Maelezo murua kabisa haya, highly recommended!, unless labda kama mleta uzi kuna kitu anatuficha hapa..Mbona una complicate hii issue, huyu ni rafiki yako ambaye inaonekana anakuamini kwa mmesoma pamoja na mnaelewana.Inavyo onekana anakukubali wewe binafsi, hivyo anaamini kuwa marafiki au watu unaotangamana nao watakuwa watu safi.
Kwa sababu hiyo kuliko yeye kuanza kujaribu jaribu bahati kwanini asikuombe wewe umsaidie katika kuchuja na kumuunga kwa kati ya washikaji zako ambao unaona wataendana nae?
Inawezekana ameshawahi pata tatizo kwenye mahusiano ndio maana anataka umsaidie.
Jamani lazima mjifunze kuaminiana na kusaidiana hata kwa jinsia tofauti, sasa nini maana ya kusoma pamoja na kuwa marafiki kama huwezi kumsaidia kwenye issue sensitive kama hiyo? Sio kila saa kufikiria kumega, kumegwa tu!
Nakushauri kaa nae msikilize anataka mtu wa aina gani na kama una washikaji ambao wako serious kuoa, basi waunganishe na waambie kabisa wao ndio wafanye final decision kama watakubaliana.
Hivi utajisikiaje siku unakutana na familia ambayo wewe ndio uliwaunganisha? Ni kitu kizuri sana na utapata baraka nyingi sana.
Msaidie bana...
"Najua sisi ni marafiki kwa muda mrefu sasa, unaweza ukafahamu kwa ufupi historia yangu ktk suala zima la uhusiano/mapenzi . Samahani kama nitakuwa nimekukwaza, NAOMBA NITAFUTIE MCHUMBA WA KUNIOA. Please, naomba uwe serious". Ni ujumbe ambao nilitumiwa wiki tatu zilizopita na dada mmoja ambaye tulisoma sekondary{ a-level) kule Ndanda, zamani kidogo. Tukakutana tena chuo baada ya miaka kama sita hivi. Anaishi Mwanza kikazi. Nami niko Dar. Lakini message hiyo ya dada yangu mwanzoni niliona kama utani tu na sehemu ya utani wa marafiki mliosoma pamoja. Lakini kinachonitatiza dada yangu huyu karibu kila siku ananiuliza kama nimemtafutia huyo mchumba? Na anasisitiza huku akionesha kuwa hatanii. Binti ni mrembo kwa kweli na ana kazi nzuri tu. Sidhani kama mwenyewe hakuna vidume vinavyompiga promo. Najisikia vibaya anapoingiza hili suala lake tunapozungumza. Nikimweleza kuwa huo utani sitaki huwa anan'gang'ania kuwa mimi ndo natania yeye hatanii. Wadau nimpotezee vipi huyu mdada? Au yuko serious kweli? Wakati mwingine huwa hadi ananikasirikia ninapomwambia kuwa sijamtafutia huyo mchumba!
Wa kuoa anatafutwa?
Mume mwema hutoka kwa Bwana, na kibaya zaidi vijana wa leo hakuoi hadi kwanza wakupime oil
Wabongo vitu used mbon ndio sera hata bungeni walipitisha sheria ya kununua vitu chakavu!Labda ishatumika sana anataka kumkamatia mtu. Jiangalieni, mi simo!
sijaoa, bado.
umri wake please mkuu????
we mpige machine kwanza halafu endelea kumtafutia. kwasababu nijuavyo mimi siku hizi hatutafutiani mchumba. ukiona mtu wa jinsia tofauti na si ndugu yako anakuambia umtafutie mchumba pambanua vizuri. wengine wanahitaji kupigwa machine wao wenyewe kama huyu"Najua sisi ni marafiki kwa muda mrefu sasa, unaweza ukafahamu kwa ufupi historia yangu ktk suala zima la uhusiano/mapenzi . Samahani kama nitakuwa nimekukwaza, NAOMBA NITAFUTIE MCHUMBA WA KUNIOA. Please, naomba uwe serious". Ni ujumbe ambao nilitumiwa wiki tatu zilizopita na dada mmoja ambaye tulisoma sekondary{ a-level) kule Ndanda, zamani kidogo. Tukakutana tena chuo baada ya miaka kama sita hivi. Anaishi Mwanza kikazi. Nami niko Dar. Lakini message hiyo ya dada yangu mwanzoni niliona kama utani tu na sehemu ya utani wa marafiki mliosoma pamoja. Lakini kinachonitatiza dada yangu huyu karibu kila siku ananiuliza kama nimemtafutia huyo mchumba? Na anasisitiza huku akionesha kuwa hatanii. Binti ni mrembo kwa kweli na ana kazi nzuri tu. Sidhani kama mwenyewe hakuna vidume vinavyompiga promo. Najisikia vibaya anapoingiza hili suala lake tunapozungumza. Nikimweleza kuwa huo utani sitaki huwa anan'gang'ania kuwa mimi ndo natania yeye hatanii. Wadau nimpotezee vipi huyu mdada? Au yuko serious kweli? Wakati mwingine huwa hadi ananikasirikia ninapomwambia kuwa sijamtafutia huyo mchumba!
Huu ushauri nimeupenda!...Mwambie hivi.
"Nimekosa bana,ila hata mimi nafaa kuwa na wewe"........
then kaa pembeni mwachie mtihani mwenyewe.
So kutafuta mchumba siku hizi ni kama kutafuta gari eh?
nami ni bachela ani pm tuongee chemba, tukifikia muafaka tunaishi.mkuu msaidie tu au naomba uni pm.
miaka 31 Mkuu!