Pishi lingine la chapati hilo

Pishi lingine la chapati hilo

CLONEY

Senior Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
104
Reaction score
29
Jifunze au ongezea ujuzi wa pishi la chapati ,wadau pishi hilo nimelikuta hukooooo kwenye blog ya Mange nikaona nililete hapa kwenu mnaweza pata chochote.


Kuna njia tofauti za kukanda chapati zako zikawa laini, lakini siri kubwa ya kupata chapati nzuri ni kuukanda huo unga vizuri na ulainike.

Mahitaji basic:

1. Unga wa ngano
2. Chumvi
3. Sukari kidogo sana kwa ajili ya seasoning
4. Mafuta kidogo ya kukandia kulingana na unga wako, usijaze mafuta kibao
5. Maji - hapa inategemea na ukandanji wako mimi natumia maji ya baridi sana ikiwezekana nayaweka kwenye freeza kidogo yazidi kuwa baridii.

Mhitaji extraa:

Hapa ni kulingana na ufundi na uzoefu wako unaweza kuweka vitu vifuatavyo ukipenda lakini sio vyote waweza chagua kimoja

1. Tui la nazi (waweza kutumia kukandia unga badala ya maji
2. Maziwa - ukitaka kuongeza virutubisho kwenye mlo wako
3. Mayai - Na chapati inakuwa laini kama sufi, kwa sababu mayai hayafanyi chapati iwe ngumu kama ni hivyo basi hata keki zingekuwa ngumu kama jiwe.
4. Vitunguu maji - kwa ajili ya kuongeza ladha
5. Nyama ya kusaga au mboga mboga yoyote ile -kwa ajili ya kubadilisha aina za chapati sio kila siku ni chapati design ile ile tu.

Kwa basic Chapati -Stage 1:

1. Tia unga wako kwenye chombo au mashine yako ya kukandia.
2. Weka chumvi, na sukari kidogo kwa ajili ya seasoning
3. Tia mafuta kwenye unga (kwa mfano kwa unga kilo moja weka mafuta 1/4 kikombe)

4. Changanya vizuri mchanganyiko wako
5. Weka maji yako kwenye unga kidogo kidogo mpaka unga uchanganyike.
6. Unga ukishanyanganyika ukande mpaka ulainike.
7. Ukisha lainika weka kwenye friji kama nusu saa hivi, kama huna friji ufunike mahali pasipo na joto.

Stage 2:

1. Changanya unga wako vizuri kisha ukate madonge madogo madogo kiasi.
2. Chukua donge moja usukume kwenye kibao au juu ya meza iliyo safi.
3. Paka mafuta kidogo juu ya chapati yako uliyoisukuma, waweza kutumia samli au mafuta mazito kama samli.
4 Kunja chapati yako irudi katika umbo la donge tena. Hapa ndio key unaweza kufanya chapati yako ikawa ngumu au ikawa laini yenye layers.
5. Sukama tena donge lako ulilolikunja, anza na lile la kwanza.
6. Weka chapati yako kwenye chuma kikavu (frying pan) kilichopata moto, kisiwe cha baridi wala cha moto sana.
7. Ikiiva upande mmoja igeuze upande wa pili.
8. Ikishaiva pande zote weka mafuta kijiko kimoja tu kikubwa cha chakula kwenye chapati yako upande wa chini.
9. Ikunje hiyo chapati na uigeuze pande zote ipate mafuta, au waweza kuisuguasugua na kijiko chako kukahikisha upande zote zinapata mafuta na kuiva vizuri (inakuwa na rangi ya brownish)

10. Ondoa chapati yako kwenye chuma iko tayari kwa kuliwa.

Waweza kula peke yake, na chai, mchuzi wa aina yoyote ile au hata na maharagwe.

NB:
Waweza kukanda unga kwa kutumia mashine kama bread maker unachagua dough, kisha unaumonitor unga ukishakandika tu ndani ya 30 minutes unautoa ndani ya mashine na kuuweka kwenye friji kwa nusu saa. Au unaweza kukanda unga kwa kutumia mixer zile kubwa na unatoa dough maker.
Hii ni kwa wale wenye hizo mashine kama mimi. Kama huna mashine basi utaukanda unga wako kwa mikono hadi ulainike vizuri. Kulainika hapa sio kujaza maji, bali kutumia viganja vyako kuulainisha mpaka unga ukiupiga unavutika. Kisha unauacha uendelee kulainika kwa kuuweka kwenye friji.
 
