Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
Kitabu cha Khamis Abdulla Ameir kimezinduliwa leo asubuhi.
Hapo chini ni sehemu ya kwanza ya pitio la kitabu hicho:
PITIO LA KITABU CHA KHAMIS ABDULLA AMEIR: ‘’MAISHA YANGU MIAKA MINANE NDANI YA BARAZA LA MAPINDUZI KHAINI AU MHANGA WA MAPINDUZI?’’
Kitabu chochote cha historia ya mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka wa 1964 ni kitabu kinachogusa hisia za watu wengi kuanza wale waliokuwapo lakini hawakushuhudia pili wale waliokuwapo na wakashuhudia hadi kizazi cha sasa ambacho hawakupo na wala hawakushuhudia.
Hawa wanaijua historia ya mapinduzi kwa simulizi zake kwa kuhadithiwa na waliokuwapo na kusoma katika kitabu kama hiki.
Baadhi ya vitabu hivi ni vya kutisha kama zilivyo simulizi za mapinduzi.
Yawezekana vipi mtu akatishwa na kitabu ilhali kitabu ni kitu ulichokishika mkononi pengine uko katika ukumbi wa nyumba yako na una kikombe cha kahawa mkononi unakunywa?
Inaeleweka mtu akisema kuwa senema fulani inatisha. Senema hakika inaweza ikatisha na watengenezaji wa filamu huweka ilani wakatahadharisha watazamaji kuwa filamu hiyo inatisha.
Filamu kiasi itishe kwa kuwa watengenezaji filamu wao hutengeneza jambo la zamani linalotia hofu wakalirejesha kwako likawa kama vile jambo lile pale unapolitazama likawa kama ndiyo muda ule linatokea na wewe unalishuhudia.
Bahati mbaya ubongo wa binadamu haujaweza kupambana na hili kwa akili kujiambia, ‘’Usiogope hii si kweli huo ni uigizaji tu hakuna maiti inayofufuka usiku ikatoka kaburini kwake ikaja Stone Town ikaingia ndani ya nyumba kupitia tundu ya kitasa ikaua watu kwa kutumia kisu kirefu chenye ncha kali kisha ikatoweka kurejea kaburini kwake.’’
Mimi naweka ilani katika kitabu hiki kuwa kinatisha. Katika kila pakiti ya sigara huwekwa ilani kwa mvutaji kumuonya kuwa kuvuta sigara ni hatari kwa afya yake.
Nami natoa tahadhari kuwa kitabu hiki cha Khamis Abdulla Ameir kinatisha.
Tutaona huko mbele In Shaa Allah ni waandishi gani ambao vitabu vyao vina historia ya mapinduzi inayomuhofisha msomaji.
Waandishi wa historia ya mapinduzi ya Zanzibar wamegawanyika katika makundi manne.
Kundi la kwanza ni kundi la waandishi wasomi kutoka nje, Ulaya na Marekani. Kwa muda mrefu uandishi wa historia ya mapinduzi ya Zanzibar ulitawaliwa na waandishi wageni wakiandika historia ambayo hawakupata kuishi ndani yake wakiandika kwa kutegemea utafiti.
Waandishi hawa wameandika historia za watu ambao hawakupata kuwaona wala kuwajua si kwa mbali wala kwa karibu.
Kipindi hiki kilianza mara tu baada ya mapinduzi. Kundi la pili ni la waandishi Wazanzibari wenyewe ambao nimewapa jina, ‘’Waandishi Mapinduzi Daima’’ na nimewaongezea jina lingine la Kiingereza nawaita ‘’Waandishi ‘’Pick and Choose,’’ yaani kalamu zao zinachagua kuandika yale yanayowapendeza wao na viongozi wa serikali inayoongozwa na Baraza la Mapinduzi.
Waandishi hawa wanaweza kuandika historia ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwa sentensi mbili ikawa kamaliza kila kitu.
Bahati mbaya sana historia ya waandishi hawa ndiyo kwa miaka mingi imekuwa historia rasmi ya mapinduzi ya Zanzibar.
Baada ya waandishi hawa na baada ya kipindi kirefu kupita likaja kundi la tatu kundi la ‘’Waandishi Mavamazi,’’ ikiwa na maana kuwa wao msimamo wao ni kuwa hapakuwa na mapinduzi bali mavamizi ya Tanganyika kuivamia Zanzibar kwa silaha wakitumia mamluki wa Kimakonde kutoka Kipumbwi, shamba la mkonge la Sakura Tanga kuongoza na kuongeza nguvu ya wanamapinduzi wa Zanzibar kupindua serikali halali.
Waandishi hawa wameandika historia ya mapinduzi wakiwa wamehama Zanzibar miaka mingi iliyopita baada ya mapinduzi na ikiwa unapenda, ‘’mavamizi.’’
Waandishi hawa wamejitahidi sana kuondoa pazia la usiri uliokuwa umegubika mengi yaliyopitika katika mapinduzi.
Hawa wameeleza jela za mateso na mauaji kuwa sehemu ya uendeshaji na utawala wa serikali ya Baraza la Mapinduzi.
Hawa ‘’Waandishi Mavamizi,’’ wamekwenda hatua moja mbele kwa kuongeza simulizi juu ya uandishi a vitabu. Simulizi hizi zimeweka wazi mengi katika mapinduzi kupita vitabu vyote vilivyoandikwa kabla.
Kwa kuhitimisha nukta hii ningependa kuchomekeza hapa kuwa Khamis Abdulla Ameir juu ya kuwa na mengi katika historia ya mapinduzi katika kitabu chake anasema hana taarifa ya Wamakonde walioingia Zanzibar kusaidia kupindua serikali ya ZNP/ZPPP.
Mwisho kwa sasa ni kundi la nne la waandishi niliowapa jina, ‘’Waandishi Wasahihishaji,’’ ambao hawa wamejaribu kuweka wazi kila kitu katika historia ya mapinduzi ya Zanzibar ili yaeleweke yote yaliyopitika ambayo waandishi waliotangulia hawakuyaandika ama kwa kutoyajua au kwa kuyaficha.
Mlango wa staili ya uandishi huu ulifunguliwa mwaka wa 2010 na Dr. Harith Ghassany kupitia kitabu chake, ‘’Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru.’’
Baada ya kitabu cha Dr. Harith Ghassany pakapiga ukimya kwa ‘’Waandishi Wasahihishaji,’’ hadi alipotokea Hashil Seif na kitabu chake, ‘’Mimi Umma Party na Mapinduzi ya Zanzibar.’’
Baada ya kitabu hiki ndiyo ameingia Khamis Abdulla Ameir na kitabu hiki ‘’Maisha Yangu.’’ Khamiis Abdulla Ameir amebeba lakabu ya ‘’Theoretician,’’ yaani ‘’Mjuzi,’’ kitu aghlabu kwa wanasiasa wa Zanzibar kuwanacho.
Hulka ya kujipa majina au kupewa majina imezoeleka kwa wanasiasa kutoka Tanganyika na kwa hakika Afrika yote kujipa majina yanayoashiria ukubwa na ubingwa kama vile ‘’Mwalimu,’’ ‘’Baba wa Taifa,’’ ‘’Simba wa Vita,’’ ‘’Kambale’’ nk. ni mambo yaliyozoeleka.

SEHEMU YA KWANZA