Matanga
JF-Expert Member
- Nov 13, 2019
- 2,281
- 3,976
Juzi ijumaa nilirudi nyumbani mchana kwa lunch na kuona watoto. Baada ya lunch na kuwahudumia kidogo nikarudi kazini.
Baada ya nusu saa dada yao akanipigia kuwa Gerry (my first born) haonekani nyumbani. Nilikuwa kwenye mkutano muhimu sana kwangu.
Nikatoka na kumpigia dada yao amtafute mpaka kwenye makabati maana anapenda tabia ya kujificha.
Hapo nilikuwa nafanya taratibu za kuomba udhuru na kumuachia mtu majukumu yangu. Baada ya kupata ruhusa nikaelekea kwenye gari ili nikasaidie kumtafuta. Kufungua gari nilipiga yowe la taharuki.
Nilimkuta mtoto akiwa anatoka jasho sana, amechoka, kwa kifupi alikuwa hoi. Hii ni kutokana na kukosa hewa kwa muda. Alipatiwa huduma ya kwanza, muhimu ilikuwa ni kupata hewa safi. Niliogopa sana, nilipata mshtuko mkubwa. Mpaka leo nikikumbuka nahisi vibaya.
Baada ya yeye kupata nafuu nilimuomba aniambie ilikuwaje. Akaniambia alivyoona naenda kazini alitangulia kwenye gari akajificha siti ya nyuma chini. Then akapitiwa na usingizi. Aliamshwa na joto kali ikabidi achukue documents zangu achane ajifutie jasho. Then akawa anachoka. Alipita uncle alimuita ila hajasikia. Ndo anaishia kusema hivyo.
Wapendwa nime share na nyie ili tuwe makini na watoto wetu. Ni watundu sana. Tukague magari yetu ndani na chini kabla ya kuondoka.
Namshukuru sana Mungu kwa maana bado ametaka niwe na mtoto huyu hadi leo.
..it's a true story
Sent using Jamii Forums mobile app