Naandika makala hii nikiwa kitandani kwangu vyeti vyangu vya chuo kabatini kwangu,miezi saba nyumbani sina lolote sina chochote sina ajira nimekuwa mtu wa kuwaza hivi kesho yangu ikoje.Siku zote niliamini kwamba nitapo maliza chuo kupata ajira kwangu itakuwa ni rahisi,niliamini haya yote huku akilini mwangu nikijua kwamba ajira ni moja ya changamoto kubwa nchini Tanzania lakini niliamini ya kwamba hali hiyo haitonikita mimi kamwe.
Mimi ni kijana niliyehitimu elimu yangu ya juu katika chuo cha Kumbukumbu ya Hubert Kairuki jijini Dar es Salaam nimesomea udaktari na nina Shahada ya Udaktari nimemaliza elimu yangu ya juu mwaka 2020 na kufanya utarajali(internship) wa mwaka mmoja.
Baada ya kumaliza utarajali nilianza na utafitaji wa ajira lakini mbio hizo za kutafuta ajira hazijaa matunda mpaka sasa ninavyo andika makala hii.Hali imekua ni ngumu, kila kunapo kucha ni siku nyingine unayokumbushwa ya kwamba huna ajira,unajaribu kufikiri nje ya boksi, kufikiri namna utakvyojikwamua lakini kila suluhisho unalolipata unaona kama vile haliendani na kile ulichosomea wala hakiendani na kile ulicho tarajia na hii ni kwa sababu elimu yetu ya Tanzania haijamuandaa kijana kujiajiri bali kuajiriwa kama ilivyosemwa na watu wengi sana.
Kwa mtu aliyesomea udaktari miaka mitano kukubaliana na hali ya kwamba mimi sina ajira kwa nini nisijiajiri nianziahe biashara ndogo kama kuuza pipi, biskuti, juisi au nifungue genge la kuuza mbogamboga na kadhalika hizi ni fursa nzuri lakini kijana ukianza kufikiri niuze pipi na biskuti wakati una elimu yako nzuri inakuwa ni vigumu kukubaliana na hali halisi ya maisha.
Kama watu wengine walivyo lipigia ngoma swala hili kuna haja ya serikali kubadili mitaala ya elimu au kuwandaa vijana kujiajiri badala ya kuajiriwa hayo yanawezekana kwa kuweka masomo ya stadi za kazi kama vile uchongaji vinyago, uchoraji, kudarizi,ushonaji na kadhalika.Masomo ya biashara pia yanayofundishwa pia yajumuishe elimu ya ujasilimali ili kijana aweze kujua kwamba hata wewe pia ni mtaji na kumfanya kijana kujiamini katika kuanza na kufanya biashara. Ningepata elimu hii wakati nipo shule ingenisidia sana mbeleni.
Kama kijana pana haja ya kuwa na uwezo mpana wa kufikiri unaweza kuanza kufanya kazi ndogo ndogo wakati huo huo ukiendelea kutafuta kazi, huwezi jua huko unakofanya biashara ndogo ndogo ndipo utapokutana na mtu au watu watakao kusaidia kufika mbali kwani “Haba na haba hujaza kibaba”.
Vijana kuwa na mtazamo mpya wa kufikiri kuhusu soko la ajira. Ninamaanisha badala ya kuwaza fursa za ajira ambazo zimekwishatengenezwa tayari katika soko la ajira na ni chache, vija atuanze kuwa ni njia gani bora zitasaidia kutengeneza fursa nyingine nyingi za ajira kwa vijana wengine. Tuanche kupoteza muda kuzunguka na CV na vyeti.
Tuwe “INNOVATIVE” Hapa simaanishi kuwa wagunduzi kama inavyofahamika na wengi. Ninamaanisha kuwa na uwezo wa kuhawilisha mawazo [yaliyogundulika tayari katika ubongo wako], ili kuwa na wateja (Customers) wengi watakaoyaunga mkono mawazo yako. Hapa ndipo pale unapopaswa kuongeza
Uwezo wa kuhawilisha wazo ili utumie mtaji wa mtu mwingine (Maana wewe hauna mtaji). Wazo likihawilishwa vizuri litapata mteja (mwenye pesa ambaye atahamasika kulidhamini wazo lako).
• Uwezo wa kutumia Ardhi ya mtu kwa wazo ulilolipata (maana huna Ardhi)
• Uwezo wa kutumia mfanyakazi (kwa kumshawishi mwenzako kutumia wazo lako na hivyo kujitoa kufanya kazi maana baada ya muda si mrefu wazo lako litaanza kuingiza kipato kikubwa).
Kutumia akili sawa sawa na wakati tulionao. kwa mfano, zama tulizonazo ni za Sayansi na Teknolojia na hivyo vijana na wanadamu wengi hawapendi tena kusoma soma maana wamehamia katika Digitali. Hata mawazo yako inabidi yaendane na wakati uliopo ili kuliteka soko.
ACHA KUJIPUNGUZIA MSUKUMO WAKO WA NDANI KWA SABABU HAUNA MTAJi (PESA). HAWILISHA MAWAZO ULIYONAYO. NI MTAJI TOSHA.

Upvote
4