Ok kama ni prosperous one among the working class, sasa twende pamoja;
1. Tuliewe sawali,
Namna nzuri zaidi na rahisi ya kulielewa swali nadhani nikwanza kulitafsiri kwa lugha inayo eleweka zaidi - kiswahili.
Kwakiswahili swali lingesomeka
"yatosha kusema kuwa kipindi cha mapinduzi ya viwanda ulaya na hasa uingereza kilikua kipindi cha mafanikio miongoni mwa tabaka la wafanya kazi. Chambua tamko hili kwaundani.
2. Academic meaning ya swali.
Katika mazingira ya shule unapokutana na swali linalokutaka ku assess,discuss or critically analyze. Na maneno hayo kuwekwa mwisho wa swali, basi tambua utatakiwa kutoa maelezo yenye pande mbili, yaani Arguments FOR and AGAINST the statement.
3. Tujibu swali sasa
Katika swali tulilonalo utatakiwa kutoa points kwanza zinazo support statement ya swali, yaani points zinazo onyesha kuwa tabaka la wafanyakazi lilifaidika sana na kipindi hicho cha mapinduzi ya viwanda ulaya na Hass uingereza. Halafu Kisha utatoa point zinazo onyesha kuwa pamoja na kua kipindi cha mafanikio kwao kilikuwa na changamoto flani, sasa unaeleza changamoto za kipindi hicho kwa tabaka hili la wafanya kazi.
Comrade, natumai nimesaidia.