Kweli kujifunza hakuishi. Sijawahi kukanda chapati kwa maji ya baridi. Natumia extra luke warm water na zinakuwa laini haswaa. Nimejifunza leo. Asante.
 
jamani mie chapati zinanishinda ..najitahidi kila kitu lakini mwisho wa siku zinzkuwa ngumu..mwishowe naamua nichemsha viazi na mihogo ndo ninywee chai

Nitajaribu na hii
 
kisa cha kuacha kujitengenezea chapati ni kwamba zinakuwa ngumu kama mikate ya enzi za kina yesu ngoja leo ni print hii lecture niweze kutengeneza kudos CLONEY for this lesson
 
Last edited by a moderator:
jamani mie chapati zinanishinda ..najitahidi kila kitu lakini mwisho wa siku zinzkuwa ngumu..mwishowe naamua nichemsha viazi na mihogo ndo ninywee chai

Nitajaribu na hii
ila kumbuka kuukanda unga wako ulainike vizuri na usiwe mgumu kama ugali wa shule
 
trick ni kwenye kukanda, unatoa pembeni kuleta kati. lakini njia rahisi zaidi ya kulainisha ni kwa kuweka mafuta ya moto sana kwenye unga. then rub in the oil (kutumia vidole tu kuchanganya na kupasua mabonge huku unanyanyua juu. hii inaingiza hewa kwenye unga ambayo inakuwa kama hamira vile)
 
tena ukipenda unaweza kuzikanda jioni ukazipika asubuhi ila hi ya kuweka kwenye friji nitaijaribu. Asante.
 
jamani mie chapati zinanishinda ..najitahidi kila kitu lakini mwisho wa siku zinzkuwa ngumu..mwishowe naamua nichemsha viazi na mihogo ndo ninywee chai

Nitajaribu na hii

Cousin... hebu njoo siku moja home nkufundishe!
 
Kweli kujifunza hakuishi. Sijawahi kukanda chapati kwa maji ya baridi. Natumia extra luke warm water na zinakuwa laini haswaa. Nimejifunza leo. Asante.
sio maji baridi tuuu yaani yawe baridiii from fridge yaani ni raha balaa
ukitaka unga umix vizuri tumia kila kitu baridiii hata mafuta ila uwe umetachemsha kitambo
 
trick ni kwenye kukanda, unatoa pembeni kuleta kati. lakini njia rahisi zaidi ya kulainisha ni kwa kuweka mafuta ya moto sana kwenye unga. then rub in the oil (kutumia vidole tu kuchanganya na kupasua mabonge huku unanyanyua juu. hii inaingiza hewa kwenye unga ambayo inakuwa kama hamira vile)
aisee mi mafuta ya moto anona majanga sana use kila kitu cold bwana....
 
khasante kwa kuniongezea ujuzi, maana toka nilipopewa fomula ya maji moto basi sikua na njia ya mkato katu shukran.
 
Kweli lazima nami nijaribu hii ya kuweka kwa friji na kutumia maji ya baridi maana ni mpya kwangu
 
Zangu ni ngano, chumvi, samli na maji baridii. You wont go wrong.

Ponda mpaka ichanganyike vizuri tia frijini for 20 minutes itoe tengeneza madonge yako round, sukuma, choma na moto wa kiasi.
 
trick ni kwenye kukanda, unatoa pembeni kuleta kati. lakini njia rahisi zaidi ya kulainisha ni kwa kuweka mafuta ya moto sana kwenye unga. then rub in the oil (kutumia vidole tu kuchanganya na kupasua mabonge huku unanyanyua juu. hii inaingiza hewa kwenye unga ambayo inakuwa kama hamira vile)

hapo umesema jambo ambalo wengi hulisahau, ili chapati iwe laini na isiyoshikamana ndani, hakikisha mafuta ni ya moto sana na unapoifanyia rising tumia finger tips hadi uchanganyike kabisa kisha ndipo utie maji na kuukanda kwa finger tips na wala usitumie palm manake kiganja hublock air spaces lakini vidole huingiza hewa. na mkandaji lazima akubuke kuukanda unga wote yaani awe anazungusha chombo chake anapokanda ili maeneo yote yiangize hewa kwa uwiano.

unga ulioingiza hewa vizuri hulainika sana na hata unapoiushika haugandi mikononi na ukiutoboa utaona tundu lake hurudi juu na hata unapoukata basi huacha vijitundu vya hewa ndani yake.

jambo jingine ni wakati wa kusukuma ili upake mafuta usipousukuma unga ukawa mpana sana na mwembamba ili uenee mafuta vizuri na usipoukunja kwa marinda madogo madogo basi chapati haiwi na layers bali itashikamana sana.
 
Asante ila hujaelezea mboga mboga NA nyama ya kusaga pia tui la nazi..tusaidie pls!


Sent from my YellowBerry 4230 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom