PISHI: Ndizi nyama zenye nazi na maziwa

PISHI: Ndizi nyama zenye nazi na maziwa

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Huu ni mlo wa kuliwa na watu wawili. Kama watu ni wengi ongeza idadi ya ndizi na nyama.

MAHITAJI YA CHAKULA HIKI
  • Ndizi mbichi 4 (nimetumia ndizi malindi), menya na kata vipande vidogo, hifadhi kwenye maji
  • Vitunguu maji 2, menya na kata vipande vidogo
  • Pilipili hoho (Nimetumia 2 za rangi tofauti), menya kata vipande, mie nimekata virefu vyembamba
  • Tui la nazi kikombe 1 (Kama hutumii nazi unaweza kutumia karanga)
  • Maziwa ya mgando (sour cream) ½ kikombe, au unaweza kutumia maziwa fresh
  • Nyama ½ kilo (Nyama mchanganyiko itakuwa vizuri ili kuwa na supu nzuri zaidi)
  • Karoti 2, zimenywe na kukatwa vipande vidogo
  • Chumvi
  • Nyanya 4 (Au tomato paste), menya, kata vipande vidogo au saga ikiwezekana
  • Kitunguu saumu 1, menya, ponda vizuri.
  • Tangawizi 1, imenywe, isagwe vizuri
  • Mafuta ya kula (nimetumia mafuta ya zaituni – olive oil)

HATUA ZA UANDAAJI

  • Kata nyama kwenye vipande vya wastani. Osha vizuri kisha weka chumvi, tangawizi na kitunguu saumu kidogo sana ili kuweka ladha. Usitumie kitunguu saumu chote, kitatumika kwenye kupikia. Bandika nyama jikoni, usiongeze maji. Acha ichemke hadi maji yake yakauke. Ongeza maji mengine ili nyama iive vizuri (kama kikombe kimoja).
  • Weka sufuria yenye ndizi jikoni, ongeza chumvi kiasi. Acha zichemke vizuri hadi ziive. Zikiiva epua weka pembeni.
  • Bandika sufuria jikoni, weka mafuta ya kula kiasi. Yakichemka weka kitunguu saumu, koroga. Weka kitunguu maji. Koroga, acha viive na kulaikia kiasi – takribani dakika 3. Ongeza chumvi kiasi. Ongeza nyanya, koroga kiasi kisha funika acha ziive vizuri.
Kama ni fresh tomato unaweza kuziponda ili zilainike na kuwa uji baada ya muda, kama ni tomato paste acha ziive tu. Hakikisha hazikauki na kuungua tu, unaweza kuongeza maji kiasi au supu ya nyama ili ziendelee kuiva vizuri.
  • Baada ya dakika kama 8 hadi 10 baada ya nyanya kuchemka, ongeza pilipili hoho na karoti. Koroga vizuri kisha funika.
  • Sauce ya nyanya ikishaiva, mimina ndizi kwenye sauce, kisha mimina nyama iliyoiva na supu yake. Koroga pamoja vizuri. Weka tui la nazi. Koroga hadi tui lianze kuchemka, kisha funika kwa dakika 5 ili tui lichanganyike na chakula.
  • Weka maziwa ya mgando (sour cream) kisha koroga vizuri ili lipate kuchanganyika. Acha ichemke kwa dakika 3 hadi 5. Epua chakula kitakuwa tayari kuliwa.
  • Hiki ni chakula kamili, ila unaweza kula pamoja na vitu vingine mfano mkate, chapati, maandazi, au hata wali na ugali. Ni chaguo lako. Jirambe na ladha ya maisha

misosi tz
 
Mbali na ingredient zote hizo, je kuna ubaya gani nikiongezea na zabibu kavu?
 
Back
Top Bottom