Pitso Mosimane Kutimuliwa Al Ahly muda wowote kuanzia sasa

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426

Hii ni kwa sababu ya mwenendo mbaya wa timu yake kwenye ligi ya mabingwa, Al Ahly hivi sasa haina tofauti na Mbeya City, ule uwezo wake wa kutandaza soka umepeperuka utadhani njiwa wa uganga.

Kwa kadri ninavyowafahamu Waarabu akishindwa kutinga nusu fainali ya ligi ya mabingwa atatimuliwa bila huruma.
 
Hili likitokea basi Wachezaji watakua wamefanikiwa kutimiza azma yao. Wale hawataki kuongozwa na yule Msouth ndio maana wanacheza chini ya kiwango ili jamaa aonekane hafai.
 
Ila Bongo raha sana wachambuzi wetu wanatafsiri kiingereza kwa kutumia dictionary na sio context. Juzi kocha Gomez kuhusu Morrison kutoenda Sudan kocha anasema "Simba Club is like a family" mwandishi akauliza kwa nini Morrison hakuenda, kocha akajibu "It's a family matter". Kitenge kashikilia bango ni suala la kifamilia ๐Ÿšฎ๐Ÿšฎ๐Ÿšฎ
 
Pitso anajua, aliwatandika hao waarabu wakiwa na kocha mzungu goli 5, waarabu hawampendi bila sababu, game yao na Vita walipoteza nafasi nyingi za wazi na hilo sio kosa la kocha.
 
Inawezekana kuna hujuma anafanyiwa na wachezaji. Pengine hawamtaki hawaoni kama ana lolote jipya kwao. So wanahitaji kochwa wa juu zaidi. Ile ni club tajiri.
Uwezo wao umeishia hapo! Kama uwezo wa Utopolo ulivyofikia mwishoni! Hata ukiwaletea Gurdiola hamna kitu! Hali kadhalika uwezo wa wachezaji wa Al Ahly umefikia kikomo!! Kama wakitaka kumtumia vizuri huyu kocha, wampe nafasi ya kutafuta wachezaji ambao anataka wasajiliwe
 
Ha ha ha haa
Hata Mimi ndiyo naielewa hiyo kauli sasa hivi
 
๐Ÿ˜€ ๐Ÿ˜€Kitenge kiingereza kwake mzozo...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