Pita hapa kuongeza siku za kuishi

Pita hapa kuongeza siku za kuishi

IAmShedeOne

JF-Expert Member
Joined
Jul 2, 2015
Posts
202
Reaction score
385
NDO MAANA NALIA...!!!!
Wakiwa wamelala, mke aliota ndoto mbaya.
Kwa wahka na kihoro, alikurupuka usingizini na kuanza kulia.
Mumewe alimtuliza na kumuuliza kwanini analia.
Mke akajibu: "Nimeota nilikuwa naondoka na kijana mmoja tajiri na mtanashati sana, aliyenishawishi nikuache ili anioe yeye."
Mume akasema: "Aah, usijali mke wangu. Hiyo ni ndoto tu, siyo kweli."
Mke akajibu kwa ghadhabu: "Najua siyo kweli, ndo maana nalia." [emoji24]

Mtoto alizaliwa, Ghafla akaanza kuongea:-
Mimi nitaishi 4 days,
Mum atakufa 6 days later na
Dad atakufa 15 days later
After 4 days, mtoto akafa.
6 days later Mama akafa.
Baba akajua next ni yeye, akauza everything, akaponda raha. After 15 days, ni Jirani yake ndio alikufa...!!!!
Watu wazima wenzangu watakuwa wameelewa...!!! [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]

Leo kidogo nipigwe na MWANAMKE baada ya LIFTI kusimama...wakati tupo kwenye lift Nilikua nayaangalia MAZIWA yake akasema "Bonyeza Moja" mi si nikalibonyeza...?
Yaani hadi sasa bado najiuliza nilipokosea. [emoji23] [emoji23] [emoji23]

TOFAUTI YA UKOPAJI, MZUNGU NA MSWAHILI:
MZUNGU:- Hi, I need $100, will pay back on Monday.
MSWAHILI:- Kaka vipi, shwari? Dah.. hatuonani mzee, mishe vipi, mnatunyima nini? Juzi nimekuona kwa mbaaali… mzee shavu dodo, full kipupwe! Sie tupo bwana, shida tu, afu misiba mingi tu, wife nae kajifungua ghafla. Sasa, kuna cheque naisubiri haijatoka hadi leo, wanasema itatoka next week, hapa nimekwama kweli. Naweza pata 'Laki Moja' ya karibu hapo nitarudisha mwisho wa mwezi…?[emoji23]

.
Stress ni nini??
Stress ni pale unapomtupia jiwe rafiki yako kwa masihara, linamkosa, linampiga bibi mzee aliyekuwa anakatiza, yule bibi analiokota na kulitia kwenye mkoba wake...![emoji23]
.
UCHAWI UPO
Unafanya Sex Na Demu Wako Ata Siku 100
Hapati Mimba...
Fanya Sasa Na House Girl
Utasikia:- Baba Mimi Sizioni Siku Zangu...! [emoji1]
House Girl Bwana
Nyinyi mna Nini!?
[emoji125] [emoji125] [emoji125]

.
Mheshimiwa mmoja baada ya kupata cheo si akapewa nyumba mitaa ya watu wenye pesa, akahamia huko akiwa na mke na mwanae. Siku moja mwanae aliyekuwa kazoea maisha ya Uswazi akawa anawinda ndege na manati kwenye uwanja wa jumba lao, bahati mbaya jiwe likapitiliza na kwenda kuvunja kioo cha nyumba ya jirani.
Mheshimiwa na mkewe wakaamua kumfuata mwenye nyumba wakamuombe msamaha.
Walipogonga mlango akafungua mbaba mmoja akawakaribisha kwa heshima, wakaingia na kuanza kujieleza. ‘Samahani sisi tumehamia karibuni hapo nyumba ya pili, mwanetu kavunja kioo chako kwa bahati mbaya, tumekuja kuomba msamaha na kuona kama tunaweza kutengeneza’.
Mwenyeji wao akawaomba wakae kisha akawaambia, ‘Naomba niwahadithie kitu. Kwanza mimi nawashukuru nyinyi na mtoto wenu. Mwenye nyumba hii ni mchawi mkubwa sana, mimi ni ZIMWI alikuwa amenifungiwa kwa zaidi ya miaka 200 kwenye kichupa ambacho kilikuwa kwenye dirisha lililovunjwa na chupa nayo ikavunjika nami nimekuwa huru, kwa hiyo kwa shukurani ombeni chochote mtakacho nitawapa, nina uwezo huo’
Hapo hapo muheshimiwa akauliza tena ’Yaani kitu chochote?’ Akajibiwa ‘Ndio’. Basi pale pale akasema, ’ Mimi naomba niwe bilionea mpaka nife’ Akajibiwa ,’ Hilo jambo dogo sana kwangu, umepata na kesho utaamka tajiri’ Mama nae akaomba vyake, ‘Mi nataka niwe na nyumba kila nchi duniani na niwe na biashara Dubai na China na HongKong’ Akajibiwa, ‘Umepata mama, kuanzia kesho hayo ni yako. Mimi nawashukuru kwa uhuru wangu lakini nina kaombi kadogo’.
Mheshimiwa haraka akajibu, ’Sema tu wewe ni kama ndugu yetu sasa’ Basi ZIMWI likasema, ‘Naomba mkeo abaki hapa kama masaa mawili tu, unajua kifungo nilichofungwa kilinizuia kila kitu, hata mke sijapata kipindi chote hicho. Nikimaliza tu hilo ntaondoka kurudi kwetu Uzimwini hamtaniona tena, itakuwa siri yetu’.
Mume na mke wakajadiliana wakaona utajiri waliopata ni mkubwa sana, na hilo jambo ni dogo sana la mara moja tu tena kwa siri, wakakubali sharti. Mke akabaki pale kwa masaa kadhaa.
Shughuli ilipokwisha, mama wa watu akiwa anajitayarisha kurudi kwa mumewe kichwani akiwaza utajiri, ZIMWI likakohoa kidogo na kumuuliza yule mama, ‘Samahani una miaka mingapi na mumeo ana miaka mingapi?” Mama wa watu akajibu, ‘Mie nina miaka 40 mume wangu ana miaka 46’ Yule Mbaba akacheka sanaa, ‘Sasa nyinyi wakubwa wazima mpaka leo mnaamini stori za MAZIMWI ?
Embu hisi kilichotokea....
.
na wewe unaweza kutuongezea usiku kwa kutiririka ha chini
 
Zimwiiiiiiiiiii.....[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
CC. Mr. Django
 
Back
Top Bottom