Mheshimiwa Pinda: Ya Ze Comedy tuwaachie kina Joti na Masanja
19 May 2009
Na Andrew Mushi
OKTOBA 22 mwaka jana, Waziri Mkuu , Mizengo Pinda (MP), alitembelea Wilaya ya Hai , Mkoa wa Kilimanjaro, pamoja na shughuli mbalimbali alizofanya , alisomewa taarifa ya Wilaya.
Taarifa inafikia zaidi ya kurasa arobaini. Nasema zaidi ya 40 kwa sababu sikupata nakala halisi ya hii taarifa ila nimetumia iliyoko katika mtandao wa tovuti (wavuti), ambapo nilipojaribu kuiweka katika kurasa za kawaida ilifikia kurasa 50.
Wakati nasoma hii taarifa , niliwaza juu ya hotuba na taarifa mbalimbali viongozi wanazosomeana na kutusomea (kuhutubia). Mojawapo ya nilichokiwaza sana , ni kama kweli hii hotuba yote aliyosomewa Waziri Mkuu na Uongozi wa Wilaya ilichukua muda gani kumalizika? Na je, Waziri Mkuu hakusinzia, ingekuwa mimi nina uhakika ningelala fofo na kukoroma.
Mawazo yaliyonijia ndio ninataka kujadili na wewe ndugu yangu unayesoma makala hii. Najua utakuwa na mengi tena zaidi yangu ambayo umekuwa ukiwaza na kuwazua.
Kila siku ijayo kwa Mungu , Tanzania kuna hotuba na risala nyingi zinasomwa na wananchi kwa viongozi wao, na viongozi nao wanapokea hii ngonjera kwa kuwatolea ngonjera yake. Basi hali mradi tumefungua kinywa kusema chochote. Siku unajua tena hizi ni zama za semina elekezi. Kama zisingekuwa ngonjera, tungekuwa tuko mbali.
Kuanzia Rais Mpaka Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wanazunguka huko na huko kukagua na kuhamasisha shughuli za maendeleo , na kila mmoja anasoma na kupokea risala. Sasa cha kuchekesha ni huu mchezo ninaouita Ze Comedy ya hizi hotuba.
Kwanza hizi hotuba ni zile zile, nikitumia mfano wa ile hotuba ya Hai, akija Rais kesho atasomewa hiyo hiyo, Mkuu wa Mkoa naye akija hiyo. Akija waziri wa wizara yeyote ile vitanyofolewa vifungu vyake na kusomewa, Mwenge ukija nao ndio usiseme. Kwa kifupi kinachofanyika ni kubadili tarehe na mlengwa.
Mara nyingi hatujiulizi umuhimu wa hotuba mbali mbali tunazosomeana katika shughuli mbali za kisiasa na maeendeleo. Mara nyingi hizi taarifa ndefu ni mazoea yasiyokuwa na tija wala hayatupeleki popote.
Ndio maana ukifika katika hizi shughuli wakati wa kusomeana hizi hotuba na taarifa kwa wastani hakuna anayesiliza, ndio maana nikaziita ze comedy. Tena afadhali ya Ze Comedy inaburudisha, tofauti na hizi hotuba zinazoumiza na kuchosha masikio.
Mara nyingi nimesikia watu wakiwalumu Wabunge kwa kusinzia Bungeni, ila mie nimekuwa mzito kuwalaumu, kiasi fulani, naelekea kuwaunga mkono. Wewe niambie unaposikiliza bunge letu, ingekuwa ni wewe ni kitu gani kingekufnaya usisinzie. Kama ni hotuba ya bajeti, unajua Waziri alichosema mwaka juzi na mwaka jana ndio atakachokirudia.
Kama anajibu swali, hataenda mbali zaidi ya ile story ya siku zote kuwa barabara korofi ya kwenda Busanda au Biharamulo inashughulikiwa, na Mheshimiwa Mbunge avute subira, sasa akivuta subira kwa kulala kidogo ana kosa gani-embu tuacheni kuwaonea Wabunge.
Wewe ona kunapokuwa na mijadala motomoto kama wakati wa kujadili Richmond mwezi Febuari mwaka jana, nani alisinzia-hamna!
Kwa wanaomjua Rais Museveni wa Uganda, akiwa katika shughuli na mtu anatoa hotuba au longolongolo, yeye hufumba macho na hata ikibidi husizia kabisa. Ukiona hivi,ujue anakuambia kama huna cha maana cha kusema ishia hapo. Mapema Febuari mwaka huu, Rais Gaddafi wa Libya alipochaguliwa Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika alitoa hotuba ndefu sana iliyoenda mpaka usiku wa manane. Marais wengi wakasinzia. Ila yalipomshinda Museveni, alimfuata Gaddafi jukwaani, akamwambia maliza, tunataka kwenda kulala. Naye akawa mpole, akamaliza.
