Ngambo Ngali
JF-Expert Member
- Apr 17, 2009
- 3,517
- 1,363
Niliandika hapa kwamba moto kuhusu katiba mpya uliowashwa na CHADEMA hakuna wa kuuzima. Sasa ni kuendelea kuishinikiza Serikali kwamba hatutaki kuongeza viraka kwenye katiba mpya ambavyo vinavyoulizana mwenzangu umekuja lini, bali tunataka katiba mpya ambayo itaendana na hali halisi ya siasa za vyama vingi nchini na pia kuhakikisha katiba hiyo inapatikana kabla ya uchaguzi ujao 2015. Hongera sana CHADEMA juhudi zenu taratibu zinazaa matunda.
Lazima kuwe na time frame kwamba katiba mpya itapatikana lini, vinginevyo wadanganyika watasubiri kama wazee wa jumuiya ya afrika mashariki
Bila samahani Mkuu. Ni kweli kabisa hili la katiba mpya ni swala linalohusu umma wote wa Watanzania ambao wana mapenzi ya kweli na nchi yetu na si la CHADEMA au CCM tu. na sikutaka kumaanisha kwamba issue hii inaihusu CHADEMA tu. Pamoja na Watanzania wengi kuipigia kelele katina iliyopo na kutaka iundwe katiba hii, safari hii chokochoko hizi za kuishinikiza Serikali kuhusu katiba mpya zilianzishwa rasmi na CHADEMA mara tu baada ya matokeo ya uchaguzi kutangazwa. Hivyo sioni ubaya wowote wa kuipongeza CHADEMA kama waanzilishi wa chokochoko hizi ambazo taratibu zinaanza kuzaa matunda.
Naam NN, CCM hawaoni kama kuna haraka yoyote ya kuwa na katiba mpya wako tayari kusubiri hata 2050 maana wanajua wazi kwamba katiba iliyokuwepo inawapa mianya mingi ya kuendelea kuwepo madarakani na hata kupata kiburi cha kutamka kwamba, CCM itatawala milele.
Baada ya kilio cha muda mrefu cha madai ya Katiba, hatimae hii leo serikali ya Tanzania imekiri kuwa ipo haja ya kuifanyia mabadiliko Katiba ya sasa ili iweze kukidhi mahitaji na mabadiliko ya sasa.
Akiongea na wahariri wa vyombo vya habari leo Jijini Dar es Salaam, Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda amesema serikali itaunda jopo la wataalam kupitia mapendekezo ya awali na ya sasa yaliyotolewa kuhusiana na mabadiliko ya Katiba.
Hata hivyo Mh. Pinda amesema serikali bado haina jibu iwapo yafanyike mabadiliko makubwa ama mabadiliko madogo kutokana na mapendekezo yaliyokwishatolewa, au suala hilo lipelekwe bungeni ama lirudishwe kwa wananchi kwa maamuzi.
Source-Mimi
Kweli ndugu si busara kumkabidhi fisi kulinda Bucha!Wakuu, mnafikiri ni busara kwa CCM ku-lead hii process ya mabadiliko ya katiba?
Mnafikiri tupo tayari kwa sasa? mnafikiri wananchi wanajua katiba ina matatizo gani?
CCM ipo very strategic, mnafikiri itajitengenezea kaburi lake yenyewe?
Nipo skeptic kidogo on this one. Sorry.
Kumbuka kwambaNaomba nirudie maneno yangu tena. Chini ya utawala wa CCM hakutakuwa na katiba mpya hiyo ya pinda ni danganya toto tu. watakachofanya ni kuiwekea viraka tu, ili kuwatuliza wananchi. CCM will never dig is own grave.
Hapana tunaweza kupata katiba MPYA kabisa chini ya uongozi wa CCM! lakini lazima kutakuwa na vifungu vitakavyoilinda CCM au viongozi wake!Naomba nirudie maneno yangu tena. Chini ya utawala wa CCM hakutakuwa na katiba mpya hiyo ya pinda ni danganya toto tu. watakachofanya ni kuiwekea viraka tu, ili kuwatuliza wananchi. CCM will never dig is own grave.
Wanatafuta kupachika OIC na kadhi kama Kenya. Sitaki katiba mpya kwa sababu hiyo tu
uongo, kasema:Pinda: Serikali kuunda jopo kuchunguza madai ya katiba mpya
Yes kama wakiweza kuandika katiba still itailinda CCM 100%. Jamani kama waliweza kucheza na akili zetu wakati wa uchaguzi na kuonyesha kama matokeo yalikuwa poa. ndivyo hivyo itakavyokuwa hata katiba watakuja na lugha tamu na laini, Na kwa sababu watanzania wengi si watu wakuchambua mambo kwa undani na ni watu wa 'NDIYO MZEE'Hapana tunaweza kupata katiba MPYA kabisa chini ya uongozi wa CCM! lakini lazima kutakuwa na vifungu vitakavyoilinda CCM au viongozi wake!