Pishi la kibachelor

Mhandisi Mzalendo

JF-Expert Member
Joined
Aug 23, 2010
Posts
6,682
Reaction score
11,461
Vaaaap napitia humu kila nikitoa jicho nakuta kila pishi ni mwendo wa saa liimoja..

Hebu wadau tushirikiane mapishi ya chap chap ya ki bachelor....
Kwangu napendelea kupika.

1. Tambi, nachemsha maji naweka chumvi na sukari kidogo then bdae mafuta then tambi mwisho(though nimepata ujuzi mwingine humu) baadae nachukua mayai nakaanga huku nikichanganya na saladi.

2. Mkate uliopakwa asali ( hapa nasisitiza asali maana huwa inaongeza nguVu mwilini na kukufanya usisikie njaa mapema) mayai na saladi na kikombe changu kimoja cha kahawa iliyochanganywa na viungo basi nikikandamiza hv naitafuta asubuhi)

3. Soseji though sipendelei sana...nachanganya na pishi hzo hapo juu.

4. Ugali samaki hapa kama nina nguvu za kusonga ugali.

Hebu tuongezee na wewe huwa unajipikia nini? Fasta fasta....

Karibuni bachelors and X bachelors....
 
Pancakes na crepes pia rahisi kutengeza...

Soup ya samaki unachemsha samaki unaweka garlic chumvi na saumu then unaweka mixed vegetable ya njegere,mahindi machanga na karot then ukikaribia kuwiva unaweka ndimu....

Njaa ikinibana sana nakata salad kamili then naweka tuna fish wa kopo then juu naweka ketchup na pilipili ya kusaga

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 
Kuna hii mikate nimekula sehemu jana nikatamani sana kujua kumeki
Ni mkate wenye sandwich ya scrumbled eggs, butter, cheese, some salads, na mingine hivi ilikuwa na chicken na ham slices! Ikatolewa kwenye friji ndio tukaila. Safi yani loh, iko na shape ya triangle, hivi wanafanyeje?
 

tehe tehe, yani umeambiwa useme chakula cha kibachelor we una-complicate
 
Reactions: amu

farkhina natamani nijue hilo pishi na kuonja ladha yake ila hiyo naona kama nitatoa kitu cha ajabu....
Anyway asante nitajaribu na hii....
 
Last edited by a moderator:

Mkuu hauongelei chicken hotdog hapo...
Kwa akili yangu ya chap tu
Unachukua mkate au tuseme skonzi hata ya raundi au triangle unakata katikati, unakata saladi yako safi tu...chukua mayai yako either kaanga na kuchanganya na saladi kidogo au pekeyake then chukua nyama ya kuku isage na then mchanganyiko wote unauweka katikati ya mikate na kuifunika !! Chukua hiyo mixer then weka kwenye oven ipate moto....
Waweza kula kwa pilipili ukishushia na kinywaji...

Sijui kama nipo sahihi kwa maelezo yangu ila nadhani hzo ndio contents zake.
farkhina anaweza kutusaidia hapa!!!
 
Last edited by a moderator:

Asante sana, yani mapishi haya bwana
 
Last edited by a moderator:
tehe tehe, yani umeambiwa useme chakula cha kibachelor we una-complicate

May be ni rahisi kutengeneza ila mie wa dakika 10 nmerudi npo hoi na njaa juu na jiko linanikenulia naona kama mchanganyiko huo ni mtihani pia...
Ila there is something good we miss....
 
Asante sana, yani mapishi haya bwana

Haya mapishi pasua kichwa na kama unaishi pekeyako ni shida unajaribu kuunga kila kitu na utajifunza mapishi ya kila aina imradi siku iende tu...
Ngoja watu waje utaona mixer za ajabu za kibachela huku....
 
Supu ya nyama:
Unakata nyama robo kilo into boxes unaiweka chumvi,pilipili manga na kitunguu saumu,unaikaanga kwenye mafuta kama 5 minutes kicha unaweka mchanganyiko wa mbogamboga kama carrot,viazi na leek vilivyokatwa into boxes unaacha vikaangike 5minutes kisha unaweka maji yazibe ule mchanganyiko wako na unafunika viive.Mwisho unamaliza na parsley.
Unaweza kutumia kuku ukipenda lakini huwa natumia timian na laurylleaf kuongeza ladha.

Supu inaliwa na mkate.

Nyama na mbogamboga
Nyama robo kilo unakata into boats,unaiweka chumvi,pilipili manga,kitunguu saumu na soyasauce.Unaikaanga kwenye frying pan kama kwa dakika 5,Unaweka mchanganyiko wa mbogamboga tofauti kama baby beans,baby carrots na baby corns au vingenevyo kaanga kama dakika 10,Msosi tayari kwa kuliwa..

Napenda kula chakula hiki na wali pamoja na sweetchili sauce!

Octopus salad:
Unamtayarisha pweza na kumkata slices,Unamuweka chumvi,pilipili na ndimu na kumkaanga kwenye fryingpan na mafuta kama dakika kumi.Wakati pweza anaiva una katakata salad,pilipili hoho nyekundu,nyanya,matango na mboga nyingine ukipendelea.Pweza akishaiva unamuweka juu ya salad.Msosi tayari kwa kuliwa.Unaweza kutumia fish filet pia ukipendelea au kitoweo kingine baadala ya pweza!

Msosi huu unaweza kula na wali ukipendelea au unaweza kuchemsha pasta uchanganye na salad iwe pastasalad🙂
 
tehe tehe, yani umeambiwa useme chakula cha kibachelor we una-complicate

Hahahahhaha basi bora niseme chipsi mayai easy to make lol

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 

Shosti mate yamenitoka.....na lile biriani lako na maandazi nimekumbuka

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 

Asante sana ngoja niongeze hii kitu kwenye diary yangu ...thanks JF chef thanks mimi49
 
Last edited by a moderator:
Hahahahhaha basi bora niseme chipsi mayai easy to make lol

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums

LOL
Chips yai tena hayo makitu nayaogopa siku hz wanasema yanaharibu naniliiiu....
Nipe nyingine
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…