikiliza Pinda kwa makini) ipo kwenye damage control kutokana na maneno ya Kombani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…