Please help me...

Please help me...

ISIMBA

Senior Member
Joined
Feb 7, 2013
Posts
144
Reaction score
30
Habarini za jioni wakubwa, nina mwanangu mdogo wa kiume mwenye umri wa miaka mitatu na nusu.

Huyu dogo kiukweli simuelewi naona kama mambo yake ni ya kikekike, mara anabeba midoli mgongoni kama mtoto, ukipigwa muziki, staili yake ya kucheza anajibinua anacheza kama anataka kubambiwa, mwenzake akilia anambeleza kama mama yake huku akimwambia nyamaza mwanangu, anapenda sana kuwaita watoto wenzake mwanangu.

Anapenda sana kuiga mambo ya kike kuliko ya kiume.

Swali langu mimi ni kwamba hivi kuna uwezekano huyo dogo akaja kuwa shoga ukubwani?

Na kama ni hivyo, nifanye nini ili huyu dogo abadilike? Hili jambo kiukweli linanifanya nakosa raha kila nikimwangalia huyu dogo.

Nisaidieni wakubwa...
 
Acha fikra potofu...mtoto anakuwa na nani muda wote?Let me guess ni mama au dada wa kazi na kuna uwezekano mkubwa pia watoto wenzake(agemates)anaocheza nao ni wa kike na ndio maana anaiga michezo ya kike.Watoto wanaiga na kufata rollemodels wao kimatendo.
Watoto wanazaliwa tofauti kitabia na kama nilivyosema awali mazingira yanaaffect pia.Wapo baadhi wanazaliwa na tabia za kike au za kiume from day 1 wanajiexclude.
Kiutaalamu mtoto anatakiwa apewe options za toys zote za kike na za kiume mfano magari na midoli,hii ni vizuri kwaajili ya makuzi ya huyo mtoto ili ajifunze knowledge ya vitu tofauti.
 
shukran mkubwa, ni reality kwamba huwa anashinda na dada wa nyumbani na watoto wa jirani ambao ndo rafiki zake ni wa kike, so nimepata point hapo na ntachukua hatua...
 
Usiwe na woga bado mdogo sana huyo, ni makuzi tu ya kawaida.
 
Back
Top Bottom