Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,599
- 9,532
Maandalizi; dakika 5
Muda wa kupika; dakika 10
Muda jumla; dakika 15
Mahitaji
1. Ndizi mzuzu tatu kubwa
2. Vijiko 4 vya chakula chenga za mkate
3. Mafuta ya kutosha ya kukaangia
4. Chumvi au viungo vingine
Maelekezo
1. Menya na kukatakata ndizi umbo la chispi kubwa kubwa kiasi; nyunyizia chumvi na pilipili manga uchanganye vizuri
2. Kwenye kikaangio kikubwa moto wa juu kiasi, weka mafuta ya kupikia acha yachemke vizuri. Wakati mafuta yanachemka, chovya vipande vya ndizi kwenye chenga za mkate hadi zifunikwe vizuri, kandamiza na mkono chenga zishike kwenye ndizi vizuri.
3. Kaanga kwa dakika mbili upande wa kwanza, geuza kwa dakika moja upande wa pili, au mpaka ziive ziwe na rangi ya kahawia.
4. Ipua kutoka kwenye mafuta, ziweke kwenye sahani yenye tissues zichuje mafuta.
Jikoni na jane