Pitia elimu fupi: Subaru forester 4th generation (eyesight)

Pitia elimu fupi: Subaru forester 4th generation (eyesight)

Joined
Jun 11, 2022
Posts
27
Reaction score
42
HII NDIYO FORESTER NEW MODEL (4th GENERATION)🔥🔥

FORESTER ni gari ambayo imepata umaarufu wake kutokana na Ufanisi wa Utendaji wake ambao ni thabiti hata katika barabara zenye changamoto.

Katika Toleo la NNE (SJ) Kuna maboresho ambayo yamefanyika.

Hapa tunazungumzia matoleo ambayo uzalishwaji wake ni kuanzia 2012 - 2018

Utofauti wa toleo hili na matoleo ya nyuma upo kwenye Muonekano na ukubwa kiasi ambapo 4th Generation imeongezeka kiasi.

UIMARA
Moja kati ya maboresho ni uimara wake hata inapotokea ajali ambapo hapa yamejizolea alama nzuri sana (97%) kwenye Jaribio la Kugonganisha (Crash Test).

Pia ni gari ambayo inadumu na ni moja kati ya vitu ambavyo vimewavutia wengi kumiliki SUBARU FORESTER katika Matoleo Yote.

MATUMIZI YA MAFUTA
Injini na matumizi ya mafuta ni kama ifuatavyo:
🔰PETROL
🔰MANUAL na AUTOMATIC
🔰2,000 CC inakwenda 14 Km/L
🔰Turbo na ambazo sio za Turbo

Yenye TURBO hujulikana kama SJG ambayo haina TURBO hujulikana kama SJ5.

Unaweza kuchagua kati ya FORESTER yenye TURBO kwa ajili ya nguvu zaidi au ambayo haina TURBO kwa matumizi mazuri ya mafuta.

VIFAA NA MAFUNDI
Vifaa vyake vinapatikana kwa jitihada kiasi hasa kwa mikoani na kwa kwa bei ya juu kiasi. Fanya utafiti katika mazingira yako kama unaweza kupata vifaa vyake. La sivyo utalazimika kuagiza Dar es Salaam Mwarobaini wa Vifaa vya magari 🤭😊

Mafundi wa FORESTER pia wapo jiridhishe na uwezo wa Fundi wako kabla ya kumkabidhi kutengeneza gari yako kwani mafundi wengi wamezoea mifumo ya Gari za Toyota ambayo ni Tofauti na SUBARU FORESTER

MAUA YAKE
Wamiliki wa FORESTER za Wamiliki wa FORESTER hii wanavunia Muonekano wa kuvutia sana na nafasi ya kutosha kwa ndani iliyoongenzwa kulinganisha na matoleo ya nyuma.

Inakuja na Teknolojia ya Eyesight ambayo inaboresha ufanisi wa uendeshaji kwa:
🔰Kufunga Breki za dharura
(Pre-collision Braking system)
🔰Ishara ya kuonyesha unahama
kwenye upande wako wa
kuendeshea
(Lane departure warning
system)
🔰Mfumo wa uendeshaji
kuendana na gari iliyo mbele
(Adaptive Cruise Control
system)

X-MODE: Hii ni Nyongeza ambayo ipo kwenye FORESTER ambayo kazi yake ni kuongeza ufanisi zaidi katika kukabiliana mazingira ya barabara zenye Changamoto sana na kufanya safari zako kuwa za kusisimua.

TUZO: Canadian Utility Vehicle of the Year, New Zealand Car of the Year Award. FORESTER haikupa tuzo hizi kwa bahati mbaya ni kutokana na ufanisi wa utendaji, Usalama na muundo wa kisasa kabisa 👏👏👏

UTULIVU
Utulivu wake ni mzuri sana kwenye barabara za lami na za vumbi kutokana na uwiano mzuri wa umbo lake pamoja na muundo wa chasis.

CHANGAMOTO
Gari hii tofauti na nyingine haivumilii oil tofauti na iliyoshauriwa na mtengenezaji. Hakikisha unaipa oil yake usije kuua injini

BAJETI
Unaweza kuimiliki SUBARU FORESTER NEW MODEL 4th generation kwa bajeti ya kuanzia TSH 30M mpaka TSH 35M

HITIMISHO
Sifa zake ni nyingi nimalizie kwa kusema zipewe tu maua yake. Kama mfuko wako unaruhusu njoo tukuagizie🌺🌺🌸🤗

Elimu hii fupi imetolewa na YETU MOTORS ambao ni washauri na waagizaji magari wenye ofisi

Mbeya: Mwanjelwa Soko Jipya
Mwanza: PSSSF PLAZA
Dar: Golden Jubilee Towers

IMG-20241013-WA0003.jpg
IMG-20241015-WA0004.jpg
 
Mkuu YETU MOTORS CO LTD asante Sana Kwa mada yako hii..
Mimi natumia Subaru forester XT/ SH ENGINE ya mwaka 2009.

Castrol oil ndiyo recommended by manufacturer na Mimi mara ya Kwanza nimetumia hiyo oil Yao,nimejaribu kutafuta engine oil kama ya mwanzo madukani hakuna nimeona Aina nyingine mpya za Castrol ingawa sijui UBORA WAKE
IMG_20241003_102544.jpg
hii ni Aina Mpya ambayo unaweza kutumia Hadi kwenye hybrid
IMG_20241003_102534.jpg
 
Mkuu YETU MOTORS CO LTD asante Sana Kwa mada yako hii..
Mimi natumia Subaru forester XT/ SH ENGINE ya mwaka 2009.

Castrol oil ndiyo recommended by manufacturer na Mimi mara ya Kwanza nimetumia hiyo oil Yao,nimejaribu kutafuta engine oil kama ya mwanzo madukani hakuna nimeona Aina nyingine mpya za Castrol ingawa sijui UBORA WAKE View attachment 3125628hii ni Aina Mpya ambayo unaweza kutumia Hadi kwenye hybrid View attachment 3125629
Hii gari unaisukuma sh ngapi?
 
Kuna wenye muscle na uwezo wa kumudu brand nyingine. Humu hatulingani kiuchumi. Uchumi wa chini mara nyingi uwezo wetu ni Toyota.
Mkuu Mimi na wewe tunaweza kumiliki brand tofauti na Toyota, haya maisha ya kumiliki Toyota yalikuwa zamani.
Mimi binafsi sina misuli mikubwa ya pesa lkn natumia brand tofauti na Toyota pia ni maamuzi Tu ya MTU kutumia brand tofauti.
Uwoga wa maisha Tu ndiyo unatufanya tuamini Toyota ndiyo kilakitu
 
Mkuu Mimi na wewe tunaweza kumiliki brand tofauti na Toyota, haya maisha ya kumiliki Toyota yalikuwa zamani.
Mimi binafsi sina misuli mikubwa ya pesa lkn natumia brand tofauti na Toyota pia ni maamuzi Tu ya MTU kutumia brand tofauti.
Uwoga wa maisha Tu ndiyo unatufanya tuamini Toyota ndiyo kilakitu
Upo sahihi kabisa. Lakini ukiangalia discussion zetu nyingi humu, ni gari za low budget. Gari ya 15+ years plus ndo tunaita new model.
Go figure.
 
Tatizo la kuunguza gasket limeisha kwenye hizo Foresta?
Mkuu hakuna gari iko perfect Kwa kilakitu.. kumbuka kila gari linahitaji matunzo Sahihi... forester zina matatizo hayo ya kuunguza cylinder head gasket hiyo inatokana na sababu nyingi hasa kwenye service
 
Back
Top Bottom