Pishi: Magimbi ya nazi

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
MAGIMBI YA NAZI

MAHITAJI
1. Magimbi
2. Nyama
3. Nazi
4. Nyanya za mchuzi(Tungule)
5. Kerot
6. Pilipili Boga (Pilipili hoho)
7. Kitunguu maji
8. Kitunguu thomu
9. Tangawizi
10. Nyanya ya paket
11. Chumvi
12. Royco
13. Curry Powder(Simba mbili)
14. Maji


MAANDALIZI
1. Menya na ukate magimbi yako vipande vidogo vidogo.
2. Yaoshe Mara mbili kwa maji safi kuondoa utomvu.
3. Weka kwenye sufuria na maji kiasi weka chumvi weka pembeni.
4. Kata nyama na uioshe vizuri
5. Twanga tangawizi,thomu na chumvi weka kwenye nyama.
6. Saga au para nyanya weka pembeni
7. Kata kata kitunguu maji,Pilipili Boga na kerot weka pembeni
8. Kuna Nazi chuja tui zito na jepesi weka pembeni.


JINSI YA KUPIKA
1. Chemsha nyama hadi Iive
2. Weka nyanya, kerot,Pilipili boga na kitunguu maji
3. Acha mchanganyiko uchemke kisha weka nyanya ya paket,royco na Carry powder.
4. Baada ya kuiva epua hakikisha mchuzi unakuwa mzito mzito.
5.Chemsha magimbi hadi yaive kisha mwaga maji.
6. Weka tui jepesi Na chumvi acha lichemke vizuri
7.Mimina tui zito acha lichemke kidogo
8. Mimina mchuzi wako acha kama dakika tatu epua.
9. Acha kidogo vijishike kisha paka tayari kwa kula.
 
Kesho j2 ntakupostia kapicha...ngoja nimwonyeshe wife.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…