Pitia hapa, kama unapenda kufanya biashara mtandaoni (Drop shipping), na hatimaye tuwe na online store ya ukweli Tanzania

Pitia hapa, kama unapenda kufanya biashara mtandaoni (Drop shipping), na hatimaye tuwe na online store ya ukweli Tanzania

Kaudunde Kautwange

JF-Expert Member
Joined
Nov 15, 2011
Posts
1,644
Reaction score
1,648
Habari wadau!

Hope mko poa kabisa, na kwa neema za Mungu tunatumai atatuvusha mwaka salama, kwa wale ambao ni wagonjwa na wenye shida mbalimbali, basi ni maombi yangu kwa Mungu wa Mbinguni akuponye na kukupatia wepesi kwa yale unayopitia.

Teknolojia inakuwa kwa kasi sana, na kila siku mambo yanabadilika, mathalani watu wako bize na michakato ya Maisha, na hawako tayari kabisa kupoteza muda kwenye mambo ambayo yanawezekana yakafanyika kwa kurahisishwa na ukuaji wa teknolojia.

Jinsi siku zinavyozidi kwenda, biashara nyingi sana zinahamia kwenye wimbi la teknolojia, ukianzia namna ya kufanya malipo (Online payment) hadi namna ya kununua bidhaa (Online Purchase), itafika kipindi watu watakuwa kila kitu wana nunua kupitia mtandano, yaani hakutakuwa na utamaduni tena wa kupoteza muda kulifuata duka.

Vijana wengi sana tunatamani kuingia kwenye ufanyaji wa biashara kwa njia ya mtandano lakini tunashindwa kutokana na sababu mbalimbali. Kwa msingi huo basi, leo nimekuletea njia rahisi ambayo mimi na wewe tunaweza kuungana na kuwa na Drop shipping iliyoshiba kabisa, na hatimaye tukampiku Kikuu.

Drop shipping ni namna ya ufanyaji wa biashara bila ya kuwa na stock, yaani wewe unakuwa kama mtu wa kati tu kwa bidhaa Fulani, lakini Jukumu lako Zaidi ni kuhakikisha unapata wateja wa hiyo bidhaa yako kwa kuhakikisha unafanya marketing iliyoshiba haswaaa..

Sasa hapa, nimekuja na njia rahisi kabisa, nime design website ambayo naweza sema ndio platform haswaa ya kuuzia bidhaa kwa njia ya Drop shipping (Sheria zinabana, nione PM nikupatie link), Sasa fuatana nami..

Website

Nime design website ambayo ndio itakuwa haswaa Platform yetu sisi Drop Shippers wachanga. Na jinsi ya kutumia hii website ni rahisi mno, na inaeleweka sana.

Kupitia website hii, utapata fursa ya kuwa na store yako, ntakuelekeza namna ya kuweka bidhaa zako toka AliExpress, na mitandao mingine, lakini pia ntakuelekeza namna ya kuchagua bidhaa na kuzielezea kwa lugha rahisi. Pia nimeweka njia za malipo za uhakika kabisa, mtu anaweza kulipa kwa kutumia M PESA, TIGO PESA au MasterCard

Namna ya kupata bidhaa

Hapa kuna Platform ntakuelekeza, yenye kukupatia uwezo wa ku upload bidhaa hadi 150 for free toka AliExpress na mitandao mingine.

Gharama

Huduma hii ni bure kabisa, lakini unatakiwa uwe serious na ujue nini unafanya, cha Zaidi sana ni kujitoa kwenye ku market product yako.

Angalizo:

Wengi watasema natafuta namna ya kuitangaza site yangu, hapana, wewe utaitangaza store yako tu, na kumbuka nimeamua kujitolea kwa hili, ili kwa pamoja tuwe na Drop Shipping yenye uhakika Zaidi.

Mawasiliano:

Email: dngonyani89@gmail.com

Calling/SMS/WhatsApp: 0656142433

Update

Kwa ambao mko interested, nime create link ya WhatsApp... karibuni sana


 
Back
Top Bottom