Infantry Soldier
JF-Expert Member
- Feb 18, 2012
- 15,892
- 16,476
Mimi ni kijana niliyehitimu elimu ya chuo kwa miaka kadhaa iliyopita. Kwa ukweli nimekuwa nikiishi maisha unyonge wa hali ya juu sana kutokana na background ya maisha ya familia niliyokulia. Kwa kweli tumekulia maisha ya hali ya chini mno!
Ukinunuliwa nguo moja leo ndio mpaka ipite miaka mitatu ndio upate nyingine. Ukienda shule haupewi hela ya matumizi hata senti tano. Na hii ilipelekea mpaka kuanza kujisikia mpweke na kuanza kuishi maisha ya peke yangu kwa kuwa wenzangu walikuwa wanatoka familia bora na kupata at least mahitaji yao muhimu kwa kiwango kizuri kabisa.
Nikawa nafikiri kama rafiki zangu na jamii inayonizunguka huwa inatucheka kwa ufukara tulionao mpaka ikapelekea kupoteza mahusiano mema na rafiki zangu wa jinsi zote za kike na kiume na hili tatizo limeacha kovu kubwa sana ndani ya akili yangu, naombeni msaada ndugu zangu!
Asanteni.