Pishi la choroko za kupaaza

Pishi la choroko za kupaaza

Nyendo

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
1,336
Reaction score
4,731
Leo jikoni tunaandaa choroko za kupaaza, twende pamoja


Vipimo:
Choroko za kupaaza - 1 kikombe kikubwa (mug)
Kitunguu maji - 1 kimoja
Binzari ya manjano ya unga - 1/2 kijiko cha chai
Kitungu saumu (thomu/galic) - 1 kijiko cha chai
Nyanya - 1 moja
Pilipili nzima - 1-2
Chumvi - kiasi
Nazi - 1 kikopo (400-500 mls)


Namna ya kutayarisha
Osha choroko zako vizuri na zichemshe kwa maji ya kiasi tu hadi ziive na zisivurugike.
Katakata kitunguu maji vipande vidogodogo.
Imenye nyanya maganda halafu iponde.
Namna ya kupika
Weka sufuria jikoni na moto wa kiasi tia mafuta kidogo.(kijiko kikubwa cha kulia)
Kaanga vitunguu mpaka vibadilike rangi kidogo
Tia binzari ya manjano kaangia kidogo
Kisha tia vitunguu thaumu kaanga kidogo.
Halafu mimina nyanya iliyosagwa na chumvi kiasi.
Acha ikaangike huku ukikoroga.(kama dakika 5-10 hivi)
Kisha mimina choroko zilizoshemshwa changanya acha maji yakauke kiasi
Mimina nazi na onja chumvi kama imekolea punguza moto acha nazi ichemkie, kiasi cha kuacha urojo wa kutosha.
Mwisho katia pilipili ziiive kiasi.

Zikisha kuwa tayari mimina kwenye bakuli lako tayari kwa kuliwa na chapati , wali nk.

1574084545555.png
 
Napenda choroko zikichanganyiwa wakati wa kupika wali na roast ya kuku yenye nazi

Kwetu tunaita mseto [emoji39][emoji39][emoji39][emoji39],mimi napenda na mchuzi wa nazi wa samaki ziwemo na nyanya chungu au bamia [emoji39][emoji39][emoji39][emoji39] yummy yummy
 
Back
Top Bottom