Pinpin Camara ataibuka shujaa kwenye derby ya leo

Pinpin Camara ataibuka shujaa kwenye derby ya leo

Metronidazole 400mg

JF-Expert Member
Joined
Aug 25, 2016
Posts
941
Reaction score
2,062
Sifa kuu ya mechi ya karikoo derby ambayo wachambuzi wengi wameshindwa kuling'amua kabisa ( wao wanaongolea mifumo, makocha na historia ya mechi zilizopita )....Kuna kitu Cha muhimu Sana Huwa akiongelewi kabisa nacho ni

UTULIVU, UTULIVU, UTULIVU

Kwanini??
Simba na Yanga siku zote zinapokutana ni Kama fainali yaani ni kufa kupona, na wachezaji wanatumia uwezo wao wote kuhakikisha timu Yao inapata kitu

Binafsi nimeangalia derby nyingi Sanaa za Simba Vs Yanga kinachohukumu timu ipi kati ya hizi mbili, nani ashinde ni UTULIVU wa mchezaji mmoja mmoja

UTULIVU unahusisha; kuwa position sahihi, kutekeleza majukumu ya msingi uliyopangiwa na kufanya maamuzi sahihi muda wote wa michezo (Ukifanya vice versa football pressure inakuwa kwenu mwisho wa siku mtafungwa TU )

Kufupisha hoja hii; a)mnapokosa nafasi nyingi za kufunga, mnakaribisha hatari ya kupoteza michezo

b)mnapofanya makosa ya kiulinzi na kimfumo, mnakaribisha pia hatari ya kufungwa

Kwanini PINPIN CAMARA??

Huyu jamaa ana sifa kubwa Sana ya UTULIVU na anajua wakati wa kuituliza timu inapokuwa kwenye presha ( rejea mechi VS Al ahly tripoli away )

Ukitaka uone ubora wake SIMBA wakitangulia kupata goli, ndio utaona ubora wa huyu jamaa utaona kipaji chake......na naweka utabiri hapa hukipitia huyu huyu kipa

Ofcoz mechi itakuwa ngumu ila Sasa;

Kama Simba atatangulia kupata goli ( haijalishi kipindi gani aidha iwe Cha kwanza/pili ) kwenye michezo wa Leo ATAIBUKA MSHINDI .......sababu nimeitoa,ok Sasa wazee wa mikeka password hii hapa msisahau kuja kunishukuru ikitiki
 
Huyo PINPIN CAMARA ndiyo yule aliyetobolewa na Max Nzengeli kwenye mechi ya Ngao ya jamii, au huyu ni mwingine?
 
Back
Top Bottom