Pindi Chana apokelewa kwa shangwe za Utamaduni na Sanaa

Pindi Chana apokelewa kwa shangwe za Utamaduni na Sanaa

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2013
Posts
790
Reaction score
964
Mhe.Chana Apokelewa kwa Shangwe za Utamaduni na Sanaa

Na Shamimu Nyaki

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana leo Februari 17, 2023 amewasili kwa mara ya kwanza wizarani hapo baada ya Kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan hivi karibuni kuiongoza wizara hiyo.

Mara baada ya kupokelewa na Mtangulizi wake Mhe. Mohamed Mchengerwa ambaye sasa ni Waziri wa Maliasili na Utalii, amejionea burudani nzuri kabisa kutoka kwa watumishi wa wizara hiyo waliobobea katika Sekta za Utamaduni na Sanaa.

Watumishi walimpokea kwa ngoma, nyimbo utenzi na majigambo yaliyoongozwa na Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Sanaa Dkt. Asha Salum

Mapokezi ya Mhe. Waziri yalipambwa pia kwa nyimbo zenye ujumbe wa ukaribisho ambazo ziliimbwa na Maafisa Utamaduni wa Wizara hiyo.

IMG-20230217-WA0661.jpg

IMG-20230217-WA0663.jpg
IMG-20230217-WA0662.jpg
IMG-20230217-WA0615(2).jpg
 
Wanafiki katika viwango vyao!
Nchi hii bila kuwa mnafiki.....

Mambo hayaendi,kila mtumishi anawaza ulaji,uteuzi nk.

Tena hao wapiga ngoma ndio wapika majungu,kama wanavyop9ga hizo ngoma!

Ila ukweli ni kwamba alieondoka hakuwa kipenzi chao,alijaa dharau shauri anapiga nyumbani kwa mama mkwe!
 
Back
Top Bottom