Pitia uzi huu ujifunze umuhimu wa kukagua gari kama una watoto wadogo

mwamwala iyunga, Bila kusahau wale watoto unakuta kaingia chini ya uvungu wa gari anacheza.

Kuna mbaba aliwahi kuua mtoto, hakujua kama kaigia chini ya uvungu anacheza.

Kawasha gari kumbe kamkanyaga kuja kuchungulia mtoto, kichwa hakieleweki na alifariki pale pale.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tahadhari ingine ni hii hakikisha unafunga ile child lock siku moja mtoto wangu alifungua mlango wa nyuma wakati gari linatembea ingelikua sinaangalia kioo cha pembeni kile cha dereva kijana angedondoka..na ningemkanyaga na tairi
Utaendeshaje gari bila ya kumweka mtoto kwenye car seat?
 
mrangi,
Hiyo ni child neglect and endangerment, huyo mama alitakiwa aswekwe ndani.
 
Watoto ni watundu , Huu utundu inatakiwa uendane na fimbo. Usimnyime mtoto fimbo. Mpe fimbo za kutosha mpaka ashibe. Mana Kuna mwingine nasikia kameza mia tano hapa.

Sent using Jamii Forums mobile app

Binafsi watoto ni watundu lakini pia malezi sometimes yanachangia mimi mtoto wangu hasogelei gari yangu kama hamuhusu kupanda kwa wakati huo. Maana nimeshamuekea mipaka anaelewa nini kinamuhusu kwa wakati gani na kipi hakimuhusu, ila tusilaumu sana watoto wengine pia sugu sana.

Kwahiyo mtoto unavyomuacha ananing'inia kwenye gari lako ovyo ovyo ndio mwisho wa siku anaishia huko kwenye kujilaza.
 
Mchezo wa kujificha ni mchezo wa kawaida kwa watoto wote duniani, huwezi kumlaum mzazi kwa hilo.....ni bahati mbaya tu imetokea. Tunachotakiwa ni kuwa makini tu
 
Tahadhari ingine ni hii hakikisha unafunga ile child lock siku moja mtoto wangu alifungua mlango wa nyuma wakati gari linatembea ingelikua sinaangalia kioo cha pembeni kile cha dereva kijana angedondoka..na ningemkanyaga na tairi
Dah! Umenikumbusha ilinitokea juzi,nilimpa dogo vitasa vya kutosha...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…