Plaza de la Revolución: Jela za siri, ndogo na zilizotisha chini ya jengo la wanamapinduzi wa kweli. It's now Cuba's Ministry of the Interior

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Joined
Feb 18, 2012
Posts
15,892
Reaction score
16,476
Plaza de la Revolución: Jela za siri, ndogo na zilizotisha chini ya jengo la wanamapinduzi wa kweli. It's now Cuba's Ministry of the Interior.



Habari za wakati huu kaka na dada zangu wote wa hapa JamiiForums.

Hilo jengo unaloliona hapo juu, lenye picha kuuuubwa ya Ernesto "Che" Guevara swahiba mkubwa wa comrade Fidel Castro Ruz pamoja na bendera ya taifa Cuba, ni lile linalojulikana kama "Plaza de la Revolución".

Kwa kiingereza tunaweza kusema ni "Revolutionary Plaza" au "Jengo la Mapinduzi" kwa lugha ya Kiswahili.

Hapo awali lilijengwa na kampuni ya taifa ya bima ya Cuba, na kisha likachukuliwa na idara ya polisi wa siri (usalama wa ndani) baada ya Mapinduzi yaliyotokea nchini humo.

Haraka sana likawa jengo linalotazamwa kwa hofu kubwa na Wacuba. Kizuizi chake kidogo, chenye ghorofa mbili katika chumba cha chini cha jengo hilo kilikuwa sehemu ambapo wapinzani na maadui wa kisiasa wa utawala walifichwa.

Watuhumiwa wa wapelelezi (spies), na watu walioshutumiwa na wengine kama maadui wa taifa pia walichukuliwa na kushikiliwa kwa uchunguzi zaidi kitengo cha polisi wa siri wa Cuba (Cuban Secret Police).



Kama ilivyoandikwa na kusimuliwa na wengine ambao walinusurika katika mchakato wa kuhojiwa - neno jepesi ninaloweza kutumia mbadala wa mateso (torture) - "Plaza" ilikuwa kama kuzimu kwa wale waliochukuliwa na kufichwa huko.

Mwanadiplomasia wa Uingereza na mpelelezi Vitalis Bruce mnamo mwaka 1983 katika kupanga njama za kupindua utawala wa Castro alitoweka ndani ya "Plaza".

Baadaye ilikuja kufahamika ya kwamba wapelelezi, ambao walikuwa wamefanya sana kazi za ujasusi kwa niaba/udhamini wa serikali ya Waingereza, waliteswa na kuhojiwa huko nchini ya "detention cells" za "Plaza" kabla ya kupelekwa msituni nje kidogo ya jiji la Havana na kupigwa risasi.



Maafisa wengi wa Jeshi la Cuba lililokuwa linafanyiwa safisha safisha kwa kuondoa mamluki wa Marekani na dunia nzima ya ubeberu mnamo miaka ya 1970 walitembea kupitia milango huko "Plaza" na kamwe hawakurudi teeeeena katika familia zao.

Asubuhi ya Oktoba 19, 1988 Miguel Sanchez, mwanaharakati wa siasa za mageuzi nchini humo (Cuba) alifika katika ofisi ya Havana ya Ubalozi wa Canada kwa mashauriano juu ya kuomba hadhi ya hifadhi ya kisiasa nchini Canada.

Ilipofika Saa 1 jioni aliacha vitu vyake ofisini na kwenda nje kununua kahawa na fitafunwa kidogo kwa ajili ya kuchangamsha mwili wake. Miguel hakurudi tena.

Mlinzi wa Ubalozi wa Canada aliona wanaume kadhaa wakiwa wamevalia mavazi ya kiraia wakimsukuma Miguel kwenye gari ndogo. Alijaribu kuwazuia, lakini walimsukumia mbali. Watu wasiojulikana wakaondoka na Miguel.



Fidel Castro aliitawala Cuba kwa miaka 30. Utawala wake ulikuwa na tuhuma nyingi sana za ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu na ukandamizaji wa kisiasa kwa jumla.

Vyombo vyake ya usalama wa ndani (Dirección de Inteligencia, DI) vilishutumiwa kwa kukandamiza kikatili aina yoyote ya wapinzani wa kisiasa. Serikali yake ilishutumiwa kujenga vyumba maalum vya kufanyia mateso katika upande wa chini cha jengo la "Plaza".

Jengo hili lililokuwa linamilikiwa na serikali katikati mwa jiji la Havana ambalo sasa linakaliwa na idara ya uhamiaji. Serikali ya sasa ya Cuba ilitoa ahadi ya kuibadilisha "Plaza" kuwa makumbusho, ahadi ambayo mpaka sasa bado haijatimizwa.



NB: Hivi unajua kwamba C.I.A walipanga operation ya kumpindua Fidel Castro almaarufu kama "Bay of Pigs Invasion" wakiwa gereji? Yaaani jengo maarufu la ghorofa mbili chini ni gereji ya magari ila juu ni ofisi za C.I.A huko Florida nchini Marekani? Kujua mkasa huu fuatiliana nami katika episode inayofuata ya "Revolutinary Plaza"

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
 
Hata hapa kwetu zipo ila zamani zilitumika sana enzi ya nyerere na mwinyi ila saa hivi hupelekwi tena huko wanamalizana na wewe siku hiyo hiyo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…