Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,761
- 216,011
Ni kaka wa ndizi, hupikwa zikiwa mbichi au zimeiva.
Zina kiwango cha potassium mara mbili zaidi ya ndizi za kawaida
Jinsi ya kupika mzuzu wa nazi
Mahitaji
Ndizi 6
Nazi
Iliki
Safron
Unga wa mchele vijiko 3 vya chakula
Ghee kijiko kimoja cha chakula
Chumvi na sukari kiasi unachopenda
Upishi
Menya ndizi zitoe moyo na ukate size unayopenda
Loweka kwenye safron
Kuna nazi, weka tui la pili jikoni na ndizi, piga tui lisikatike,
Twanga iliki weka iliki ndani
Koroga unga wa mchele kwenye kijombe cha maji, hakikisha hauna mabonge weka kwenye ndizi endelea kupiga tui lisilete mabonge.
Weka tui bubu
Weka ghee (kama unapenda) hasa kama huna wasiwasi wa unene
Weka chumvi na sukari kama ndizi hazina sukari ya kutosha.
Tui likiiva okoa sufuria jikoni.