Tuyaache ya Museveni turudi kwetu. Cha kuchekesha zaidi, mara nyingi wanaosomewa hizi hotuba ndio wao wameziandika. Nikupe data kidogo. Mfano, kama Waziri fulani amealikwa kuwa mgeni rasmi katika shughuli iliyoandaliwa na NGO fulani. Ile NGO itaandaa hotuba mbili, moja ya kwao ya kumsomea mgeni rasmi, na nyingine ya mgeni rasmi kwa ajili ya kujibu ile ya kwao, ila yeye atamalizia kwa kusema, natangaza , washa hii imefunguliwa au imefungwa rasmi. Makofi, kisha kila mmoja atatawanyika kwenda kusubiri hotuba nyingine.
Sasa niambie, katika hali kama hii, huyu waziri anawajibika kutekeleza nini katika hotuba ambayo hakuiandaa. Sidhani, hata kama ukimuuliza kesho yake, katika ile hotuba nini alichosema, kama atakuambia-hakumbuki!
Hali haishii hapo tu. Katika hizi hotuba zinazosomwa zisizokuwa na miguu wala kichwa, kuna utamaduni wa kulipwa posho kwa kufanya hiyo shughuli nzito ya kuhutubia. Huu mchezo uko kwa mawaziri mpaka viongozi wa ngazi ya chini kabisa. Nina uhakika, Rais, Makamu wa Rais, na Waziri Mkuu hili hawahusiki. Ila mawaziri, makatibu wakuu, wakurugenzi, maofisa, bila bahasha hajakufungulia au kukufungia warsha yako kama hana uhakika wa bahasha.
Kama huamini, kamuulize mtu yeyote aliyekwisha kuandaa warsha au kongamano. Mbaya zaidi, wengine wanauliza bahasha yangu ina bei gani, akiambiwa bei ni ndogo hasemi ongeza, ila anasema siku hiyo atakuwa na shughuli nyingine, atamtuma mtu wa ngazi ya chini (wa bei hiyo), na unajua ukipata wa ngazi ya chini na shughuli yako itaonekana ya chini, hata kwenye TV haitoki.
Mimi nashawishika kusema tumeongea na kusundubua sana, inabidi tubadilishe hii tabia, tena sio tabia tena, bali imeshakuwa ni utamaduni. Tuwe na hotuba zinazoruhusu kushikishana na kujadiliana zaidi. Na kama ukiamua kuyapa tafsiri sahihi ya yanayotokea sehemu nyingi za Tanzania, utagundua wananchi wako mbele hatua moja zaidi ya viongozi. Sidhani kama inaisha wiki bila vyombo vya habari kutueleza kiongozi huyu au yule amezomewa .
Hii kuzomea zomea, wakati mwingine sio kuwa wananchi hawataki kusikia kiongozi akiongea, la hasha! Wanataka staili mpya ya kuongea. Hawataki hotuba, wanataka mazungumzo na mijadala. Uzuri wa mazungunzo na mijadala, mara nyingi inapelekea pande zote zilizoshiriki kuchukua hatua. Upande wa hotuba , unapoweka nukta, na ndio mwisho wa kila kitu.
Wananchi wanataka kujadiliana ili kujua njia za kutatua matatizo yao ya kila siku. Hii mara chama changu, shirika langu, litawafanyia hivi au vile, litawaletea hiki, hawataki, maana licha ya kujua ni kuwazuga tu, wanajua hata mwenyewe humaanishi unachoongea. Japo mdomo wako unakitamka, wakikuangalia usoni, wanaona sura na macho yako yanakana mdomo ulichotamka.
Nina uhakika Waziri Mkuu anaweza akafungulia njia na kutuletea njia mbadala katika hizi hotuba na taarifa. Kwa watu wanaomjua Mh. Pinda, watakubaliana na mimi kuwa sio mtu wa longolongo na haendekezi longolongo. Na ninamsikitikia sana anavyoweza kusikiliza hizi Ze Comedy kila siku. Najua anajionea kero tu.
Pinda siku zote amekuwa ni mtu wa maneno mafupi lakini yenye vitendo. Nina uhakika akipania tunaweza ndani ya muda mfupi tukajikuta tunaacha kupoteza muda na kuchoshana. Tukajikuta tunakuwa na utamaduni mpya wa kupeana taarifa na mipangilio ya kazi bila maneno mengi yasiyo na kichwa wala mkia.
Kwangu huu ni ufisadi. Kila siku tunafikiri ufisadi ni kukwapua pesa za EPA na Richmond tu. Hapana, ni pamoja na huku kuchorana katika hizi hadithi za akaenda, akaenda, akaenda na hadithi yangu ikaishia hapo.
Nani hajui, huduma za afya, elimu, barabara, na nyinginezo hazitoshi. Kwa nini kurudia rudia maneno kama kasuku. Tutumie muda mwingi kupanga mipango inayotekelezeka, ya Ze Comedy tuwaachie kina Joti, Mpoki na Masanja.
amushi1@yahoo.com