Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,599
- 9,532
Jinsi ya kutengeneza Kalimati ya maharage:
Maharage yanatumika katika mapishi aina nyingi sana, Leo tutapika kalimati kwa kutumia maharage!. Kaimati hii ni nzuri sana kwani ina maharage yenye protini nyingi.
Maandalizi na Mahitaji
Ingredients
Jinsi ya kutengeneza Kalimati hatua kwa hatua
Maharage yanatumika katika mapishi aina nyingi sana, Leo tutapika kalimati kwa kutumia maharage!. Kaimati hii ni nzuri sana kwani ina maharage yenye protini nyingi.
Maandalizi na Mahitaji
Ingredients
- Maharage yaliyopikwa na kuiva 1/2 kikombe.
- Maziwa safi 1/4 kikombe.
- unga wa ngano Kikombe kimoja.
- Mafuta ya kupikia.
- Chumvi kiasi.
- Yai 1.
- Baking powder 1/2 kijiko cha chai (ukipenda).
Jinsi ya kutengeneza Kalimati hatua kwa hatua
- Chemsha maharage hadi yalainike na kukauka maji.
- Maharage yakipoa songa hadi yalainike vizuri.
- Chukua Una wa ngano changanya na barking powder kisha chekecha na tia chumvi.
- Changanya unga na maharage katika bakuli kubwa safi
- Koroga yai.
- Tia yai katika mchanganyiko huo, changanya vizuri
- Tia maziwa kwenye mchanganyiko huo, hakikisha unakuwa mzito wa kutosha unaokatika ukimimina.
- Chemsha mafuta katika kikaangio chako.
- Chota na kijiko cha chakula weka kwenye mafuta yanayochemka.
- Choma mpaka ziwe za kahawia. Tayari kitafunwa.